Traffic lights kona ya ITV zimeongeza jam

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,389
2,000
Yaani badala ya kusaidia kupunguza jam hizi taa hapa ITV junction zimeongeza kero aisee sijui nini wataalam wetu wameshindwa kutatua. Kwanini hata wasingewaza magari ya kutokea upande wa ITV yanayoelekea mwenge yakazungukie bamaga? Na Yanayotoka bamaga kuingia Mikocheni yakaingilie mwenge? Mbona ni jirani sana? Kama ubungo magari ya kutoka mawasiliano yanazungukia kijazi kwenda mwenge why hapo ITV hamjafanya hivyo badala yake mmeongeza jam?
 
Ubungo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
1,243
1,500
Hata Traffic light za Pugu, ni kero tu. Hapa mahali hapajawahi kuwa na msongamano lakini sasa upo wa kutosha hasa peak hours
 
Scaramanga

Member
Aug 19, 2020
55
125
Yaani badala ya kusaidia kupunguza jam hizi taa hapa ITV junction zimeongeza kero aisee sijui nini wataalam wetu wameshindwa kutatua. Kwanini hata wasingewaza magari ya kutokea upande wa ITV yanayoelekea mwenge yakazungukie bamaga? Na Yanayotoka bamaga kuingia Mikocheni yakaingilie mwenge? Mbona ni jirani sana? Kama ubungo magari ya kutoka mawasiliano yanazungukia kijazi kwenda mwenge why hapo ITV hamjafanya hivyo badala yake mmeongeza jam?
Yaani umesema ukweli kabisa.Ukiwa unatoka ITV au Sinza kuingia Bagamoyo Road ni adhabu .Taa zinaruhusu njia ya Mona tu ya Bagamoyo road muda mrefu utadhani hizi njia nyingine watumiaji hawahitaji endelea na safari zao.Badala kupunguza foleni zimekuja ongeza foleni .Trafik lights no mfumo wa zamani sasa hivi wabuni bypass ,fly over au keep left kubwa ambazo zinaweza kabisa ondoa tatizo.Sasa pita mlimani city kama unaenda ubungo foleni sababu ya taa.
 
isambe

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
2,195
2,000
Huko TZ,sijui hao wasomi wa mipango miji na wahandisi wanavyokwenda nchi zilizoendelea kama wanajifunza vitu kuhusu taaluma zao,au wanakuwa busy kushangaa na kujitwika makoti mazito kupooza baridi.sio lazima kila pahali uweke robots ( traffic lights),kuna sehemu nyingine wanatakiwa waweke round about kama pale junction ya tbc na Sinza walitakiwa waweke pia,lakini naona tumekuwa kama washamba wa taa hizo kila pahali.
 
Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,020
2,000
Nimeobserve sana hizi round about hupunguza tatizo la foleni kwa kiwango kikubwa sana. Laiti wangeweka round about pale sayansi, bamaga na ITV then mwenge pawekwe flyover tatizo la foleni lingeisha.

Tuangalie mfano pale msamvu Morogoro, bila Ile round about pale pangekuwa na foleni kubwa sana maana Ile barabara ipo busy mno lakini ukifika pale huwezi kunotice kama kuna magari mengi sana sababu ya Ile round about.
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,389
2,000
Huko TZ,sijui hao wasomi wa mipango miji na wahandisi wanavyokwenda nchi zilizoendelea kama wanajifunza vitu kuhusu taaluma zao,au wanakuwa busy kushangaa na kujitwika makoti mazito kupooza baridi.sio lazima kila pahali uweke robots ( traffic lights),kuna sehemu nyingine wanatakiwa waweke round about kama pale junction ya tbc na Sinza walitakiwa waweke pia,lakini naona tumekuwa kama washamba wa taa hizo kila pahali.
Wao wanajua mataa mengi ndo maendeleo yaani aisee wanaongeza jam kila sehem na awali hakukua na jam kama saizi
 
isambe

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
2,195
2,000
Kwa
Wao wanajua mataa mengi ndo maendeleo yaani aisee wanaongeza jam kila sehem na awali hakukua na jam kama saizi
wemzetu wanatumia hizo taa sehemu ambazo waenda kwa miguu ni wengi wanakatisha barabarani,lakini huko ndio wamezijulia kuzifunga basi kila maungio ni taa na matuta wakati ndio yanaharibu barabara
 
Manyema

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
364
500
Sinza huko ndo kero kabisa.
Sinza ni upuuzi mtupu kama pale Africa sana ndiyo hovyo kabisa, magari mengi yanatoka Bamaga kwenda shekilango cha ajabu taa inawaka sekunde 30 tu inazima mnasubiri dk 1 na nusu. Unakuta taa inawaka zinavuka gari tano sita inazima yaani. Sehemu nyingine ya hovyo ni pale Mugabe taa inaweza wasimamisha alafu hakuna hata anayevuka wote mnabaki mnaangaliana tu, maana ikiwaruhisu wale wanaotoka ile njia ya mawasiliano kule unaweza kuta hakuna hata gari moja. Something should be done
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,142
2,000
Ujenzi wa kipumbavu sana.. hata dhakilango road kuna mataa kibao.

Kikubwa subiri mataa ya kimara kibaha highway..

Imagine mataa sehemu hizi

Stop over, suka, temboni, kwa msuguri, mbezi mwisho, mbezi High, luguruni, kibamba hospitali, etc hadi kibaha kuna maeneo kama 30 yanayo wekwa mataa ya kuongoza magari.

Nadhani tanroad wameongezewa jukumu la kuremba mji.
Yaani badala ya kusaidia kupunguza jam hizi taa hapa ITV junction zimeongeza kero aisee sijui nini wataalam wetu wameshindwa kutatua. Kwanini hata wasingewaza magari ya kutokea upande wa ITV yanayoelekea mwenge yakazungukie bamaga? Na Yanayotoka bamaga kuingia Mikocheni yakaingilie mwenge? Mbona ni jirani sana? Kama ubungo magari ya kutoka mawasiliano yanazungukia kijazi kwenda mwenge why hapo ITV hamjafanya hivyo badala yake mmeongeza jam?
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,389
2,000
Ujenzi wa kipumbavu sana.. hata dhakilango road kuna mataa kibao.

Kikubwa subiri mataa ya kimara kibaha highway..

Imagine mataa sehemu hizi

Stop over, suka, temboni, kwa msuguri, mbezi mwisho, mbezi High, luguruni, kibamba hospitali, etc hadi kibaha kuna maeneo kama 30 yanayo wekwa mataa ya kuongoza magari.

Nadhani tanroad wameongezewa jukumu la kuremba mji.
Kwanza kituko cha pale mbezi mwisho junction ya goba na mbez kila siku nacheka mziki wa foleni utakaokuwepo maana kwa akili hizi za kuona taa ndo suluhu hakyanan tutajuta stendi kuhamia mbezi. Saizi tu foleni ya daladala inaanzia mbezi stand ndani kabisa...na njia ya goba stand hadi kona ya makabe...na hapa bado mziki kamili kuanza. Wasomi wetu kituko sana angalia tu foleni tu ya pale kimara korogwe yaani kitu kidogo tu kuchepusha stendi ya daladala wameshindwa matokeo yake miaka yote daladala zinasimama kupakia na kushusha katikati ya barabara zinatengeneza jam. Nahisi hawa Tanroads wanaendeshaga helicopter so hizi kero hawaziishi
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,389
2,000
Sasa tujiandae kisaikolojia maana hawa jamaa wanaamini traffic lights nyingi ndo maendeleo...baada ya sayansi tutegemee taa kona ya Makumbusho pale mbele ya Demi plaza...halafu taa nyingine victoria lazma waweke...wakitoka hapo wanaweka tena pale mbele ya jengo la voda kabla hukafika morocco....nanunua pikipiki wallah
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom