TRA na malipo ya fire inspection - nini maana yake?

Vyote viwili ROAD LICENCE NA FIRE INSPECTION sio kodi bali ni adhabu ya kumiliki gari TANZANIA. Lakini kwa vile tumelogwa na mlogaji wetu alikufa hatuna mtu wa kutuzindua tutaendelea kuumizwa hivi hivi,bunge letu tukufu lililidhia wizi huu.
kama kila litre ya mafuta niwekayo kwenye gari langu ina tozo rasmi kwa wenye gari kwa ajili ya road fund,the road licence ni ya nini ? Fire inspection ili kiwe nini ? fire wameamua kujitafutia kipato toka kwa wenye gari, kwa nini nilazimishwe kukata bima ya gari na nilizamishwe kununu fire extinguisher ? kama bima ni pamoja na gari ikiungua kwa nini iwe lazima kwa mimi kuweka kifaa cha kuzimia moto na si kwamba hicho kifaa kitolewe na kampuni ya bima ambayo inataka kupunguza risk kwa ajili ya moto ?
Kwa kweli wigo wa rushwa kwa trafiki wetu unapanuliwa kila iitwapo leo.
 

Wizi, wizi, wizi, serikali ccm hata haya hawana. Leo nimesimamishwa naulizwa sticker ya sumatra? Ndio kitu gani hicho?
 
Mimi ni mtanzania mwenye ki tipa cha mchanga.
Kwa kifupi kwenye kioo cha mbele panatakiwa pawe na stika zifuatazo kwa mwaka:
1.Road Licence 240,000.00
2.Bima 120,000.00
3.Manispaa 10,000.00
5.Sumatra 10,000,00
6.TRA Mapato 520,000.00 (hii wanaruhusu kulipa hata kwa instalment)
7.Wiki ya Nenda kwa Usalama 7,000.00
Yaani kioo changu kejaa vistika hadi nashidwa kuona mbele sawasawa!
 
hili swala ni kama la NSSF tu.......ni Tanzania tu inayo,Kenya hakuna,Uganda hakuna,Rwanda na Burundi hakuna,kwa wenzetu ukilipia road licence ndo umemaliza kila kitu.
 
Nilipokumbana na hilo nikalilia taifa langu kwanza ndo nikalipa?Wangekuwa wanatoa hata mtungi ingekuwa sio wizi mbaya lakini kwakuchukua elfu 30 na ukienda fire wanataka kumi yakukagua mtungi nchi imeelaaniwa.
 
Huu ni wizi mwingine, mchana kweupe,kuna hitajika juhudi, wabunge wetu wasaidie katika kupinga hili, kwani insurance tunayokata ina cover moto pia.

Kama una bahati mbaya basi ni wewe! Mkuu huna mbunge wewe! Hawa jamaa wakiingia tu bungeni kitu ya kwanza wanahongwa gari! Watakukumbuka wewe? 40,000 kwao issue ndogo sana! Kikao kimoja tu wanalipa kila kitu! Why worry about Eeka Mangi with his/her Volkswagen beetle inherited from his grandfather? Walisema MWENYE KUSHIBA HAMJUI MWENYE NJAA.
We need a very serious government. Mtanisamehe sana ila what I believe its totally different. Niliwahi kuwinda na wale jamaa Wahadzabe kule Mang'ola! Wale jamaa wanatoka kwenda kuwinda amini usiamini wakipata tu hupekecha moto na kuchoma kile walichokipata then huwapelekea mabaki kama sio ngozi! Viongozi wenu wana utapia mlo mpaka washibe ndo wawakumbuke. Tunahitaji viongozi wasio na utapia mlo!
 

Napendekeza ili lisisubiri CCM kuondoka madarakani, wabunge wetu bila kujali wa chama tawala au upinzani watake maelezo kutoka serikalini haya malipo ya nini hasa? Kama ni kwa ajili ya fire inspection hiyo kazi inafanyawa saa ngapi baada ya mwenye gari kulipia Tshs. 30,000?

Tiba
 

Mkuu tupo pamoja lakini nina amini kuna baadhi ya wabunge wanaweza kulipigia kelele hili!!!!

Tiba
 
Nilipokumbana na hilo nikalilia taifa langu kwanza ndo nikalipa?Wangekuwa wanatoa hata mtungi ingekuwa sio wizi mbaya lakini kwakuchukua elfu 30 na ukienda fire wanataka kumi yakukagua mtungi nchi imeelaaniwa.

Sasa kama fire wanataka Tshs.10,000 ili wakague mtungi hizo elfu 30,000 au 40,000 tunalipa za nini tena? Huu wizi unafanyika kwa baraka za serikali, it is a shame!!!!!

Tiba
 
hili swala ni kama la NSSF tu.......ni Tanzania tu inayo,Kenya hakuna,Uganda hakuna,Rwanda na Burundi hakuna,kwa wenzetu ukilipia road licence ndo umemaliza kila kitu.

Kwa wenzetu wa Kenya, road licence inalipiwa mara moja pale unafanya importation ya gari. Hakuna haya malipo ya kila mwaka hata kidogo. Sisi hapa tunakamuliwa na mafisadi mpaka tone la mwisho la damu.

Tiba
 

Sasa uliza hizo pesa zote zinapelekwa wapi? Kujenga mahekalu na kuwapeleka mafisadi India kuangaliwa afya zao!!!!

Tiba
 

Ndugu yangu huu ni wizi mtupu anaofanyiwa nwananchi na serikali yake.

maana yake wananchi tumelala usingizi wa pono wajanja wanajineemesha!
 
Nimechukia siwezi changia kidogo nipige mtu tra mwezi wa nanekwa ajili ya fire.......
 
Siyo kwenye magari tu,saivi wamehamia kwenye maduka na pikipiki ambapo wameanzisha kulipia fire extungisher yan ni wizi mtupu
 
Siyo kwenye magari tu,saivi wamehamia kwenye maduka na pikipiki ambapo wameanzisha kulipia fire extungisher yan ni wizi mtupu

Inawezekana wana sababu za msingi za kufanya hivyo lakini wananchi tunapashwa kuelimishwa na kueleweshwa hizi pesa zinakusanywa kwa ajili ya nini? Na mbona hizo sticker zisitolewe pale TRA wakati wa kuchukua road licence au watoe maelezo ya wapi unapashwa kwenda baada ya malipo!!!!

Huu ni wizi uliokomaa kabisa unaofanywa na serikali!!!

Tiba
 
Sasa kama ni fire inspection kwa nini wasilipwe watu wa Fire brigade ili wafanye hiyo inspection. TRA inawahusu nini watu hawa? Mwishowe tutaambiwa hata bima, nenda kwa usalama (kituko kingine hiki) na regular services tukalipie TRA maana wanatafuta kila namna kukamua pesa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…