Traffic atekwa jijini Dar...!

Traffic atekwa jijini Dar...!

Polisi wa hii nchi sio wazima ni wachawi au walevi wa gongo! Wanajua maana ya kutekwa hawa? Wamuulize dr uli
 
Yule Nurse aliyetekwa alishapatikana, aliwa salama kabisa!
 
Askari wa usalama barabarani ambaye jina lake halikufahamika ameokolewa na askari wenzake baada ya kutekwa na mwendesha bajaji, tukio hilo lilitoke barabara ya alihasan mwinyi maeneo ya sayansi.

Inadawa mwendesha bajiji aliposimamishwa alikataa kusimama ndipo askali huyo alidandia bajaji na kumlazimisha aende kituoni baada muda bajiji ilikimbizwa na kuanza kupelekwa kusikojulikana walipo katiza taa za sayansi polis huyo wa usalama barabarani alipiga kelele na kuokolewa na wenzake...huku mwendesha bajaji akihama njia kuu na kuchepuka na barabara ya LHRC.

Hapa ni wanausalama wa barabarani wakimthibiti mtekaji...
attachment.php

Askari una kitambi, unawezaje kuwadhibiti madereva?
 
Jamaa anastahili tuzo ya ujasiri
Hao traffic wanahangaika na vibajaj wanaacha milori na midaladala mibovu ikiua na kuvunja sheria.
 
Traffic hajui kazi yake, kisheria ni makosa kwa askari wa usalama barabarani kupanda kwenye kipando cha mtuhumiwa hata kama ana makosa, alichotakiwa kufanya ni kumsimamisha na endapo angekataa angetoa taarifa kwa wenzie na angenakili namba za hicho chombo kwa hatua zaidi za kiusalama!
 
Angekuwa wa kike, kama huyo kwenye picha, sijui ni kipi kingemtokea mbele ya safari mmmh !!
 
Huyu ni shdaa
akuna kutekwa hiyo ni trella msiidandie bajaji za watu bila maelewano
 
Traffic hajui kazi yake, kisheria ni makosa kwa askari wa usalama barabarani kupanda kwenye kipando cha mtuhumiwa hata kama ana makosa, alichotakiwa kufanya ni kumsimamisha na endapo angekataa angetoa taarifa kwa wenzie na angenakili namba za hicho chombo kwa hatua zaidi za kiusalama!

Nduo maana hapo juu nikasema traffic kajiteka mwenyewe...... alipanda kutafuta nini???
 
Na yeye sheria inamruhusu kudandia kipando kilichokataa kusimama...
 
hapa ndio nikikumbuka ile clip ya magaidi wa Tanga naanza kuamini kuwa TZ hakuna askari. bajaji hata ingekuwa mm sina mafunzo yoyote wala mazoezi ningempiga loba ya kufa mtu hadi asimamae mwenyewe
 
Back
Top Bottom