TRA valuation system ya magari haiko fair

Ushuru unatozwa kwa kilometers?
 
Mkuu naunga mkono hoja. Mi nilidhani nchi kama Japan ama china ndo zingekua na ushuru mkubwa ili discourage kuingiza magari toka nje coz wao wanatengeneza. Napata shida kuelewa kwanini nchi yetu inafanya hivyo, labda mwenye uelewa zaidi wa suala atujuze KWA NINI?
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
Tembelea website ya tra utajua vizuri ,gari inaangaliwa cc ,mwaka na wala hawaangalii kilometers
 
Juzi nimechoka nina million tisa naambiwa huwezi nunua ist kwa bei iyo anzia million 15
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !

Sawa Barbosa nimekuelewa.

Ok nimeibiwa. Sasa kwanini Serikali inaniadhibu zaidi?

Kwani kwa TRA kuongeza thamani ya gari ni kunaashiria kuwa gari ni chakavu au lina thamani kubwa? Nimeuziwa gari kwa $4,455 na TRA wamelithaminisha $10,880. Kitu kinachothaminishwa zaidi ya bei/uhalisia kinamaanisha hicho kitu kina hadhi kubwa au ni chakavu? Labda unipe ufafanuzi hapa ili nijifunze.
 
Kwani TRA wana base kwenye km au mwaka? Ila vyovyote iwavyo kodi yetu bado naona ni kubwa mno kwa upande wa magari. Mi nadhan wengi tunachukulia gari kama chombo cha starehe (luxury good) lakini kumbe inamrahisishia mtu kuongeza kipato binafsi ambacho huenda sanjari na kuongeza pato la nchi
 

Ahsante DN kwa ufafanuzi.

Lakini sasa kwanini TRA wameniadhibu, kwa kitu ambacho sikuwa na control nacho? Mimi nimeliona gari na nikalipenda. Nikauliza bei nikapewa na nikaikubali. Sasa kwanini TRA wamehamua kuniadhibu zaidi kwa kunipiga ushuru ambao hauna uhalisia kwa bei niliyolipa? Ni kwamba hawaamini kuwa nimelipa hiyo bei ama? Kama ni hivyo, kwanini wasingenipa nafasi ya kuwasilisha documents ambazo zinaweza kuthibitisha/kutothibitisha kuwa nimelipa kiasi ninachosema nimelipa?
 
Mkuu Quemu, yawezekana kuna kitu flani ulikuwa haukijui! Angalia CIF price yako uliyonunulia gari na Custom Value CIF iliyopo kwenye kikokotozi cha TRA.
Kama custom value CIF ni ndogo kuliko CIF uliyolipia gari lako basi utachajiwa hela kubwa na TRA kuliko inayoonekana kwenye calculator yao (hapo sijui wanafanyaje mpaka hela inakuwa kubwa) , ila kama CIF yako ni ndogo ama inalingana na custom value CIF basi utalipia exactly kama iliyopo kwenye TRA calculator.

Mimi niliagiza gari kidogo niingie kwenye matatizo haya bahati nzuri kabla sijalipia pesa Japan nikawa nimeingia JF nikakuta uzi unaongelea kuhusu hili, ikabidi nibadili maamuzi na ku-negotiate na seller na bahati nzuri tukashushana mpaka CIF price nikawa chini ya custom value CIF ya TRA (difference ilikuwa 200USD). B/L zilipokuja TRA wakafanya analysis na kodi ilikuja ile ile niliyotarajia ambayo haipo juu kihivyo, CIF price inatofautiana kwa 1.5mil na kodi niliyotakiwa kulipa!!
 
Yoyote atakaye agiza Gari CIF $2500 ajiandae kulipia 6M Kodi ya ushuru. Saivi kuna kuchangia Kodi ya Ujenz wa Reli.
 
hili jambo la TRA kuwa kamua wananchi wanapotaka kujikomboa kwa kujipatia kau safiri hata mimi nawaomba Serikali kupitia waziri wa Fedha walipitie upya maana ni kero sana Jamani.

Yaani ushuru ni mkubwa kuliko hata bei ya kununulia gari lenyewe!!!!!!!

Chonde chode serikali yetu Embu tunaomba mtusaidie wananchi wenu Ushuru huu umekuwa mzigo mzito sana.
 


Lkn pia linachafua mazingira, na ndiyo maana kodi ni kubwa ili ununue gari mpya ambayo haichafui mazingira sana, hiyo ndiyo sababu na Dunia nzima hufanya hivi kwa namna moja au nyingine!
 


Unatakiwa ununue gari mpya ambayo haichafui mazingira yetu hiyo ndiyo sababu!
 
Ndugu pole.Naona ulivyoandika ni kama umekuwa "taken in surprise" na huo mchanganuo wa hizo gharama. Ukiuliza humu katika JF kwa waliowahi kuagiza magari watakuambia kwamba huo ni utaratibu uliopo kwa sasa ambao kama ulivyosema unatoa maswali mengi zaidi ya majibu.Ni vyema next time ukitaka kuagiza gari tumia JF kupata ushauri (Kuuliza si ujinga) hasa katika mambo yanayohusu Kodi za kulipa Tra, website za kupata magari mazuri, jinsi ya kunegotiate nk.
Ahsante
 
Wewe hata gari huna halafu unabishana na wanaume. Pumbaf.


Wala sihitaji kwa maana najali mazingira yetu zaidi, hivyo TRA yetu wako sawa kabisa ukitaka nunua gari mpya ambayo ina teknolojia inayozuia uchafuzi wa mazingira!
 
hamna namna kodi italipwa tu, Ipande tu maradufu tuwe nchi ya viwanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…