TRA/Polisi wamfanyia umafia hakimu Nyasige wa Mbozi

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Tarehe 1/4/2011 ofisa wa TRA Mbeya aitwaye Kasimba alikamata gari ya hakimu Nyasige likiwa na mwanamke aliyepewa rifti na hakimu huyo akiwa na vipodozi vya tshs 148,000/= hakimu huyo alikuwa na tshs 25,000,000/= ambazo alikuwa anapeleka benki. Ndani ya gari hiyo TRA wakiwa na polisi mkoani Mbeya walitaka wapewe rushwa kutoka kwa hakimu huyo, lakini mwenye vipodozi akakiri kuwa mzigo ni wake na hakimu hahusiki.

Polisi na maofisa TRA wakamnyang'anya hakimu huyo gari na kulipeleka kwenye ofisi za tra kwa upekuzi ambapo walipora pesa tshs 25m na kumufungulia hakimu kesi na 72/2011 mahakama ya wilaya mby.
Baada ya kesi hiyo kusomwa , bi Zena Mwakamela alijitokeza kumuwekea dhamana hakimu akatoka.

Baada ya hakimu kuanza kudai fedha yake 25m, tra na rco mby wakafanya njama ya kumuwekea tena hakimu huyo vipodozi ili akamatwe kwa mara ya pili.

Polisi walimtuma dereva wa tra aitwaye dominic mwaisumbi na kwenda kumuhonga mdhamini wa hakimu (zena) na kumupa fedha 200,000 akaenda kununua vipodozi na kumuwekea hakimu huku akiwasiliana na polisi Mbeya ofisi ya RCO.

Polisi walimpa maelekezo zena kuwa akiweka vipodozi asipande gari hiyo lakini yeye alikosea na kukamatwa kwa mara ya pili akiwa na hakimu.

Zena na hakimu walipelekwa rumande gereza la ruanda mby na hakimu akakosa dhamana, baada ya kupata mateso Zena akaamua kuandika maelezo ya kweli juu ya umafia wa polisi na TRA na njama za kumutuma kumuwekea vipodozi.

Baada ya kukiri mbele ya mahakama akapewa faini ya 600,000/= na TRA wakamulipia kwa siri akatoka rumande . Sasa jambo la kushangaza polisi bado wanamshikiria hakimu kwa visa huku wamepora fedha yake.

RCO Mbeya ameweka msimamo wa kumnyima dhamana hadi leo.
 

Attachments

  • POLISI T.R.A MBEYA.pdf
    320.9 KB · Views: 128
hivi mahakimu hawana chama? mbona haendi hata kujua nini kiunaendelea kwenye kesi ya mwenzao?
ila polisi wa nchi hii ni tatizo, sito jali sana kama hii habari ni ya kweli au ya uongo ila polisi wa nchi hii wamepinda sana tu

hakimu anajua sheria apambane nao hakitoka na atende haki kuanzia hapo kwenye kazi yoyote hatakayo pata
 
I know the inshu, yule hakimu ambaye awali alikuwa askari polisi kabla hajaenda kusoma na akaacha kazi ya polisi ni kweli alikuwa dealer mzuri sana wa biashara ya vipodozi. c suala la kufanyiana umafia, anashirikiana na jamaa wa Tunduma kule ktk biashara na one of the guys ni bwana ake. However bado polisi wetu ni hovyo sana katika ufanyaji kazi wao
 
ila kweli hata hiki kisa kina maswali mengi, kama huyo hakimu alishashikwa na huyo mwanamke akiwa na vipodozi inakuwaje tena anaendelea kumpa lift?
na hiyo milion 25 alikuwa ameitoa wapi? kuna account yake yoyote inayooshesha hizo ni hela safi alizitoa bank? au ana biashara kuonyesha hayo ni mapato kutoka kwenye hiyo biashara?

mtu kama hakimu wa wilaya kuwa na milioni 25 kwenye gari CASH kuna maswali mengi kuliko majibu,
je ni rushwa, wizi, au hela ya vipodozi vilivyokwisha uzwa?
 
safi sana wacha hawa mafisadi, wanyonyaji na wadhulumu haki za watu waumizane. hakimu huyo akitoka hapo atajifunza ubaya wa kuonea wa TZ
 
Mimi nashindwa kuelewa ni kwa nini polisi na tra wafanye njama za kumuwekea hakimu vipodozi ili akamatwe halafu akose dhamana. Kama huyo hakimu ni delear mzuri wa vipodozi kwa nini wasimkamate na hivyo vipodozi mpaka wana mubambikizia.

Tuna wafanya biashara wengi sana wa dawa za kulevya lakini huwezi kununua dawa za kulevya na kwenda kumuwekea halafu ukamukamata.

Polisi tunduma walikamata 50kg za heloni wakapeleka kwa rpc, lakini ploisi hao hao wakaiba 8kg mpaka leo hazijulikani.

Kesi ya dawa za kulevya mwaka 2006 zilizo kamatwa tumboni mwa marehemu kombo siriri , kesi imehujumiwa na polisi mby mpaka leo.

Ni aibu kwa tra kutumia nguvu kubwa kumukamatisha hakimu vipodozi badala ya kukamata shehena kubwa zinazo vuka mpaka dsm.


Kama zene mwakamela amekili ametumwa na tra kumuwekua hakimu vipodozi , uadilifu wa tra kumunyima hakimu dhamana uko wapi???
 
Hakimu amekamatwa na vipodozi vya 200,000 lakini polisi wameiba 25,000,000/= sasa hapa nani mhalifu???
 
Hivi dawa za kulevya na vipodozi vinavyo kamatwa huwa vinapelekwa wapi???
 
Bora wabambikiane kesi wenyewe kwa wenye, Hakimu na Polisi wote lao moja Polisi wanapeleka raia asiyekuwa na kosa Mahakamani na Hakimu bila ya kuuliza au kuangalia ushahidi wanamfunga mtu. Sasa waacheni wafungane wenye kwa wenyewe, Pumbafu zao wote TRA, POLICE na HAKIMU
 
hapa kuna maswali mengi kuliko majibu. hizo hela kapata wapi? kwa mshahara wa hakimu take home yake kwa sasa 600000
hawezi pata mkopo unaozidi mil 10. labda tusema kauza nyumba ok
hata hivo iso ishu sana ni kwa nn anyimwe dhamana kwnai kosa lake halimzuii kunyimwa dhamana
na yeye kama hakimu hawezi kutoroka na sio kosa la kumfanya jamii imuadhibu kama vile jambazi au mbakaji,

nadhani kuna kukomoana hapa hyu mama namfahamu amekaa kigoma pia kama hakimu yupo serious akiwa kazini
na sii mtu wa kucheka cheka hovyo kama waswahili ni damu typical kutoka mkoa ule wa walyanchanki na walyanchori.
labda akiwa polisi mbeya kuna ishu aliwakomoa hao hao wanaomwandama.

lingine mume wake alifariki miaka 2 au 3 ilopita sasa kaolewa lini kwani hata ndoa hiyo hatujaisikia
sasa anaejiita mume wake pia inatia shaka yawezekana ndio hao hao tena mchaga tena
kamuuza huyu hakimu,lol makubwa..sijajua kama ungozi wa mahakama kanda ya mbeya unafanya jitihada zozote kufuatilia hali hiyo.
pole mama nyasige kama uko innocent soon utapata haki yako.
 
hi kali tangu lini hakimu akafunga mtu bila kujiridhisha na ushahidi wa pande zote?? hakimu ni sawa na mizani anatoa hukumu pale mizani inapoelemea. sio rahisi kwa dunia ya sasa hakimu afanye ujinga kama huo unaosema labda kama ni wale wazee kwani hakimu akifunga mtu lazima watakata rufaa na yeye sio mjinga aonekane hajui kazi mbele ya maboss wake kwani hatapanda daraja. labda ww ni wale wale mnaokuwa na dhana hasi kwa mahakama. hakimu atakufunga bila kuridhika na ushahidi? au ww ndio unataka hata vibaka na majambazi waachiwe kwa vile ni ndugu zako?? acha mambo ya kizamani na ya kijiweni kasome hata certificate uelewe japo sheria kwa ufupi.

Bora wabambikiane kesi wenyewe kwa wenye, Hakimu na Polisi wote lao moja Polisi wanapeleka raia asiyekuwa na kosa Mahakamani na Hakimu bila ya kuuliza au kuangalia ushahidi wanamfunga mtu. Sasa waacheni wafungane wenye kwa wenyewe, Pumbafu zao wote TRA, POLICE na HAKIMU
 
Tanzania inaelekea wapi? Milioni 25 ni nyingi sana kuna visa ambavyo vipo chini ya kapeti vimefichika so ni ngumu kuamua hiyo kesi na kama RCO naye yumo ndani na hiylo dili hapo pagumu.
 
Kazi ya polisi ni kulinda haki na sio kuba mbikizia kesi ,
tra mby wamekosa uadlifu kwani hapo kuna kashifa nyingi.
Kwani tra watumie pesa za walipa kodi kununua vipodozi na kumubambikiza hakimu???
 
Back
Top Bottom