TRA na Ushuru wa magari toka Japan, shida ni nini?

Leo nimekuwa nikipitia tovuti ya TRA na hasa ile sehemu ambayo unawezakukokotoa kiasi cha ushuru (Tax) utakachopaswa kulipia kama ukiagizia gari toka nje ya nchi (Japan kwa mfano), nimeshangaa kuona makadirio yao ni makubwa mno.

Mfano gari ndogo Toyota Avensis ya mwaka 2010 ambayo CIF (cost, insurance and freight) yaani bei yake mpaka bandarini Dar kabla ya kulipia ushuru ni USD 5600 (TZS 12,769,535) hii calculator yao inaniambia nitalipia ushuru wa TZS milioni 10.2, Hivi ni kwa nini? Yaani gari ninunue milioni 12.8 kisha ushuru nilipie milioni 10.2? asilimia 80?

Hiki ni kiwango kikubwa sana kwa mawazo yangu, lengo lao ni kuwa-discourage watu wasinunue magari? Ama kuna kitu sielewi? Kuna wanaojua ukweli wa haya mambo? Tafadhali nipeni elimu kidogo!

View attachment 789250
Inaelekea Wewe Ni Mgeni Kwenye Uagizaji Wa Magari, Yaani Ushuru Unakua Ni Zaidi Ya Bei Ya Kununulia Gari, Tena Hata Hiyo Calculator Usiiamini, Nenda Ofisi za TRA Physically, Wakupigie Wenyewe Mahesabu Yao, Hiyo Mil 12 ya Ushuru Inabadilika Inakua Mil 16
 
Mkuu mambo ya zenji waachie wenyewe. We sikia hvyo hvyo ukipata ukweli wenyewe huto amini.
Tena ikiwezekana wapunguziwe zaid
Mkuu wabara waliopo zenji wanaenjoy kweli urahisi wa kumiliki magari, wakimaliza wanauza zao fresh, moto upo huku, rangerover autobiography ya mwaka jana ina ushuru mkubwa kuliko scania la miaka kumi double trailer....
 
Bongo mtu akimiliki Harrier,fortuner tunajua tajiri ila natembea hapa south Africa mpaka nashangaa sina ya magari mazuri na mapya raia wanamiliki. Kutokana na ushuru Mkubwa ndiyo Maana watanzania wananunua magari makongwe yanayo chafua mazingira (hewa),pia ajali za mara kwa mara kutokana na uchakavu.
Unafaa kuwa mbunge, yaani umeona mbali, ila hivi vilaza vyetu hawaoni
 
Serikali badala ya kuweka ushuru ambao watu wataumudu, watu waagize magari, uchumi ukue, serikali ipate ushuru zaidi,inafanya tofauti.

Inatoza ushuru mkubwa ajabu,watu wanakuwa discouragedkuagiza magari, uchumi unadhoofika, na mapato ya serikali kwenye kodi yanashuka.

Kifupi, serikali inakimbiliakuwafanya wananchi kuwani chanzo cha mapato, na kuua uchumi, badala ya kukuza uchumi na kuongeza kodi kutokana na uchumi kukua.

Kwanini wanaweka kodi kubwa kweli kila kitu? Hata bidhaa nyingine kodi inakuwa nusu ya bei ya bidhaa hiyo
 
Inaelekea Wewe Ni Mgeni Kwenye Uagizaji Wa Magari, Yaani Ushuru Unakua Ni Zaidi Ya Bei Ya Kununulia Gari, Tena Hata Hiyo Calculator Usiiamini, Nenda Ofisi za TRA Physically, Wakupigie Wenyewe Mahesabu Yao, Hiyo Mil 12 ya Ushuru Inabadilika Inakua Mil 16
Ni kweli mkuu, sijaagizia gari toka mwaka 2007, kipindi kile hali haikuwa mbaya kiasi hicho, in fact jumla ya kodi yote ilikuwa nusu ya CIF (mfano gari yangu iligharimu USD 5000 kutoka Japan hadi Dar na tax ikawa USD 2500)! Ushuru wa hivi sasa ni kukomoana na actually ni kuzuia serikali kupata mapato yake kwa wingi.
 
Bongo mtu akimiliki Harrier,fortuner tunajua tajiri ila natembea hapa south Africa mpaka nashangaa sina ya magari mazuri na mapya raia wanamiliki. Kutokana na ushuru Mkubwa ndiyo Maana watanzania wananunua magari makongwe yanayo chafua mazingira (hewa),pia ajali za mara kwa mara kutokana na uchakavu.
Mkuu upo sahihi, nadhani hata Kenya hali ni tofauti kabisa na Tz! Anyway, ngoja tupambane na hali zetu!
 
Mkuu hiyo yako ni scenario moja tu..kuna zingine ukiingia kwenye hiyo claculator unajikuta unalipia gharama sawa au zaidi ya CIF unapoingiza gari.

Wale mabingwa wa kushangilia tu kila kitu wanasema ni sawa lipa kodi ila kama uko na reasoning ya kutosha utaona kuna tatizo pahala....
Na unajiuliza hivi tumefikaje hapa lakini?
 
Trend kuagiza magari imeshuka watu wananua gari hapa chini hususani ya watu sababu ndo bei nafuu. Mfn bei ya ist 2003 km68000 ni $2600 n ushuru milioni 5 alafu rim sio sport. Hapa hapa tanzania unalenga ist no. DL KM 80000 AU 90000 RIM SPORT NA AIJAGOGWA WALA KURUDIWA RANGI KWA M.8 TU.
Bro ya $2600 na ushuru milioni 5 si ndio yale yale kama ya mwanzisha mada. Kodi iko juu.
 
Kabisaaaaaaaa

Waziri wa Mazingira aanze yeye huko..
Mkuu hapa natofautiana na wewe. Hakuna Mtanzania anayeweza kununua gari jipya, kama wapo hawafiki hata asilimia 5. Ukiongelea uchafuzi Wa Mazingira ni siasa za uongo, magari hayachafui mazingira, viwanda ndio mchafuzi Wa mazingira, embu fikiria vijijini tunakopika kwa kuni kila nyumba, mazingira ni salama. TRA inapaswa kupunguza ushuru Wa magari, unaponunua gari serikali itapata kodi kwenye gari,mafuta, vilainishi na spare. Kuna haja ya kuliangalia tena hili.
 
Kulinda uchafuzi wa mazingira ni muhimu kuliko kupata fedha nyingi!
Trump ameruhusu uchimbaji makaa ya mawe na anakuambia Uchafuzi Wa mazingira ni siasa. Lakini sisi tunaiga tu hii .Tuna viwanda vingapi kama China na India.
 
Mkuu hapa natofautiana na wewe. Hakuna Mtanzania anayeweza kununua gari jipya, kama wapo hawafiki hata asilimia 5. Ukiongelea uchafuzi Wa Mazingira ni siasa za uongo, magari hayachafui mazingira, viwanda ndio mchafuzi Wa mazingira, embu fikiria vijijini tunakopika kwa kuni kila nyumba, mazingira ni salama. TRA inapaswa kupunguza ushuru Wa magari, unaponunua gari serikali itapata kodi kwenye gari,mafuta, vilainishi na spare. Kuna haja ya kuliangalia tena hili.

Yesu na Maria..
 
Sasa hapo ndipo wanapokosea, mimi kwa uelewa wangu nilifikiri ingebidi wachaji kodi kubwa zaidi kwa gari za zamani ili ku discourage wananchi wasiagize magari kuu kuu ambayo huchafua mazingira na yana asilimia kubwa kusababisha ajali.

I stand to be corrected.
uko sawa kabisa mkuu kwenye suala la utunzaji mazingira. Ila, ni wananchi wangapi wataweza ku-afford kununua gari ambazo si za zamani sana (na pengine mpya) ilhali vipato vyetu kwa kiasi kikubwa bado viko chini?

Tatizo ni income mkuu, waki-discourage magari ya zamani wengine tutashindwa kabisa kutimiza ndoto zetu za kumiliki magari mkuu
 
Back
Top Bottom