TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,551
Reaction score
28,510
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.

YATOKANAYO-UPDATE
====================

Asante sana Waziri Mpango kwa kulifuatilia hili lalamiko na kutoa maagizo ya kutatua kero hii.

20201217_081408.jpg
UPDATE II
TUNASHUKURU SANA
Kwa Mama Samia kuona umuhimu wa kulitatua tatizo hili la uonevu wa dhahiri wa TRA.
Wizi huu inaelekea ulikuwa na baraka za "walio juu".
Lakini tumeona matokei yake, kufungwa kwa biashara nyingu na wenye mitaji mikubwas kuikimbiza nje ya nchi.

Wakati mwingine tunajiuliza kama walioratibu wizi huu kwa wafanyabiashara wananchi, kama kweli ni raia wa Tanzania au la!
 
Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.
Haya ndio yanayoendelea na yamekuwa common nchi nzima kwa kuwabambikia kodi wazalendo kiasi kwamba kuna ambao wanafunga hizi biashara na rushwa wanailamisha sana.

Rafiki yangu wa AR walimwambia kwa miaka kumi anadaiwa 70M akaonyesha mahesabu yake yote yaliyovyokuwa (tax clearance) lakini wapi walibanana nae hadi ikawa 30M hapo wakakomaa alipe. Hadi sasa hajui anazipata wapi!
 
Umelimbikiza madeni nenda kalipe na TRA wanakubali malipo kwa awamu
Naona bado huelewi mantiki hata ya mfano wa ndizi.

Kodi hutokana na tozo na faida ya biashara.

Kama tozo hakuna na faida hakuna na bado ukapigwa kodi, tena kubwa, maana yake FUNGA BIASHARA.

Na wengi wanafunga.

Watanzania tusipolielewa hilo tunafikiri kodi ni kupanda migongo ya punda anayeitwa wafanyabiashara.
Sasa hivi hawa punda wanakufa kwa wingi.
 
Huwa wanafunga Account kihuni kienyeji kisha wanakubambikia VAT kienyeji kihuni hawafuati Sheria za Nchi, hawajali kama una File zote za ukaguzi ambao kisheria ni miaka mitano nyuma, wao hurudi nyuma hata miaka 12 kienyeji tu ili mradi kumkomoa mfanyabiashara na kutengeneza mazingira ya Rushwa, wafanyabiashara wengi wamefungiwa Account kisha kuwatishia kesi za utakatishaji fedha na uhujumu, ukwepaji kodi, na kibaya kupita vyote hufunga A/C kihuni pasipo kumtaarifu mhusika kabla, sasa TRA imekuwa Sumu ya kuua biashara na pia inasababisha wafanyabiashara kuacha kuweka pesa zao bank kwa hofu ya kuporwa na TRA
 
Acheni kulalamika tulipowapitia mtuchangie pesa za kulipa mawakala mligoma kabisa mkawachangia ccm sasa lipeni kodi ninyi wazalendo mimi sio mzalendo.
Kodi zinalipwa na wakaguzi wanapita lakini wapo baadhi hukataa ukaguzi wa awali wanaamua kufunga A/C kienyeji kwa njia haramu za kishetani ili kutengeneza mazingira ya Rushwa au kumkomoa watu.
 
Mimi yalinikuta tayari hivyo hivyo ulivyoeleza.
Mkuu yamewakuta wafanyabiashara wengi.Na serikali sikivu iko kimya.
Hata waziri wa sasa Nd Mwambe alivyokuwa TIC alilieleza tatizo wazi kabisa lakini serkali hailifanyii kazi.
Tax base inazidi kupungua na ni dhahiri matokeo yake ni kodi kupungua.
Seikali sikuvu-kimya!
 
Back
Top Bottom