TRA; kulazimisha watu kwenda kuhakiki wa namba ya mlipa kodi (TIN) ni Usumbufu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,545
22,050
Kuna hili tangazo la TRA, la kuwataka watu wote wenye tin Namba kwenda kuhakiki taarifa zao ili wabadili mfumo mimi binafsi naona ni usumbufu uliotukuka; kwani wao hawana kumbukumbu za wateja wao hadi mwenye tin aende pale? Na kwanini waweke deadline? Wameweka deadline ya 30 January 2017 Kwa mkoa Wa dar es salam! Na wanasema hawataruhu mtu kuhakiki baada ya mda huo.

Swali; Hawatambui kuna watu walikuwa wamesafiri nje ya nchi hadi waweke ukomo?
Kwanini was I update automatically mpaka wamsubiri Mteja aende kwani hawajui?
Kwanini kwenye kudai madeni ya road licence na vipuri Vya magari wanadai automatically pasipo kumuuliza mlengwa?

TRA KWAKWELI KWA HILI MIMI MMENIKERA SANA MAANA NIMESAFIRI TOKA NJE YA NCHI KWA AJILI YA HUU USUMBUFU WENU WA KIZEMBE JARIBUNI KUWA WABUNIFU.
Makosa ya barabarani mnakamata watu automatically lakini hapa mmejifanya hamwezi hadi kusumbua watu walio busy na kazi zao.
Sijapenda huu usumbufu
 
Mie nimeenda hakiki leo huku moshi, kwa kweli hili zoezi ni kero na kupotezea watu mda wa kufanya mambo mengine bora wangefikiri utaratibu mwingine kwani huu wa sasa una mlolongo mrefu
 
Kwakweli hao Tra wasumbufu sana; na nasikia hawataongeza mda tena; waliopuuzia watapelekwa mahakamani kushitakiwa! Hii inch inakera sana, makosa wayafanye wao halafu adhabu apewe mwananchi..
 
TRA huu ni ujinga wa hali ya juu. Miaka iliyopita tulikuwa tunajiandikisha mtandaoni unapata TIN kesho yake unaendea cheti TRA sasa na maendeleo eti unaenda kujipanga
Sijui waliwaza nn
 
Kwanini mnasubiri kujazana kwenye deadline ? Kumbuka zoezi la uhakiki wa tin lilianza tangu Mwezi August mwaka jana miezi Sita sasa imagine bado sioni sababu ya kuilaumu Tra ktk hili Kwa Kweli
 
Kwanini mnasubiri kujazana kwenye deadline ? Kumbuka zoezi la uhakiki wa tin lilianza tangu Mwezi August mwaka jana miezi Sita sasa imagine bado sioni sababu ya kuilaumu Tra ktk hili Kwa Kweli
Hawajui kwamba watu wnasafir? Kwanini wasibuni njia Mpya zaid kuriko hii ya kupotezeana mda watu wapo busy na mambo yao! Walishindwa hata kutumia simu yaani mtu unapiga call center Anasikilizwa?
 
Kwakweli hao Tra wasumbufu sana; na nasikia hawataongeza mda tena; waliopuuzia watapelekwa mahakamani kushitakiwa! Hii inch inakera sana, makosa wayafanye wao halafu adhabu apewe mwananchi..
Mahakamani kwa kosa gani na sheria gani?
Wakusanye kodi waache siasa...na ujinga pia.
 
Kwanini mnasubiri kujazana kwenye deadline ? Kumbuka zoezi la uhakiki wa tin lilianza tangu Mwezi August mwaka jana miezi Sita sasa imagine bado sioni sababu ya kuilaumu Tra ktk hili Kwa Kweli
Na hakuna siku ambayo watu hawakurudishwa kwa vile muda umeisha.
wenye tin ni zaid ya 1.5m dar pekee hata miezi sita wasingeisha.
waache upuuzi...watu waruhusiwe ku verify muda wowote kabla ya kuhitaji huduma.
mkifanya ubishi mtakosa kodi
 
Huku mza mvua zikinyesha singida mkongo wa taifa unazima, munaambiwa mje kesho, wakati huohuo maduka yamepigwa makufuli na jiji, ujinga huu ipo siku utafika mwisho.
 
Kwanini mnasubiri kujazana kwenye deadline ? Kumbuka zoezi la uhakiki wa tin lilianza tangu Mwezi August mwaka jana miezi Sita sasa imagine bado sioni sababu ya kuilaumu Tra ktk hili Kwa Kweli

Tatizo TRA hawana watu wabunifu. wanafanya kazi kwa mazoea. Wangetumia akili kidogo wangepanga utaratibu mzuri ambao usingeleta usumbufu kabisa.
 
Kwa nini na nyie mnasubiri mpk deadline ifike ndio mkajazane kwenye foleni?wkt cku za nyuma kulikua hamna watu kabisa?hapo wkt mwingine tusiwalaumu,mimi nilienda mwanzoni kulikua hakuna watu kabisa.ndio hivo wabongo tulivyo.
 
Unafikili watu wote wapo dar? Hutambui kuna kusafiri au kuhama? Huo usumbufu Wa kurudi ktk kituo huoni ni kero?
 
Back
Top Bottom