TRA na Kuregister Magari- Mmechemsha Vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA na Kuregister Magari- Mmechemsha Vibaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bobby, Jul 22, 2009.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Sifahamu kama baadhi yetu mmekwisha onja adha ya utaratibu mpya wa TRA ambapo tofauti na zamani sasa once ukilipa kodi unalipia na registration fee kabisa. Well hawa jamaa huenda walikuwa na sababu nzuri ya kuanza utaratibu huu mpya. Lakini kama ilivyo kwenye mambo mengine ya serikali hii iliyokithiri usanii unaotia kichefuchefu TRA hawakujipanga hata kidogo katika hili. Utaratibu huu unaleta usumbufu usio na lazima kwa wateja. Registration cards zinachelewa sana kutoka na hakuna utaratibu wa kucheck anayechukuwa kama ni kweli mwenyenayo au matokeo yake cards kibao zinapotea. Pia hizo cards zenyewe makosa kibao yaani ili mradi ni usumbufu. Infact ukienda hicho chumba cha registration unaweza kulia kwani ni chaotic kwa kweli.

  Lakini kinachouma zaidi at the end mteja analipa gharama ambayo hapaswi kulipa. Mfano kuna truck yetu mwezi wa pili huu sasa haijapata reg kadi so haiwezi kufanya kazi. Kimahesabu kuna millions hapo hasara. Ingekuwa ndani I know tungechajiwa storage charges na bandari. Iko nje kwa kosa la serikali ninachajiwa mimi mteja. Na hu ni mfano tu ila nawajuwa watu wengine wengi ambao huu utaratibu unawasababishia hasara kubwa sana. Sorry lawyers naomba msaada hakuna namna ya kuishitaki serikali ili japo kidogo wachangie hii hasara tunayopata kwa uzembe wao?
   
Loading...