Kodi ni lazima zilipwe hakuna kukwepa wala kuacha kulipa kodi, lakini wale baadhi ya maofisa wa TRA wapenda Rushwa lazima wachunguzwe wachukuliwe hatua kali iwe mfanoHawa maofisa kama wapo ni lazima washughulikiwe, "wachunguzwe mali zao...); na hapo hapo usisahau wafanyabiashara ni lazima walipe kodi zao stahiki. Hilo haliepukiki.
Tumewapa nchi hii washenzi waongoze sasa wanaumiza wananchi ili wafidie ufisadi wao.Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.
TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.
TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.
Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.
Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.
UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.
Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.
Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.
Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba
Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.
Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.
Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.
Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.
Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.
USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
Mkuu sikatai wapo baadhi ya maafisa wa TRA ambao sio waaminifu, lakini pia kuna wafanyabiashara wengi hawafuati ipasavyo sheria za kodi.TRA ifumuliwe isukwe upya wale maofisa vinara wa kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kuwafungia Account zao waanze kuchunguzwa na Takukuru kwani wengi wamekuwa matajiri kwa Rushwa hii utapunguza uonevu uliokithiri sasa
Nakubaliana nawe kwa asili mia kuhusu hao maofisa.Kodi ni lazima zilipwe hakuna kukwepa wala kuacha kulipa kodi, lakini wale baadhi ya maofisa wa TRA wapenda Rushwa lazima wachunguzwe wachukuliwe hatua kali iwe mfano
Mfumo mzuri ni kuwa na kodi rafiki kodi nzuri kodi isiyowaumiza watu, kodi ambayo haitawafanya watu kuiona mzigo kwao, kodi ndogo ikitolewa na wafanyabiashara wote pasipo kukwepa Nchi itaingiza pato kubwa mno, Elimu kwa mlipa kodi isambazwe mitaani kote kwa wajumbe wa nyumba kumi Serikali za mitaa iwe ni mitaala mashuleni na kisha mfumo wa kodi uwe na Link ya kitambulisho cha Taifa mtaa na kuwe na Sheria ya endapo mlipa kodi kahama mtaa kijiji kata wilaya atoe taarifa kuanzia Serikali za mtaa na ofisi za kodi, wataalam wasuke system ya kisasa ya kodi kama kule China , America Ulaya kuwabaini wakwepa kodi kiwepesi kuliko hii mbinu ya kukadiria watu ambayo huzaa Rushwa na malalamiko mengi kila kukicha ya kubambikiwa kodi kubwa kufungiwa account kienyeji kwa njia haramu za kishetaniMbona sikuelewi mkuu 'minyoo'.
Nimetoa visingizio gani vilivyokuvuruga akili kiasi hiki?
Sikatai kwamba kunaweza "...kuwa na usumbufu" katika utendaji kazi wa watumishi wa TRA.
La msingi ninalolizungumzia hapa ni kwamba pande zote zinaweza kubeba lawama, kutokana na kutokuwepo na mfumo maalum unaowezesha kodi zilipwe bila ya misuguano mingi kama ilivyo sasa.
TRA wana wajibu kuweka utaratibu mahsusi unaoeleweka vizuri na walipa kodi; na walipa kodi wawe na ufahamu mzuri wa utaratibu uliowekwa na TRA ili wasisumbuliwe baadae na madai yasiyokuwa na uhakika.
Nimetoa mfano wa wenzetu huko nchi za nje, ambako sio lazima kufuatilia mlipa kodi kila mahali, kwa vile wajibu wake anaufahamu na miundombinu imewekwa aitumie ili alipe kodi bila ya usumbufu mwingi.
Hapa sielewi unanilalamikia nini kuhusu "visingizio".
Ushauri mzuri.Mfumo mzuri ni kuwa na kodi rafiki kodi nzuri kodi isiyowaumiza watu, kodi ambayo haitawafanya watu kuiona mzigo kwao, kodi ndogo ikitolewa na wafanyabiashara wote pasipo kukwepa Nchi itaingiza pato kubwa mno, Elimu kwa mlipa kodi isambazwe mitaani kote kwa wajumbe wa nyumba kumi Serikali za mitaa iwe ni mitaala mashuleni na kisha mfumo wa kodi uwe na Link ya kitambulisho cha Taifa mtaa na kuwe na Sheria ya endapo mlipa kodi kahama mtaa kijiji kata wilaya atoe taarifa kuanzia Serikali za mtaa na ofisi za kodi, wataalam wasuke system ya kisasa ya kodi kama kule China , America Ulaya kuwabaini wakwepa kodi kiwepesi kuliko hii mbinu ya kukadiria watu ambayo huzaa Rushwa na malalamiko mengi kila kukicha ya kubambikiwa kodi kubwa kufungiwa account kienyeji kwa njia haramu za kishetani
Kweli ukiambiwa kitu usipuuze.Wachunguzwe na nani kama anaewatuma ndo last say wa state.
Hii inchi imewekea malengo ya ukusanyaji hadi Traffic police na Hospital sasa sielewi wamelenga makosa ya barabarani yaongezeke na watu wazidi kuumwa ?
Rais Hussein Mwinyi akiapishwa Mawaziri wa Serikali yake alisema kuwa Kodi kubwa kwa walipa kodi haihakikishi mapato makubwa ya Serikali bali Kodi rafiki walipa kodi wengi. Huyu ni Rais wa wananchi wake milioni 1.5, inashangaza Rais wa watu milioni 60 pamoja na wale haelewi ukweli huu badala yake anatoa maagizo na malengo makubwa ofmagumu kufikiwa. Hii inawafanya wakusanyaji Kodi kutumia nguvu na ubabe kufikia viwango walivyoagizwa wakiongeza cha juu chao na kufanya viwango kuwa vikubwa zaidi kutolipika. TRA ni moja ya Taasisi chache wafanyakazi wao wanalipwa vizuri sana na rushwa njenje kuwa hiyo vilaza wa wakubwa wamekaa huko. Idara ya Polisi hapo zamani ilikuwa inapata shida sana kupata wafanyakazi hata wasio na kazi yoyote ya kuwaletea kipato hawakutaka upolisi lakini leo ni vigumu sana kwa mtoto wa mwananchi wa kawaida kupata kazi ya upolisi ni watoto wa wakubwa na wa Polisi wenyewe ndo wamejaa huko kwa sababu ya fursa ya rushwa. Kuhusu ukusanyaji Kodi, TRA ndo iandae malengo yao kila mwaka bila cha juu kulingana na hali halisi kiuchumi kwenye maeneo yao ya kazi na kupeleka malengo hayo Serikalini ili iandae bajeti zake. Lengo la ukusanyaji lisipofikiwa ni TRA wa kulaumiwa.Wizi mtupu. Wamejazana maofisini kurudia kazi zile zile. Sio wabunifu.
Kodi zimeacha makampuni mengi yakiwa na madeni yasiyolipika. Wengi wanatumia assessment kama sehemu ya kuchukua rushwa tena bila aibu.
TRA wanaua biashara zetu kwa kubambikia kodi zisizolipika.
Hivi kwenye hizi biashara zetu, Kuna kampuni ngapi zinazopata faida zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka? Mbona wao wanakuwa kama sio wasomi. Kila hela kampuni inayoingiza wanaichukulia kama ni faida.
Yes TRA sio mbali sana mtakuwa hamna mtu wa kukusanya tena kodi. Yatabaki madeni yasiyolipika
Mkuu uelewa wa kodi ni simple kabisa.Mbona sikuelewi mkuu 'minyoo'.
Nimetoa visingizio gani vilivyokuvuruga akili kiasi hiki?
Sikatai kwamba kunaweza "...kuwa na usumbufu" katika utendaji kazi wa watumishi wa TRA.
La msingi ninalolizungumzia hapa ni kwamba pande zote zinaweza kubeba lawama, kutokana na kutokuwepo na mfumo maalum unaowezesha kodi zilipwe bila ya misuguano mingi kama ilivyo sasa.
TRA wana wajibu kuweka utaratibu mahsusi unaoeleweka vizuri na walipa kodi; na walipa kodi wawe na ufahamu mzuri wa utaratibu uliowekwa na TRA ili wasisumbuliwe baadae na madai yasiyokuwa na uhakika.
Nimetoa mfano wa wenzetu huko nchi za nje, ambako sio lazima kufuatilia mlipa kodi kila mahali, kwa vile wajibu wake anaufahamu na miundombinu imewekwa aitumie ili alipe kodi bila ya usumbufu mwingi.
Hapa sielewi unanilalamikia nini kuhusu "visingizio".
Kwamba wafanyabiashara hawajui kodi hilo ni kisingizio tu cha kutetea mfumo mbaya wa kodi.Mkuu sikatai wapo baadhi ya maafisa wa TRA ambao sio waaminifu, lakini pia kuna wafanyabiashara wengi hawafuati ipasavyo sheria za kodi.
Jambo lingine watz hatujui sheria za kodi, hata ambao wamesomea mambo ya uhasibu wengi wao hawajui kodi vizuri mimi ni shahidi wa hili.
Kwahiyo hapa kuna shida mbili
1.ignorance
2.integrity
Ngoja nikueleweshe kidogo tofauti ya withholding tax, provisional tax na corporate tax.Kwamba wafanyabiashara hawajui kodi hilo ni kisingizio tu cha kutetea mfumo mbaya wa kodi.
Siyo siri, mfanya biashara akitozwa kodi ZOTE na tozo juu, basi anatoka na deficit katika biashara.
Kodi zimetungwa kiholela na TRA wanazi enforce kiholela.
Its as if its a crime kufanya biashara.
Sasa wewe IFRS hebu nipe mchngo wako wa mawazo.
Kama biashara inapigwa Corporate Tax, halafu huku mwanzoni mfanya biashara amesha katwa Witholding tx na provisional tax , jumla ya ambavyo ni kubwa kuliko Corporate Tax, sasa hapo si kudhulumu biashara?
Kodi aina mbili ndizo zenye usumbufu kwa wafanyabiashara, Mapato na VAT. Upande wa mapato ukikadiriwa wanakadiria kubwa, ukipeleka hesabu wanazikataa. Ukija kwenye VAT mazingira ya biashara na ushindani uliopo, idadi ya wafanyabiashara waliosajiliwa vs wale wasiosajiliwa, uwezo wa wateja (purchasing power) vinafanya VAT kuwa burden kwa mfanyabiashara badala ya mteja wa mwisho.Prevention is better than cure, kama VAT tu ambayo inatakiwa kuwa rahisi inawashinda hesabu zake na kuishia kulalamika kubambikiziwa malipo.
Income tax si ndio kasheshe huko naona ndio wanatandikwa mpaka wanatia akili.
Sitoshangaa nikisikia 90% ya wafanyabiashara wakitanzania awaelewi ‘2008 income tax act’.
Hao wachache ambao wanaijua kwa kuangalia mwenendo wa malalamiko sidhani kama wanaweza tengeneza income statement sambamba na sheria kuweza kufanya expense adjustments za ‘allowed and disallowed expenditures’, uelewa wa treatments za depreciation of assets, capital allowances; etc kwa manufaa yao ili kupunguza kodi wanayotakiwa kulipa.
Solution ya haya matatizo ni accounting services na mtaalamu mmoja wa tax kutoa kitabu cha income tax kinachokuwa updated annually baada ya budget kuwasaidia accountants kwenye kufanya hesabu zao. That’s what other people do in the world.
So far kwetu kwenye maswala taxation mwerevu wa sheria ni mmoja tu “TRA” wafanyabiashara wapo at his mercy; balance inahitajika wafanyabiashara lazima na wao watumie wataalamu kuwaandilia hesabu.
Tatizo ninalo liona ‘knowing us Tanzanians’ mijitu itakayotoa hizo services itaanza tamaa kuja na charges za millions na kuwafanya watu waone gharama kwenda. Badala ya kufikiria in terms economic of scale. We ukipata wateja 300 wa kuwafanyia tax kila mmoja ukamcharge laki moja tu kwa mwaka maisha umeyapatia.
Akuna cha tax consultant wala nn.... hao wajiita tax consultant are just mesengers siku iziajiri tax consultant wa maana
Ndio maana binafsi naona ni busara wafanyabiashara kutumia accountants ninacho ona hapo ni vice versa.Kodi aina mbili ndizo zenye usumbufu kwa wafanyabiashara, Mapato na VAT. Upande wa mapato ukikadiriwa wanakadiria kubwa, ukipeleka hesabu wanazikataa. Ukija kwenye VAT mazingira ya biashara na ushindani uliopo, idadi ya wafanyabiashara waliosajiliwa vs wale wasiosajiliwa, uwezo wa wateja (purchasing power) vinafanya VAT kuwa burden kwa mfanyabiashara badala ya mteja wa mwisho.
Mfano wa kitoto huu.Ngoja nikueleweshe kidogo tofauti ya withholding tax, provisional tax na corporate tax.
Withholding tax ni kodi ya mapato ya awali(advance payment) inayokatwa na kuwasilishwa TRA na mlipaji kwa niaba ya mlipwaji.
Mfano mimi kama tax consultant nikaja kukusaidia kazi za kiuhasibu kwa makubaliano wa kunilipa TZS 10,000,000.
Unatakiwa ku-withhold 5% ya contract price, ambayo ni 500,000 na badala yake unanilipa net ya TZS.9,500,000.
Assume mwaka mzima nilipata kazi hiyo moja tu.
Lakini niliingia gharama za operating cost may be 8,000,000 kwa mwaka mzima.hivyo faida ni 10,000,000 minus 6,000,000= hivyo faida ni 4,000,000.
Sasa corporate tax ni 30% ya faida ,hivyo natakiwa nilipe 1,200,000.
Sasa before sijalipa
(i) natakiwa ni-deduct advance payment ya withholding tax ambayo ni laki 5.hivyo tax payable inapungua kutoka 1200,000 to 700,000
(ii) natakiwa ni-deduct provisional taxes nilizolipa kwenye all 4 installments, let say nililipa 150,000 for each installment, hivyo nimeashalipa total of 600,000
Hivyo basi tax liability inapungua kutoka 700,000 to 100,000.
In summary corporate tax of 1200,000 umeilipa kama ifuatavyo
● 500,000 by way of withholding tax
● 600,000 by way of installment
● 100,000 by way of final tax.
Nadhani hakuna double taxation hapo
Tatizo mkuu zipo tahasisi zinakinzana Sana,naungana na wewe mkuu kwamba waofisa wa TRA wote wachungunzwe Mali zao, maana Wana wanakwiba Sana,ita iundwe task force kwa kazi hiyo Lila wilaya tz itakayojumlisha na takukuru,ila wasiachiwe takukuru tu,Takukuru waingie kazini maofisa wote vinara wa kuwabambikia kodi kubwa kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetani wachunguzwe mali zao na ikibidi washitakiwe
Mkuu hii ni mifano ya kitabuni kama mnavyo fundishwa.Ngoja nikueleweshe kidogo tofauti ya withholding tax, provisional tax na corporate tax.
Withholding tax ni kodi ya mapato ya awali(advance payment) inayokatwa na kuwasilishwa TRA na mlipaji kwa niaba ya mlipwaji.
Mfano mimi kama tax consultant nikaja kukusaidia kazi za kiuhasibu kwa makubaliano wa kunilipa TZS 10,000,000.
Unatakiwa ku-withhold 5% ya contract price, ambayo ni 500,000 na badala yake unanilipa net ya TZS.9,500,000.
Assume mwaka mzima nilipata kazi hiyo moja tu.
Lakini niliingia gharama za operating cost may be 8,000,000 kwa mwaka mzima.hivyo faida ni 10,000,000 minus 6,000,000= hivyo faida ni 4,000,000.
Sasa corporate tax ni 30% ya faida ,hivyo natakiwa nilipe 1,200,000.
Sasa before sijalipa
(i) natakiwa ni-deduct advance payment ya withholding tax ambayo ni laki 5.hivyo tax payable inapungua kutoka 1200,000 to 700,000
(ii) natakiwa ni-deduct provisional taxes nilizolipa kwenye all 4 installments, let say nililipa 150,000 for each installment, hivyo nimeashalipa total of 600,000
Hivyo basi tax liability inapungua kutoka 700,000 to 100,000.
In summary corporate tax of 1200,000 umeilipa kama ifuatavyo
● 500,000 by way of withholding tax
● 600,000 by way of installment
● 100,000 by way of final tax.
Nadhani hakuna double taxation hapo
Wapo baadhi ya maofisa wa TRA hawajui Sheria ni mbumbumbu walisoma kiujanja janja tu na hao ndiyo vinara wa kufunga Account na kuwabambikia kodi hewa wafanyabiashara pasipo kuzingatia mtaji wa biashara<kuu hii ni mifano ya kitabuni kama mnavyo fundishwa.
Kwenye biashara kitu ingine kabisa.
Kwanza inaelekea hujui kuwa Witholding Tax si 5% ya total contract price, ni 5% on service and labour!
Biashara ukiikata 5% ambayo ndiyo mark up ya profit, basi unaelekea kuua biashara.
Sasa kama ninyi mnaojiita wahasibu(especially kama uko TRA) hamulielewi hili basi ni majanga!
Pili total aggregate witholding tax (pamoja na provisonal tax) mara zote inazidi 30% on profit katika kukokota Corporate Tax.
Hapo ndio tunaona TRA ikimega Capital ya biashara.