TRA na kodi ya Mabango ya Indoor

vunjo

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
1,323
2,607
Habari wadau, nimekutana na changamito na hawa TRA sehemu ya biashara yangu kuna stika nimebandika katika vioo vya frame yangu ambayo ipo ndani ya shopping mall hapa jijini. Sasa wakapima na kulazimisha ni sign gharama ni laki nane na ilipwe ndani ya siku saba sasa naomba kuuliza kwa mwenye uelewa je kodi hizi za mabango ya ndani ya jengo ni halali kulipiwa?
 
We ndo utaokoa jahazi la goli walilopangiwa tra. Japokuwa sio haki lakini sasa tutaponaje mzee
 
Mbona Utaratibu unaeleweka Billboards, Banners Zinalipiwa Ilimaradi ziwe sehemu ambayo watu wanaona. Lipa Kodi kwa Maendeleo ya Taifa.
 
Mbona Utaratibu unaeleweka Billboards, Banners Zinalipiwa Ilimaradi ziwe sehemu ambayo watu wanaona. Lipa Kodi kwa Maendeleo ya Taifa.
Kwa iyo ata nikiandika kwamba kuna bucha mita 2 kutoka apa lazima nilipe iyo pesa.
 
Ofisi yangu ipo ndani ya jengo la kibo complex tegeta sasa ofisi kama umeweka stika yoyote au hata logo ya kampuni wanapima na kuchaji ila ofisi na biashara zingine za nje ya jengo hatujasikia kitu kama hiki.Sasa hizi kodi zinabagua maene
 
Mbona Utaratibu unaeleweka Billboards, Banners Zinalipiwa Ilimaradi ziwe sehemu ambayo watu wanaona. Lipa Kodi kwa Maendeleo ya Taifa.
Ati lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa? sio kwa maendeleo ya wapigaji?
 
Kwai haya makusanyo yanongozwa na sheria gani? na utaratibu wa fine untumia sheria gani ?
 
eti kodi ya kujenga taifa!

unaweza lipa halafu uondoe hayo mastika, la sivyo watarudi tena hadi uwanja wa chato ukamilike!
 
Back
Top Bottom