TRA na ushuru wa kuingiza gari


si ndio hayo macontena yalikuwa yanapita bila kodi halafu wao humu ndani wanayawekea kodi
 
Ni wizi na unyonyaji, ukaguzi wanaoufanya ni sawa na ule unaofanywa na garage za kawaida (MOT) kwa ?40 lakini wao wanachaji $200.
 
Hii kitu mbaya ndio maana watu wanaishi kuendesha magari mabovu na sio vizuri kwa usalama barabarani sababu wakitaka kubadili wanafikilia kodi.
 
Ni wizi na unyonyaji, ukaguzi wanaoufanya ni sawa na ule unaofanywa na garage za kawaida (MOT) kwa ?40 lakini wao wanachaji $200.

Mkuu huu ni ufisadi tena wa hali ya juu. Halafu hizo tenda zilitolewa kwa ufisadi bila kufuata utaratibu.
 
wakati wa nyerere baiskeli zilikuwa zinakatiwa leseni na zilikuwa na namba kama magari, kumiliki gari ulihitaji kibali cha ikulu kupitia shirika lililoitwa state motors corporation na mtoa vibali mkuu alikuwepo mama mmoja wa kipare na jamaa mmoja wa kisukuma nafikiri aliitwa fumbuka.

leo hii sijui hatakama serikali inajua kuna baiskeli ngapi nchini, huko vijijini bodaboda wala hazina usajiri zinaendeshwa na watoto kama baiskeli. Hili la magari tusione magari ni kitu cha anasa tuone ni chombo tu kama vile fridge jiko la gesi etc, yatozwe ushuru wa kawaida tu. Leo unaagiza kari kwa mil tatu unalipia ushuru mil 15 ndo nini sasa, udokozi tu wa mchana. Wakati tunakamua wananchi na mikodi ya ajabu akina bhakresa wanapitisha mikontena chungu mzima bila kodi, siku moja mungu atawalipa.
 
si ndio hayo macontena yalikuwa yanapita bila kodi halafu wao humu ndani wanayawekea kodi

Ni kweli mkuu, kwny moja ya zile containers inaonekana range rover vogue ikiwa imefichwa kwa kufunikwa na fenicha za ndani!

Ni ngumu sana kushindana na watu wa aina hii!😉
 
Hawa jamaa wamepandisha ushuru wa kuingiza magari kumbe nao ni wizi tu. Unanunua gari mill 7 ushuru TRA unalipa mil 20. Huu ni uwendawazimu kabisa. Haiingii akilini.
Wakuu inawezekana tunalipa ushuru mkubwa sana, na hivyo serikali inapaswa itusikilize. Lakini pia jaribu kulinganisha ushuru walipao wenzetu Kenya kwa kutumia calculator ya Tanzania, na Kenya. Inaonesha Kenya wanalipia maradufu.
Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools
KRA Motor Vehicle Import Duty Calculator
 
Siyo tu zisimamishwe.... wapigwe faini kubwa sana. Na ihesabiwe wameingiza kwa dhuluma pesa ngapi tangu waanze. Zikusanywe, zirudishiwe wenyewe wa halali, ili liwe fundisho.
Hapa JK pia ana mkonoooo.....au ni uzembe wake tu wananchi wanadhulumiwa hivyo. Huyu jamaa hakuwa kbisa na huruma wala uchungu na wananchi. Akamatwe!
Wakati watu waandamane kumwunga mkono JP..............jamaniiiiii!
 
Ndugu yangu fanya utafiti. Magari yapo kwenye mitandao na TRA calculator ipo kwa weside yao. This is the plain truth. Kodi zipo juu mnoooo

Kodi zipo kisheria kutokana na uchakavu wa gari lenyewe au la kifahari n.k so sio kusema gari m7 kodi 20m griiiii! it dependi gari yako either umepewa zawadi au umenunua kwa mtu mwenye shida kakuuzia kwa bei poa au umenunua kwa bei ya offer is up to you huku tushawekewa standard yetu hizo hizo gari ukiuziwa kwa bei juu kuliko kodi itakuwa ni ile ile kwa mwenzako aliyeuziwa kwa bei ya offer au zawadi.... tuwe wawazi sio kuponda kwa kupitiliza.... la muhimu tuombe kupunguziwa kodi na wabunge wetu ndio waliotunga.... na tuache kununua mitumba tuzoee vipya au hamjui ni raha magari mabovu ni sawa na jini litakunyonya hakika
 
Ni kweli mkuu, kwny moja ya zile containers inaonekana range rover vogue ikiwa imefichwa kwa kufunikwa na fenicha za ndani!

Ni ngumu sana kushindana na watu wa aina hii!😉
Mkuu usiamini kila caption ya picha. Ni kawaida sana mtu kusafirisha gari, hasahasa toka Ulaya kwa kujaza na vifaa vyake kwenye container. Container husaidia sana kukwepa kuibiwa vitu. Lakini kuweka gari kwenye container haimaanishi halitoonwa, labda muamue kutoliona tu, ambapo kutoliona si lazima lifichwe kwenye container.
Picha iliyokuwa inasambazwa ni ya watu wanafunga Vogue ikae vizuri kwenye container kabla ya kusafirishwa. Usiamini kila kitu mkuu.
 
Dadavua hilo la TBS na tenda za kifisadi!?
 
Sawa mkuu Mlaleo. Ila issue hizo standards zilizowekwa ni za kinyonyaji. Halafu unvyoongelea magari mapya jua pia kwamba kodi ya gari jipya ni juu mno. Better used. Anyway issue kubwa ni hawa watu wafikirie namna ya kupitia upya hii sheria. Waweke ushabiki wa kisiasa pembeni na wafanye kwa maslahi mapana ya taifa.
 

GDP ya Kenya na tz ni saw a? Je marginal propensity to earn or consume tz na Kenya iko sawa? Compare na per capita income ya izo nchi mbili. Generally and intellectually huwezi linganisha ivo bila kuangalia economic environment ya izo nchi mbili.
 

Mlaleo ilo ndio tuliloomba wala hatusemi ni kinyume na sheria. Ila sahihisho, wabunge hawatungi kwa kutoa nani halipe sh ngapi, ilo upangwa na wataalamu wa wizara au taasisi husika za serikali. Rates and charges hawatungi wabunge, wao utunga sheria.
 
Ni watu wangapi wa kawaida wanaweza Kumudu kununua gari jipya?Lawama kubwa ziende kwa wabunge especially wa ccm (ndo kwa wingi wao)wangeweza kabisa kuzuia dhuluma hii ovu.TRA tunawalaumu bure,wanatekeleza sheria.
 
Wana calculator lao hilo ni hatar.. Unaingiza sijui mwaka, CC, model hio bei inayotoka hapo..utajuta!!! Bora mie na baskeli yang
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…