Kusajili VAT (VAT registration)

luck_martine

Member
Jun 6, 2023
10
6
Pengine ulikua hufahamu kwamba kuna umuhimu wa kusajiliwa VAT na kuwa na VRN(VAT Registration number?!

Okay soma hi
Mfanyabiashara mwenye matamanio ya kukua zaid kwenye kibiashara yake anahitaji VRN imsaidie kwenye

• kuomba tenda za kazi zake haswa kwa wale suppliers.
VRN inakuongezea credit unaonekana unauwezo wa kuhimiri na kuifanya hiyo tenda husika ipasavyo
• pia inakuongezea credit wewe mfanyabiashara kupata mikopo kwaajili ya biashara husika kwenye taasisi za kifedha ikiwamo mabenki kwani yatakuamini mojakwamoja kwa kuwa unatambulika na mamlaka ya mapato kama mlipakodi mkubwa NK
Ili kujisajili VAT
• unapaswa kuwa na mauzo ya kuanzia milion200 kwa miezi kumi na mbili Au milion 100 kwa miezi sita
• Kama haujafikisha mauzo hayo na ungehitaji kwaajili ya matumizi flan mfano kuombea tenda ya kazi, inawezekana ilimradi tu ukidhi vigezo vilivyopo

Karibu uwasiliane nasi tukusaidie huduma zote za kihasibu na masuala vote ya KODI(tax)

Call 0612885532,
WhatsApp no 0711697881
Karibu tukuhudumie Kwa gharama nafuu
 
Kwani vat huwa inalipwaje?
Malipo ya VAT hufanyika kila baada ya kufunga hesabu za mwezi za mfanya biashara kutokana na MANUNUZI na MAUZO alioyafanya, na hilo litajulikana kupitia mauzo/manunuzi aliofanya kwa mashine ya risiti (EFD – machine) na kiasi kinacho tozwa ni asilimia 18% ya manunuzi/mauzo yote , manunuzi/mauzo hayo yataingia moja kwa moja kwenye mfumo wa ritani ya TRA, na hivyo mfanyabiashara akifungua tu ataona kiasi anacho takiwa kulipa km rejesho/malipo ya VAT kwa mwezi husika.

Kumbuka kinacholipwa / au kurejeshwa TRA ni tofauti ya kodi kati ya MANUNUZI na MAUZO uliofanya katika mwezi, iwapo manunuzi ya mwezi husika yalikuwa makubwa kuliko mauzo, hapo hutolipa VAT bali hapo mfanyabiashara yeye ndio atakuwa anaida TRA, na ikiwa mauzo yake ni makubwa kuliko manunuzi hapo mfanyabisha atawajibika kulipa kodi baada ya ukokotozi kufanyika kwa kupitia mfumo wa ritani wa TRA.
 
Back
Top Bottom