Mh naona hizo gharama inategemeana upo mkoa gani na unataka piki piki ya matumizi gani! Ktk hali isiyo ya kawaida Tanga walianza na sh 10,000/= kadi mpya(biashara) na tra wanasingizia kuwa ni mfumo huo unatoa kadi ya commercial, ukitaka kubadili kuwa private unalipa sh 5000/= police kisha unaenda kwa vehicle unampa kima cha chini 5000/= ,eti ili akague na kukuandikia taarifa ya kubadili kadi toka commercial kwenda private, baada ya hapo unarudi tra na kadi ya commercial unalipa tena sh 10000/= unapewa kadi ya private. utaratibu huo umefanyika hata kwa kadi ambazo tayari zilikuwa private ukiwauliza wanakwambia mfumo hautoi private unatoa kwanza commercial na kisha ndio ubadili kuwa private! Je wahusika wa tra mikoa mingine mnasemaje huo ndio utaratibu? yani kulipa 20,000/= tra na kisha 10000/= polisi? Kwa nini mnawakamua walalahoi kisa ni wanyonge? nb hapo madeni hayapo ni gharama za kadi tu na bado malipo ya plate namba