DOKEZO TRA, TAKUKURU na Uhamiaji mko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bususwa

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
429
1,011
Nimekuwa mfanyakazi wa kampuni moja kubwa sana hapa Dsm kwa zaidi ya miaka Saba sasa, baadae nilipelekwa mkoani kwaajili ya kazi yangu hiyo hiyo,hapa sitataja Mkoa kwa sababu ya kuficha uhusika wangu kamili.

Hii kampuni imekuwa na mambo ya ajabu sana, tumeajiriwa kwa jina la kampuni x, lakini pesa zote zinapelekwa na kuwekwa kwenye kampuni, hii kitu niliwahi kuhoji kwenye vikao vya management, nikaishia kutishiwa kufutwa kazi! Hii Kampuni inafanya kazi ya kuuza bidhaa jamii ya chakula, Mkurugenzi wetu kwa kusaidiana na Mkuu wa fedha, wamekuwa wakisema tusitoe list ya EFD, hii itasaidia wao kukwepa kodi!

Niliwahi kuuliza iweje niwe na Mauzo ya Tshs 200,000,000 lakini EFD machine yangu inasoma Tshs 30,000,000 nilijibiwa kama hutaki kazi endelea kuwa unaingia kila Mauzo kwenye EFD machine, sababu na Mimi nina familia niliamua kukaa kimya!

Pia hii kampuni imeajiri watu kutoka jamii ya Asia, wakati hizi kazi wanazofanya wao hata sisi wazawa tunaweza kuzifanya bila shida yoyote kabisa! Watu wa UHAMIAJI mko WAPI?? Watu wa idara ya kazi mko WAPI?? Hawa wahindi wanatudharau sana sisi wazawa na baadhi ya wazawa wapo pamoja na hawa wahindi

Mhindi anafanya kazi analipwa Tshs 30,000,000,mzawa ambaye ndizo mzalishaji Mkubwa analipwa Tshs 500,000!

Mmiliki wa hii Kampuni kuna wakati hua anatuita sisi mbwa! Yaani anasema kabisa wewe Mbwa hebu njoo hapa.

Tatu hii Kampuni ilikuwa inaitwa kampuni x zamani,lakini wakaja wakauza kihuni na kuipa jina la kampuni y,hapo wataalum wa kodi mnaweza kujua kabisa kwamba,walikwepa hapa,ili waweze kupiga pesa!

Watu wa TAKUKURU hii Kampuni mkifanya kazi kwa undani kabisa, mtakuta kuna madudu mengi sana hapa, niliwahi report hili suala kwa moja ya wafanyakazi wa TAKUKURU sijui hili jambo liliishia wapi,hadi leo ni kimya kweli na watu wanazidi kufukuzwa kazi kwa sababu zisiso na misingi!

Mhindi anasema kabisa kama, watanzania wenzeni wanashindwa kuwasaidia sisi tutawasaidia vipi? Nenda kwetu kama utakuta Bwana Fedha wa kampuni ya India ni mtanzania, sana sana atakua anapiga deki kwenye vyoo tu huko!

Watu wa UHAMIAJI, TAKUKURU na TRA nipo tayari kutoa ushahidi wa kila kitu,kama tu mtakuwa tayari kunihitaji popote pale nitakuja.

Asanteni sana
 
Japo umeongea kwa uchungu kizalendo lakini hao uliowataja wakifika hapo watafata bahasha ya khaki na kuondoka. Thus mhindi kakuambia "kama watz wenzenu hawawezi wasaidia" jiongeze Acha Kazi
 
Japo umeongea kwa uchungu kizalendo lakini hao uliowataja wakifika hapo watafata bahasha ya khaki na kuondoka. Thus mhindi kakuambia "kama watz wenzenu hawawezi wasaidia" jiongeze Acha Kazi
Yaani acha tu! Tunadharauliwa sana tena sana!
 
Japo umeongea kwa uchungu kizalendo lakini hao uliowataja wakifika hapo watafata bahasha ya khaki na kuondoka. Thus mhindi kakuambia "kama watz wenzenu hawawezi wasaidia" jiongeze Acha Kazi
Mkuu kitaani pasikie tu! Nina jamaa yangu mmoja, hivi ana MBA na hana kazi! Kila siku ukiona simu yake ni kwamba anaomba Tshs 5000! Sasa nina mke na watoto ninafanyaje sasa? Naongea kwa uchungu walau basi, watulipe sitahiki za maana
 
Ilimradi wanakulipa mshahara we piga kazi jiongeze fungua kampuni yako.
Bora mkuu wangu, naomba kujua gharama zakufungua kampuni kama za usafi maofisni na kama za udalali!

Halafu walivyo wajinga sasa, wanasema uwe makini, usije kamatwa na TRA huko kwenye maduka ya watu,maana ukishikwa bila kutoa risti hilo ni lako! Ukitoa risit pia wana mind kwa nini umetoa risti
 
Nimekuwa mfanyakazi wa kampuni moja kubwa sana hapa Dsm kwa zaidi ya miaka Saba sasa,baadae nilipelekwa mkoani kwa ajiri ya kazi yangu hiyo hiyo,hapa sitataja Mkoa kwa sababu ya kuficha uhusika wangu kamili

Hii kampuni imekua na mambo ya ajabu sana, tumeajiriwa kwa jina la kampuni x,lakini pesa zote zinapelekwa na kuwekwa kwenye kampuni y,hii kitu
Hilo la kuajili watu wa kwao wasio na Sifa nikawaida sana nchi hii,kuna wachina walikuwa wanakuja kwenye kampuni moja ambayo niliondoka miaka kadhaa iliyopita,Kwa nafasi yangu na department yetu tulikuwa tunawapokea na kiwatafutia training ya kazi ambayo wanatakiwa kufanya,yaani wanakuja hata kushika mausi ya computer hawawezi...........pia kazi za kijinga jinga tu yaani mtu anaajiliwa (mchina) kazi yake ni kugonga mihuri nyaraka za kampuni..........Vibali vya kazi na kuishi kupata simple tu maana kila kibali wachina walitoa dola 300 Kwa maofisa wanaohusika.....

Kwahiyo mtu anakuja anapata mpaka kibali Cha kazi wakati hajui chochote.......na ujanja unao tumika kwenye vibali ni kuandika kazi kama Mechanic,Mashine operator, Business Manager etc........lakini wanakuja weupe kabisa........ kampuni za kichina majanga tupu wanaleta ndugu zao Tz,tuliokaa nao wanadai China maisha magumu sana na hali ya hewa mbaya,huku wakikaa mwenzi tu hata vimiili vinakuja.......maana wanapokuja duuh wanakuwa kama mtu anayeugua na hajapona vizuri.

Samia Ile kauli yake ya wawekezaji waje na watu wawatakao,daaah Ile ni fungulia mbwa nchini
 
Nimekuwa mfanyakazi wa kampuni moja kubwa sana hapa Dsm kwa zaidi ya miaka Saba sasa,baadae nilipelekwa mkoani kwa ajiri ya kazi yangu hiyo hiyo,hapa sitataja Mkoa kwa sababu ya kuficha uhusika wangu kamili

Hii kampuni imekuwa na mambo ya ajabu sana, tumeajiriwa kwa jina la kampuni x,lakini pesa zote zinapelekwa na kuwekwa kwenye kampuni y,hii kitu niliwahi kuhoji kwenye vikao vya management,nikaishia kutishiwa kufutwa kazi! Hii Kampuni inafanya kazi ya kuuza bidhaa jamii ya chakula,
Pole sana .
 
Kama malipo hayapiti kwenye EFD si ndio fresh, na wewe kula kwa urefu wa kamba yako hapo...
 
Bora mkuu wangu,naomba kujua gharama zakufungua kampuni kama za usafi maofisni na kama za udalali!

Halafu walivyo wajinga sasa,wanasema uwe makini,usije kamatwa na TRA huko kwenye maduka ya watu,maana ukishikwa bila kutoa risti hilo ni lako! Ukitoa risit pia wana mind kwa nini umetoa risti
Kufungua kampuni sio gharama sana inaanzia 150k na haizidi 1m. Inategemea na mtaji. We ndenda Brella watakusaidia.
 
Kama malipo hayapiti kwenye EFD si ndio fresh, na wewe kula kwa urefu wa kamba yako hapo...
Si rahisi kaka! Umepewa carton 100, umeuza 50,lazima wazione hizo 50 kama stock iliyobaki! Pia huwezi ongeza bei ya bidhaa,wateja wakipiga simu,kazi huna au unaambiwa unafanya sabotage kwa kuweka bei ya juu,ili mpinzani auze
 
Mhindi anafanya kazi analipwa Tshs 30,000,000,mzawa ambaye ndizo mzalishaji Mkubwa analipwa Tshs 500,000!
Kifupi wewe mleta mada akili huna
Unataka ulipwe sawa na wenye kiwanda au ndugu wa wenye kiwanda
Kiwanda cha muhindi akimlipa mhindi mwenzie hata milioni 100 hata kama kazi hajui wewe unskuhusu mini.Laumu umaskini wenu wa ukoo wenu ambao hauna kiwanda na nyie muajiriane mlipane mamilioni wakati kazi hamjui wanafanya wengine

Huwezi kutaka kulipwa sawa na mtoto wa Reginald mengi ITV kwa mfano kisa eti huyo mtoto analipwa mamilioni wakati hajui hata kutangaza tangazo la kifo na hakusomea uandishi wa habari!! Huwezi fanya kazi AZAM halafu kudai kutaka kulipwa sawa na watoto au nduguze hata kama mnafanya kazi moja inayofanana

Wewe rizika na mshahara wako kama hutaki acha kazi katafute kwingine hujazuiwa
 
Waliokuwa wanapambana kuondoa huu ujinga mlikuwa mnawatukana kuwa wanafukuza wawekezaji! Acha tukione cha moto nchi ndio imefunguliwa.
 
Back
Top Bottom