TRA kuzima mifumo ya Usajili na Kodi kwaajili ya Maboresho kwa saa 43

Scaramanga

JF-Expert Member
Aug 19, 2020
420
574
TRA yatoa taarifa ya maboresho ya mifumo yake kuanzia feb 3 mpaka feb 5 2023.
WhatsApp Image 2023-02-02 at 16.35.36 (1).jpeg


=====

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kufanya maboresho ya Mifumo hiyo kuanzia Februari 3, 2023 Saa 12 kamili Jioni ili kuongeza ufanisi wa Huduma zinazotolewa

Huduma za Usajili wa Namba za Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na Usajili wa Walipa Kodi wa Ongezeko la Thamani (VAT), Uwasilishaji wa Ritani mbalimbali na Usajili wa Malipo ya Kodi mbalimbali hazitapatikana hadi Februari 5, 2023 Saa 7 Mchana

Kutokana na maboresho hayo, tarahe iliyopangwa kuwa mwisho wa uwasilishaji wa Ritani na Kulipa Kodi za Maendeleo ya Ufundi Stadi (SDL) na Kodi za Ajira (PAYE) za Januari 2023 zimesogezwa hadi Februari 10, 2023.

TRA
 
Hahahaa kingereza cha TRA 😁!! hebu tuachane na lugha za watu, swala lina wahusu watanzania vingereza vya nini?
 
Hahahaa kingereza cha TRA 😁!! hebu tuachane na lugha za watu, swala lina wahusu watanzania vingereza vya nini?
Ukiona hivyo wewe sio mlipakodi ,imetumika lugha ya mawasiliano baina ya walipakodi na hapo walipakodi tumeelewa na tumeelewana.
 
Kwa wiki ya pili ya mwezi februari 2023, mamlaka ya mapato tanzania(TRA) inatajia kuanza kutumia mifumo ya moduli za kikodi iliyoboreshwa kwenye lango kuu la huduma kwa walipa kodi(Taxpayer portal) na mifumo ya uwasilishaji wa ritani mbalimbali(Efiling system). Chini ni baadhi ya picha za taarifa rasmi mbalimbali

Watumishi wako
Moms Consulting
0712685025
Kwa ushauri na huduma mbalimbali za kikodi, kiuhasibu usajili wa biashara ya mtu binafsi, ubia na makampuni


IMG_5319.jpg

IMG_5320.jpg

IMG_5321.jpg
 

Attachments

  • IMG_5319.jpg
    IMG_5319.jpg
    317.4 KB · Views: 7
  • IMG_5320.jpg
    IMG_5320.jpg
    398.8 KB · Views: 6
  • IMG_5321.jpg
    IMG_5321.jpg
    404.7 KB · Views: 6
  • IMG_5319.jpg
    IMG_5319.jpg
    128.5 KB · Views: 6
  • IMG_5320.jpg
    IMG_5320.jpg
    155.4 KB · Views: 6
  • IMG_5321.jpg
    IMG_5321.jpg
    164.2 KB · Views: 7
  • IMG_5319.jpg
    IMG_5319.jpg
    128.5 KB · Views: 5
  • IMG_5320.jpg
    IMG_5320.jpg
    155.4 KB · Views: 6
  • IMG_5321.jpg
    IMG_5321.jpg
    164.2 KB · Views: 6
Back
Top Bottom