pole sendeu,
endelea kutafuta kazi mahali pengine, mtu kuitwa interview kwa nafasi mbili tofauti kwa wakati tofauti ni jambo la kawaida, aidha kurudia kwa sehemu ya maswali haimwongezei mtu nafasi ya kushinda hiyo usaili. kuitwa zaidi ya nafasi moja inaingeza probability ya yeye kupata kazi toka TRA. ila kwa maswali kurudia haina msingi, swali laweza kuwa ni moja , lakini likawa linapima kwa kiwango tofauti- hii ikafanya marking scheme ikawa tofauti. labda tahadhari kwa wengine, tusichukulie maswali kiurahisi. ni kama unakwenda intetview saa saba mwenzio alikwenda saa nne asbui, hata akikwambia alichoulizwa waweza ukajikuta ukikosa kazi.
huenda kulikuwa na vimemo, na watu hawakuwa na sifa... lakini ni kwa kiwango gani tuna uhakika wa hilo???. mwisho wa siku TRA wangeajiri idadi ya watu waliotakiwa, kwahiyo lazima kuna watu wangekosa nafasi, sasa kama huna ushahidi, TRA watasema wewe unalalamika kwa kuwa umekosa. Kaza buti interviews zijazo, usikatishwe na TRA na Mumbe University