TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

Setuba Noel

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
426
Reaction score
210
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.
 
mkuu
mbali ya hiyo mashine leseni sasa ni.kuanzia tsh 200,000 hadi 800,000 wanaangalia uwezo wa duka kila mwaka.
_fire kila mwaka 100,000.
~taka sh 24,000kila mwezi.
na hizi zote wamemlenga mwenye duka.
sasa tumechoka kuwa chuma ulete,kesho mgomo unaendelea
 
mkuu
mbali ya hiyo mashine leseni sasa ni.kuanzia tsh 200,000 hadi 800,000 wanaangalia uwezo wa duka kila mwaka.
_fire kila mwaka 100,000.
~taka sh 24,000kila mwezi.
na hizi zote wamemlenga mwenye duka.
sasa tumechoka kuwa chuma ulete,kesho mgomo unaendelea

mkuu mimi bado sijakuelewa hii laki moja kwanini ilipwe kila mwaka? Inamaana kila mwaka wanakupa fire extinguisher mpya?
 
Kuwabebesha wafanya biashara kodi kubwa ni kama kuchezesha bahati nasibu bila kuahidi jackpot. Mwisho wa siku hakuna atakayecheza bahati nasibu na serikali itakosa mapato kabisa.
 
Mfanyakazi hana gharama???au mnazo nyinyi tu??acheni kulialia mlipe kodi
tatizo wafanyabiashara wengi hawana mazoea ya kulipa kodi na wamezoea kuwaibia wateja kwa ajili ya kutengezeza milima ya faida...jamani lipeni kwani mnategemeaje Tz kuwa kwenye nchi zilizoendelea bila ya kumpa kaisari cha kwake
 
Mfanyakazi hana gharama???au mnazo nyinyi tu??acheni kulialia mlipe kodi

tatizo wafanyabiashara wengi hawana mazoea ya kulipa kodi na wamezoea kuwaibia wateja kwa ajili ya kutengezeza milima ya faida...jamani lipeni kwani mnategemeaje Tz kuwa kwenye nchi zilizoendelea bila ya kumpa kaisari cha kwake

Subirini mfumuko wa bei utakapo anza mwisho wa siku anaumia mwananchi wa mwisho mlaji
 
Setuba Noel Ulichosema ni sawa kuwa mwenye mauzo ya kuanzia milioni 14kwa mwaka anatakiwa kuwa na mashine.Ila kwa taarifa yako kwa awamu hii ya pili hicho c kigezo pekee kinachotumika wao TRA walisambaza barua kwa wafanyabiashara 200,000 tz nzima ambao wanatakiwa kutumia mashine hizi awamu ya pili na ni wafanyabiashara wakubwa tu.

Sio kweli kama unavyodai kuwa kwa awamu hii hata mwenye mauzo ya 38,000 kwa siku anatakiwa kuwa na mashine,na wengi wanafuata mkumbo tu bila kujua.Na wafanya biashara wa kariakoo wengi wanafanya biashara ki magumashi ndio maana hawataki kusikiaa habari za EFD.Kwani mwanzoni walianza kuwa tatizo ni bei sasa wanadai hata wakipewa bure hawataki!

Which is which?

Ila Nashukuru serikali inapokuja na msimamo ambaye hawezi arudishe leseni na TIN. Akafanye shughuri nyingine,uone kama hawatafyata mkia.Kuna ubaya gani serikali kujua mauzo yako?

kama hakuna kitu unachoficha kwani ktk kodi mauzo ghafi ndio yataonyesha kiwango cha kodi unachotakiwa kulipa.
 
Last edited by a moderator:
mkuu mimi bado sijakuelewa hii laki moja kwanini ilipwe kila mwaka? Inamaana kila mwaka wanakupa fire extinguisher mpya?

kila mwaka watakuwa wanafanya ukaguzi wa mtungi na kukupa certificate.
kumbuka mtungi unanunua na auhusiani na laki moja.
na wanasema hiyo sheria imepitishwa na halmashauri ya jiji la mwanza ambayo na wenje yumo
 
kila mwaka watakuwa wanafanya ukaguzi wa mtungi na kukupa certificate.
kumbuka mtungi unanunua na auhusiani na laki moja.
na wanasema hiyo sheria imepitishwa na halmashauri ya jiji la mwanza ambayo na wenje yumo

cdm mza bure kabisa wametia lami barabara ya kwenda malaika hotel na kuacha barabara ya buswelu na kiseke inayotumiwa na wapiga kura wao.
 
kwa hiyo mnataka msilipe kodi? na wafanya kazi watasemaje? acheni kujibalagua lipeni kodi na mwaka huu wananchi wamewashtukia wala hawawaungi mkono
 
Kuwabebesha wafanya biashara kodi kubwa ni kama kuchezesha bahati nasibu bila kuahidi jackpot. Mwisho wa siku hakuna atakayecheza bahati nasibu na serikali itakosa mapato kabisa.

kodi kubwa ipi??kinachogomba hapa ni kuwa wafanyabiashara hawataki mauzo yao ghafi yajulikane,ili walipe kodi stahiki.kwani kuna wafanya biashara kama 16,000 hivi wanazitumia mashine hizi toka mwaka 2010!hii awamu ya pili inayo walazimisha wengine 200,000 watumie machine ndio inakuwa nongwa???hapa serikali lazima ishinde tu na ndio maana wamesema ambaye hataki arudishe leseni ya biadhara afanye shughuri nyingine.Hata wakati VAT inaanza ilikuwa hivi hivi.Na kwa taarifa yako wafanya biadhara wengi hususani kariakoo wanalipa kodi ya mapato kwa makadillio ya mauzo yao hawataki kusikia kitu kiitwacho VAT,wanacho fanya ni kipunguza kiasi cha mauzo kwa mwaka.ila kwa mashine ya EFD hawataweza tena kuficha kiasi cha mauzo na moja kwa moja watakuwa na sifa za kusajiliwa kwenye ongezeko la thamani (VAT) ndio mziki hapo.Haka kwa akili ndogo tu pale kariakoo mtu analipia kodi ya pango milioni moja kwa mwezi ila kodi ya mapato analipa laki 5 kwa mwaka!!!!
 
kulipa kodi watu hawakatai kichogomba ni wapi kodi inakatwa. Tra wanataka kuchukua kodi ya%20 kwenye mauzo yako ambayo wewe mwenye duka umeuza kwa siku,ambapo unakuta faida yako nindogo sana haifiki hata %20
 
Subirini mfumuko wa bei utakapo anza mwisho wa siku anaumia mwananchi wa mwisho mlaji
Khaa!! Mfumuko?? Kwa taarifa yako kuna watu wanaombea mgomo uendelee mwaka mzima. Wanauza balaa
 
Mfanyakazi hana gharama???au mnazo nyinyi tu??acheni kulialia mlipe kodi

mi ni mfanyakazi lakini nawasapoti wafanyabiashara.hata wakinunua hizo mashine bado mzigo ni kwetu sisi walaji.kama ujuavyo biashara za bongo ni maelewano.hatujafika hatua ya kuwa na fixed price.nguo ya elf 40 utainunua kwa 15000.just imagine wauza mitumba wa karume au mchikichini wawe na efds unategemea walalahoi tutavaa?.suruali ya ekf 10 utainunua kwa elf 25.ile ya dukani ya elf30 utainunua kwa 50.mshahara wenyewe laki 4 utaweza kuishi?usiwe na myopic minded.kabla ya kuropoka uwe unafikiria matokei ya kitu kwa mapana yake.sio tu ushabikie wafanyabiashara kulipa kodi bila kujua position yako itakuwaje kama mlaji katika mzunguko wa kibiashara.
kwa wafanyabiashara kulipa kodi ni sawa kabisa kakini kuwepo na utaratibu ambao hautaleta madhara kwaa end user.bei ya umeme imepanda maji nayo yamepanda kutoka50 kwa ndoo moja hadi 100 tsh.kwa uelewa wako mdogo hapo muathirika ni nani?unadhani ni tanesco au serikali?acha ushabiki usiokuwa na tija kijana
 
inacho uma zaidi hata hiyo kodi ikilipwa hainufaishi inchi Bali inawanufaisha wala nchi wachache
.mAdini na wanyama pori wanawamaliza na kuwafaidi peke yao hawawatoshi na sasa wamehamia kwetu wananchi
?
 
Back
Top Bottom