Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Tanzania bwana, hasa katika hii awamu ya uongozi, tutasikia kila namna ya mambo ya ajabu.
Hili la hivi karibuni la TRA kuwaambia timu ya Yanga na timu nyingine kwamba pale watakapoamua kuwaingiza mashabiki wao bure kuangalia mechi za mpira, bado watakatwa kodi. Sasa unajiuliza, ikiwa kodi inatakiwa kukatwa kutokana na mapato, msingi wa kuwakata kodi timu y mpira wakiamua kuingiza mashabiki bure ili wapate nguvu ya kushangiliwa unakuwa nini hasa? Je hii si itakuwa kwamba timu hizo zinakatwa kodi toka mapato ya awali yaliyotozwa kodi tayari? Kuingiza watazamaji bure maana yake timu inajiingiza hasara, sasa utakataje kodi sehemu yenye "negative" revenue, hasara? TRA wamefikia mahali ambapo "charity act" inatakiwa kukatwa kodi?
Tunaelekea kuambiwa kwamba ukitoa msaada wa aina fulani lazima ukatwe kodi, ambapo ni kinyume na kanuni za kodi.
Labda hii mbiu ya Raisi Magufuli ya kusema shule itakuwa bure inabidi iachwe sasa, maana toka itangazwe tumeona ni jinsi gani hii elimu sio bure kwa kweli - ni kama TRA sasa wameshikwa na munkari wa kukamua kodi kwa kila namna, hata zile ambazo hazikubaliki katika misingi ya kodi. Tumesikia kodi za kodi za taasisi za dini, malipo ya kiinua mgongo, miamala ya benki, utalii, na sasa charity acts - hivi hizi mbio za kodi za kulazimsha zitaishia wapi? Kama suala ni kupata fedha za elimu ya bure basi afadhali turudi kule kule kwa jana ili tusitwikwe mizigo ya kodi ambazo hazieleweki sasa! It is too much!