TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Leo 01/01/2021 mamlaka ya mapato Tanzania kupitia kwa waandishi wa habari, imetangaza makusanyo ya mwezi Disemba 2020 kuwa ni takribani trilioni 2, hii ni rekodi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hii mwaka 1996

Hii ni hatua ya kupongezwa sana kwa Watanzania wote walipa kodi na mamlaka ya mapato nchini, kukusanya trilioni 2 kwa mwezi( Disemba) ni jambo lenye kutia moyo sana kwa sisi wananchi

Nilikuwa napitia mapitio ya uchumi ya kila mwezi( Monday Economic Review) kutoka benki kuu yetu( BOT) kwa mwezi Disemba 2020

Ripoti hiyo ya Disemba, inaonyesha kwa mwezi October pekee, 2020, serikali ilikusanya takribani trilioni 1.682, hii ni jumla ya makusanyo yote ya kikodi( Tax Revenue) na yasio ya kikodi ( Non Tax Revenue).

Ambapo kwa mwezi huo wa October 2020, makusanyo ya kikodi( Tax Revenue) pekee yalikuwa ni trilioni 1.295 , na makusanyo yasio ya kikodi( non tax revenue) yalikuwa ni bilioni 282.2 na makusanyo kutoka local government ( own source) yalikuwa ni bilioni 51.2.

Lakini tukienda kwenye matumizi ( Government Expenditure) kwa mwezi October 2020, ripoti hiyo( Monthly Economic Review) inaonyesha kuwa serikali ilitumia takribani trilioni 1.854.

Ambapo matumizi hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo, kwenye matumizi ya kawaida ( Recurrent Expenditure) ilikuwa ni trilioni 1.282 na matumizi kwenye miradi ya maendeleo ( Development Expenditure) ilikuwa ni bilioni 571.

Ambapo matumizi makubwa zaidi kwenye serikali yanakwenda kwenye mishahara( wages bills) za watumishi wa umma, kwa mwezi October serikali ilitumia takribani bilioni 601.7 kulipa mishahara kwa mwezi mmoja tu.

Na pesa nyingine inatumika ku service madeni yetu( Debt expenses), ambapo kwa mwezi October pekee, serikali ilitumia takribani bilioni 192.4 kulipia interest ya madeni yetu ya nyuma na sasa.

Kwa maana hiyo kwa mwezi October 2020, serikali ilitumua fedha nyingi zaidi( trilioni 1.854) kuliko pesa tulizoingiza(trilioni 1.628) kwa mwezi( budget deficit).

Kwa hatua ya leo ya mamlaka ya mapato kukusanya trilioni 2, kama itaendelea hivi hivi kila mwezi, maana yake ni kwamba serikali tunakwenda kuwa tunaingiza/ kukusanya fedha nyingi zaidi kuliko matumizi yetu kwa mwezi.

Hii itasaidia sana kwa nchi yetu kupunguza mzigo wa kuendelea kukopa mikopo ya bei nafuu( concession loan) kutoka kwenye multilateral lending institutions au mikopo ya kibiashara( non concession loan) kutoka kwenye mabenki ya kibiashara duniani.

Kongole kubwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania 👏👏👏

Ngamanya Kitangalala Mwaswala kngamanya@yahoo.com
0756 669494
IMG-20210101-WA0026.jpg
IMG-20210101-WA0027.jpg
 
Hakuna shida cha msingi tupo uchumi wa kati wa chini.

Mitano tena.

Tuendelee kununua Mavieite ili matumizi yaendelee kuwa makubwa zaidi kuliko mapato.

Wanaosubiri nyongeza na madaraja ya mishahara basi waendelee kusugua magaga. Maana matumizi bado makubwa kuliko kipato.

Nasema uongo ndugu zangu?
 
bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
 
Zamani local government na taasisi nyingine za serikal zilikuwa zikikusanya na kutumia fedha zake kulingana na mahitaji ya eneo/mamlaka husika na hivyo kuboresha huduma na miradi kwa wakati.

Siku hizi TRA inazikusanya na inazitangaza kama sehemu ya mapato yao.Alafu Kuna urasimu kuzirudisha toka hazina kwenda kwa wamiliki na hivyo kusababisha huduma,malipo,madeni,miradi n.k kukwama. Alafu TRA inajisifia!
 
Matumizi yanapokuwa makubwa kuliko makusanyo
 
Watumishi wanatunyonya Sana, yaani karibia nusu ya pato kwa mwezi wanachukua wao, na bado wanadai nyongeza,

Sioni kama Taifa namna tunaweza fanya maendeleo kama kipato almost chote tunalipana mishahara tu.
Kwa hiyo unashauri serikali iondoe watumishi ili ijiendeshe kwa miujiza? bongo kuna mishahara gani hadi watumishi wasidai mishahara bora.
 
Kwa hiyo unashauri serikali iondoe watumishi ili ijiendeshe kwa miujiza? bongo kuna mishahara gani hadi watumishi wasidai mishahara bora.
Mishahara iendane na kipato,

Kwahiyo unaona sawa wengine wakamuliwe ili wakanufaike wengine,

Kama unaona mshahara ni mdogo si unaacha tu wengine watafanya.
 
Back
Top Bottom