YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,900
- 52,051
Kufuta Usajili wa Vyombo vya Moto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwajulisha watu wote wanao miliki vyombo vya moto (magari, matrekta, pikipiki na matela) ambavyo havipo tena barabarani au haviwezi tena kurudi barabarani kwa sababu ya uchakavu, kuwasilisha maombi yao TRA ya kuvifuta kwenye usajili.
Kwa mujibu wa Kanuni Namba 177 ya mwaka 2001 ya Sheria ya Usalama Barabarani ya Mwaka 1973 kinamtaka mwenye chombo cha moto ambacho hakifai kuwa barabarani kuomba kufutwa kwenye usajili wa magari
Mwongozo:
1. Mmiliki atatakiwa kwenda Ofisi ya Usalama Barabarani (Polisi) kwa ukaguzi wa chombo cha moto na kupata cheti cha ruhusa ya kufuta usajili
2. Mmiliki atatakiwa kuwasilisha barua ya maombi ya kufuta usajili ofisi ya TRA iliyokaribu ikiambatanishwa na kadi halisi ya gari na cheti kutoka ofisi ya usalama barabarani
3. Baada ya TRA kuridhika na taarifa zilizowasilishwa maombi yatakubaliwa na chombo husika kitafutwa kwenye usajili na mmiliki atapewa cheti kuthibitisha kufutwa kwa chombo husika
Lengo:
Lengo la tangazo hili ni kuwahimiza wenye vyombo vya moto ambavyo haviko barabarani kuwasilisha maombi ya kufuta usajili haraka ili Serikali iwe na kumbukumbu sahihi ya idadi ya vyombo vya moto vinavyotembea barabarani kwa ajili ya kurahisisha mipango yake ya maendeleo ya taifa