TRA ni kiboko sasa

TRA ni kiboko sasa

malogi1976

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
297
Reaction score
168
Nyie TRA ni kiboko yani wamekuja hotelini na kuuliza wateja wangapi wamelala nikawaambia na kuwaonesha kitabu mpaka hapo sawa baada ya hapo leta Risiti nikawaambia wateja hulipa siku wanayotoka mara napewa barua na maofisa kwa kosa la kutotowa Risiti.

Kwanini mnakuwa waonevu nikaenda the next day kuripoti na kumuona ofisa mwingine naye akawa anashangaa wakati mteja hulipa siku ya kutoka hotelini. Kwa kweli TRA hawasikilizi mtu na hii ni too much Kwa kweli.

Tunaomba mtueleweshe kuhusu hili jambo kwa ufasaha na kama mtu mwingine amekumbwa na hili naomba atuambie.
 
Nami nashangaa wakati wanatakaga cha kwao mapema.usipolipa asubuhi hao mlangoni

Mtoa habari wakati mwingine uwe unafikiria kabla hujaleta Uzi. Hivi wapi Tanzania hii wakuache ulale eti siku ya kuondoka ndiyo ulipe? Tusidanganyane kama wazee wa kodi wamekudaka basi tulia dawa ikuingie.Bora Hata ungedanganya wachache bado. Nielekeze ni hoteli IPI nashida na roomvkwa short reason maana nategemea dili language litabuma baada ya masaa 2 nikimaliza ntakulipa.
 
Ningekuwa nimedakwa nisingeandika na hawajanifungulia kesi wameiacha wenyewe waliangalia vyumbani wapo ngapi na kwenye kitabu wapo wangapi kwahiyo nisingeandika Kama nimedakwa ni sababu sitaki usumbufu wakati manager wao anasema mteja alipe akiwa anaondoka! Kama umewahi lala hotel utaelewa
 
Ila nawe unatupiga kamba,
Mteja alipe siku ya kuondoka je akiingia mitini?
 
Nyie TRA ni kiboko yani wamekuja hotelini na kuuliza wateja wangapi wamelala nikawaambia na kuwaonesha kitabu mpk hapo sawa baada ya hapo leta Risiti nikawaambia wateja hulipa siku wanayotoka mara napewa barua na maofisa kwa kosa LA kutotowa Risiti. Kwanini mnakuwa waonevu nikaenda the next day kuripoti na kumuona ofisa mwingine Naye akawa anashangaa wakati mteja hulipa siku ya kutoka hotelini.kwa kweli tra hawasikilizi mtu na hii ni too much Kwa kweli. Tunaomba mtueleweshe kuhusu hili jambo Kwa ufasaha na Kama mtu mwingine amekumbwa na hili naomba atuambie
mkuu vumilia tu usijeitwa mchochezi we lipa tu
 
Kaka umesema ukweli hapo hao tra walikuja kwetu wakajua watakula hela nikawafuata hapo gerezani nikawafyatua wakatulia wenyewe ...eti wasema mteja akilala mpe risiti hata kama hajalipa na kama akicancel kulala zaidi ya siku moja basi uandike barua kwao ....pambaaf
 
Mashine zenyewe za efd siku 3 sasa zinasumbua network hata z report hazitoi....waambie hao watu wa tra wakuonyeshe sheria ya hotel na huduma inayosema utoe risiti kabla mteja hajafanya chekout...wakikutisha wanaandika faini waambie sawa andikeni halafu hakuna kulipa
 
Mwenzangu nilienda Na kumwambia meneja Ili watuelimishe naye akasema nyie nendeni hamtasumbuliwa tena sielewi tatizo humu wengine wanafikiri Kila mtu hataki lipa Kodi sidhani Kama ni wafanya biashara Hawa watu tunataka kuelimishwa na tra Mtu anasema nimekamatwa watanzania Kila kitu kuweka negativity aisee
 
Kaka jana nimesema "mjinga muache na ujinga wake ukibishana nae unakuwa mjinga" wengine hapa kodi gani inalipwa hawajui wewe piga hatua na tra wasikuzingue sasa tuntumia sheria yao wenyewe kuwakomoa
 
Hao officers kuna malengo wamewekewa kiasi cha kukusanya, sasa kama kila mwezi unakusanya kodi chini ya malengo unapewa haati chafu. Maofisa wa TRA hiyo inawasumbua sana ndo mana waanakuwa hivyo
 
Wewe wamekuweza maana ulikuwa unataka kuwadanganya eti wateja hulipa siku wanaondoka? Hotel ya wapi hiyo? Mkwepa kodi mkubwa wewe!
 
kodi zenyeww tunazokusanya wanazichezea huko sijui chato eapoti. Sasa mimi chato ya nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom