Traffic Morroco jirekebisheni

Traffic Morroco jirekebisheni

Digaller

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
886
Reaction score
840
Heshima kwenu wakuu,

Kwanza nalipa pongezi jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ambayo wanafanya haswa kitengo cha usalama barabarani kwa kazi kubwa mnayofanya.

Pili ningependa kutoa ushauri kwa traffic mnaoongoza magari hapo moroco acheni hii tabia ambayo imeanza kuota mizizi, hivi mnawezaje kuruhusu magari ya upande mmoja nusu saa mzima na hakuna msafara wowote wa kiongozi unaopita?

Leo asubuhi mmetukalisha dakika 33 tunaotoka magomeni kwenda kawe na jioni pia mmefanya hivyo hivyo.

Afu hii tabia ya kukamata watu wanaowaambia ukweli imeanza lini?

Masikini mzee wa watu mmekalisha kwenye foleni almost 40 minutes, anakuja kuwaambia upupu mnaofanya sio fair mnamweka ndani.

Naomba kama mmeshindwa kuongoza magari basi acheni taa zifanye kazi yake na nyie mbaki hivyo hivyo kama mlivyojigeuza TRA.
 
Hapo Mkuu umesema Kweli wao wanaangalia gari zinazotoka Posta tu hasa jioni, Kuna siku watu walijaa hapo morocco nilihisi kuna maandamano kumbe magari yanayotoka kawe kupita kawawa yamesimamishwa masaa mawili
 
Mkuu walichofanya leo sio fair kabisa, asubuhi tumekaa dakika 33, jioni pia almost 40 minutes.

Kuna mzee kaenda kuwaambia upuuzi wanaofanya sio fair cha ajabu wamemkamata na kumweka ndani "what a shame".

Tunaliomba jeshi la polisi makao makuu waliangalie hilo jambo kwa jicho la pekee, hii tabia ya kuanza kubaguana kwa sehemu tunazofanyia kazi si jambo zuri hata kidogo.
 
Wajirekebishe aiseee...poleni sana watu wa Dar

Thanks, yaani na joto lote la Dar, afu ukifikiria unakoenda ni mbagala au gongo la mboto na umesimama kwenye gari asee roho inauma sana.

Kama wameupata huu ujumbe labda wanaweza kujirekebisha.
 
Thanks, yaani na joto lote la Dar, afu ukifikiria unakoenda ni mbagala au gongo la mboto na umesimama kwenye gari asee roho inauma sana.

Kama wameupata huu ujumbe labda wanaweza kujirekebisha.
kweli aisee, wajirekebishe
 
Back
Top Bottom