TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Pumbav wewe
We ni mmoja wao? Je kweli kwa akili ya kawaida watu mil hamsin waende somea kapato,nini mgawanyo wa majukum,wao wako pale kwa kazi iyo ya kodi ,kutoa elim na si kuonea watu KWA bambikia makodi.na kila fani inaumuhim wake,Sasa ukisema kila mtu akasomee Mambo ya kodi, hivyo hivyo ipo siku utasema Kila mmoja akasomee ualim,police,bwanashamba n.k ,hoja ya maajabu Sana hii,na ya funga mwaka
 
Hii ndio JF yenye manufaa hasa, hata sisi tusiokuwa na ABC ya haya mambo ya kodi tunafaidika vizuri kabisa.

Ahsante sana mkuu 'IFRS' kwa kuongeza thamani ya JF.
 
Unajua, kelele nyingi zinazosikika sasa, baadhi yake ni sababu za ujinga (kutojua) kwa walipakodi. Duniani kote, mkusanya kodi huwa ni mtu wa kuogopwa.Hata kwenye biblia wameelezwa, kwa kutopendwa na wafanya biashara.
 
Ingependeza Kama mkuu watahalam wa wambo ya kodi wengeanzisha uzi mahalum kuhusu elimu ya kodi ,maana kweli wenda watu wanapigwa na TRA kutoka a na uelewa ndogo,
Kodi zinatokana na sheria ambazo accountants inabidi wazitumie ila siyo kitu constant maana kodi zenyewe zinabadilika kila mwaka wa fedha na mara nyingine kubadilika kwake zinabadilisha treatment of certain items in the final accounts.

Jinsi wenzetu wanavyo update practice wataalamu wa sheria za kodi (ambao na wenyewe lazima walikuwa accountants in their past life) wanatafsiri application za sheria kwa kutoa vitabu ambavyo accountants wote wasiobobea kwenye tafsiri za sheria wanatumia, that’s how things work.

Vinginevyo bila ya watu kama hao kila mwaka all accountants will need to get the entire budget manuscript and start to interpret the law, utaratibu utakuwa ni majanga sio wote watasoma kwanza na kwa watakaosoma chances are kutakuwa na variation of interpretation.

Kurahisisha mambo ndio maana wataalamu wa tax law ambao ni accountants waliojiongeza wanatafsiri kodi zilizobadikika kwenye budget na application zake pamoja na mambo mengine allowed or disallowed expenditures and so for forth to do with VAT taxes as well final accounts.

Na hao ndio wataalamu the likes of international accounting firms such as PWC or KPMG hire, watu kama hao sheria zetu za copy and paste wanazijua applicability yake kushinda accountants tia maji tia maji wa TRA.

Ndio maana unaona makampuni makubwa ya kigeni wanatumia hizo large accounting firms kuwafanyia hesabu zao matokeo yake tunabaki tunalia hawalipi kodi wakati sheria wanazotumia tumepitisha wenye bungeni.

Kwa ivyo kusema utaanzisha mjadala wa kodi wakati mambo yanabadilika kila mwaka sio tu kwamba watu wanaweza pishana interpretations (kama ulivyoona baadhi ya wachangiaji humu kwenye treatment za withholding tax) bali unaweza kuwa mjadala usio jenga.

Ni muda wa kuchapisha kitabu cha kutumiwa na proffesionals (ambacho kinakuwa updated kila mwaka) kama nchi nyingine wanavyofanya mambo, iwapo ili jambo alifanyiki kwa sasa.
 
Thats the crux of the matter.
Mkuu hujijui kuwa hujui.
Mfano uliotoa umejionyesha kuwa licha ya kuwa "Tax Consultant" hujui hata kukokotoa With Holding tax kwa kukosa uelewa.
Chuo cha kodi kama threshold ni form four failures na kinapokea watu kama wewe, then you know what to expect.
 
Kuna uzi umeletwa humu maafisa wa tra wasimamishwa kazi na waziri mpango
Makosa yao moja yapo ni kubambikia watu mikodi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Mkuu kuna watu wajinga wajinga wanafikiri hatujui wanachokifanya .
Hii ni trela maana sasa tutanza kutoa zile transactions ambazo huwa wanazifanya kukomoa mfanya biashara ili wavute michuzi.
Tnashukuru Waziri Mpango ameanza kufungua macho sasa.
 
Kama vipi na viongozi wachunguzwe tokea enzi za nyerere sehemu aliposaini mktaba pia utajiri wake na Hela aliyokuwa analipwa kama na tax return TRA Iko proportion hata kama ana biashara je alikuwa anazilipia kodi.
Yaani lisisalie jiwe juu ya jiwe.

Ila hawa majamaa tokea nilivyowanaga mwaka 95 wanampiga dingi mdogo kama 10M niliwaogopa sana.
Mpaka wamenifanya nilitaka kufanya biashara nawaza TRA mana kama ni kovu na nilivyokuwa mdogo jamani
 
Bahati mbaya hujui kama hujui, hivi unashindwa kuwa na uelewa wa kodi rahisi kama withholding tax payments halafu unashinda humu kuwalalamikia TRA. TRA kazi yao ni kusimamia na kutafsiri sheria za kodi na sio kufundisha watu sheria.kama hujui angaika kutoa huo ujinga
 
Wafanyabiashara wengi wanafuata Sheria pasipo kukwepa kodi, lakini TRA wakiamua kusaka Rushwa ama kumkomoa mtu humbambikia VAT hewa kodi bandia kwa njia haramu za kishetani, maofisa vinara wa kupora pesa za wafanyabiashara hawakosagi sababu hata kama mfanyabiashara analipa kodi zote bila Tatizo, wakidhamilia kutaka Rushwa hulazimisha chochote mpaka wafanikishe malengo yao
 
Hizi kazi inabidi wapewe watu waliowiva.
Mfano uliotoa kweli ni kilaza.
 
Nikupe swali jingine rahisi ili kuku expose dunia nzima ijue aina ya watuwetu wa kodi tulio nao.

Je katika biashara yako uliyoieleza , profit yako ni kiasi gani?
 
Nekwenda kwenye moja Kati ya maduka maarufu ya nguo na viatu vya kiume hapa Dar lililopo kariakoo nikanunua kiatu kwa TZS 90,000/- namdai risiti ananiletea stori kwamba mashine imeharibika. Nilipokuuliza kuhusu barua toka TRA hana nikamwambia anirudishie hela siwezi kutoka bila Risiti.

Akainama chini ya counter akaniprintia Risiti fasta.

Kesho mkisikia maduka hayo yamefungwa kama kawaida yenu mtaanza kuimba mapambio ya TRA wanaonea wafanya biashara.

Nyambafu kabisa...
 
Hali halisi iko wazi. Kinyume cha hapo ni wizi. Na wanatumia nafasi kama hizo kujipatia rushes.
 
Mbona nyambafu wengi zaidi mnao majumbani kwenu wakijenga mahekalu huko Kimara, Kinsudi, Bonyokwa na kwingineko.
Semeni tu !
Tulianzishe kuleta picha humu mtandaoni?
Na uzuri siku hizi unaweza weka hata google location.
 
Tuzidishe spana habari zinawafikiaView attachment 1651677
Safi sana waziri sasa umeanza vizuri, tunaomba wana JF waje na List ya maofisa wa TRA vinara wa kufunga Account kuwabambikia kodi kubwa hasa wilaya ya ilala kule long room makao makuu ya TRA, TRM mkoa wa Dsm Kinondoni na Temeke ndipo kuna vinara wa kuwabambikia kodi na kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…