"Traffic" Nunua gari yako upande

"Traffic" Nunua gari yako upande

Hunyu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,774
Reaction score
4,339
Habari ya usiku wakuu. Poleni na majukumu ya siku nzima.

Leo nimekutana na hiki kisa cha huyu mama Traffic Police.

Nilikuwa natoka kwangu naingia mjini, kwa mbaali nikamuona traffic anaelekea ninakoelekea. Nilipomfikia nikampita tu sikusimama. Kwakuwa sikuwa speed, baada ya kumpita hatua chache nikajisikia moyoni kumpa lift yule mama traffic.

Kweli nikasimana na nikaanza kurudi nyuma ili nimfikie. Nilipomfikia, nikamuuliza anakoelekea akasema naenda pale sehemu(akaitaja) kwasababu kuna msafara. Nikamwambia, panda afande twende, kweli akapanda tukaanza kuondoka.

Baada ya story za hapa na pale mama akaanza kunishukuru kwa kumpa lift. Nikasema usijali mama wewe ni boss wangu.

Akasema, mwanangu pamoja na uaskari wangu huu, siwez kuomba lift ktk maisha yangu hata siku moja, nikauliza why, akasema iko iv. Kuna siku alisimamisha gari akiwa na uniform kwa lengo la kuomba lift, yule mtu alimjibu "NUNUA GARI YAKO UPANDE" anasema toka siku iyo hawezi kuomba lift kwa jinsi alivodhalilishwa.

Nilishangaa na nikajisikia vibaya sana kwa majibu hayo alojibiwa yule mama traffic.

Wadau, je ni sahihi kweli hata kama wanakera hawa askari?
 
Mi huwa sioni sababu yakuwanyima. Wapo ambao wanafanya kazi zao kwa haki na wapo waoneaji poa
 
Lala tu ila kesho uje kujibu tuhuma za kumpa hongo mtumishi wa uma, kitendo kinachotafsiriwa kama kumziba mdomo ili siku ukicommit crime barabarani akudeffend!
 
Anunue lake ndio....

Mkuu aisee kauli zingine ni kali mno, kwann usinjibu kistaarabu tu? Huwez jua kesho kitatokea nn, hatupashwi kulipa ubaya kwa ubaya
 
Lala tu ila kesho uje kujibu tuhuma za kumpa hongo mtumishi wa uma, kitendo kinachotafsiriwa kama kumziba mdomo ili siku ukicommit crime barabarani akuoffend!

Mkuu mbona hata simfaham na yeye hanifaham, na ndani ya dak chache sikumkalili hata sura yake na yeye naamini vilevile. Nilifanya kiroho saaaaafi kabisa bila kutarajia malipo yeyote.
 
hii heading na wakati naanza kusoma nikadhani wewe ndio ulimwambia hivyo....kiukweli mwisho wa siku linapokuja suala la utu,haliangalii umevaa uniform gani ama unafanya kazi gani...
 
Mkuu mbona hata simfaham na yeye hanifaham, na ndani ya dak chache sikumkalili hata sura yake na yeye naamini vilevile. Nilifanya kiroho saaaaafi kabisa bila kutarajia malipo yeyote.

Ngoja nikumegee siri kuna mmoja anasimama (panahifadhiwa kwa sasa) kwa kuwa mimi si msemaji wa familia yake...ila for sure ukimpa ride hutojutia muda wako...in fact ana faa sana kwa matumizi binafsi!
 
Hunyu umefanya jambo jema sana ubarikiwe. Huyo jamaa aliyemjibu ivo ana matatizo makubwa sana
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu gari kwake ni zaidi ya mtoto.anaona kamaliza yote.

Usishangae.
 
Haaa nyie hamjui traffic police walivyo washenzi, mimi simpi lift labda aniombe, kuna siku nilikuwa natoka bagamoyo Polisi aliomba lift nikampa lakin mle ndani tulikuwa na jamaa yangu tunakula samaki na mazagazaga mengine tukamnyima shenzi
 
Back
Top Bottom