TRA: Ku transfer umiliki, taratibu zikoje?

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
3,023
Wakuu, habari za mida hii. Nitashukuru kwa mawazo.

Nataraji kununua gari used ya biashara, Coaster, lakini mmiliki wake wa sasa hana karatasi yeyote kuonyesha alikuwa akilipa kodi ya mapato toka 2007 ambayo na hakika ni lazima uonyeshe kuwa uko up to date na kodi zao wakati unapotaka ku renew leseni ya biashara au hata usajili wenyewe wa gari, yani ku transfer kwenda kwenye jina langu. Yeye ana TIN namba yake, mimi sina, na sina deni na TRA.

Sasa nikienda TRA ku transfer jina huo mzigo wa kodi zake bado utaniangukia mimi? Nifanyeje.
 
hata mimi nasubiri mawazo,naona wengine hawajaamka si unajua blue Monday! au foleni
 
MADA ZA KUELIMISHA WATU HATUCHANGII.....ULIZA MASWALA YA NGUVU ZA KIUME.....UMEFUMANIWA.....KUIBIWA KURA......BAR/CLUB NZURI IPO WAPI UTAPATA MAJIBU LUKUKI....lakini...MADA YENYE FAIDA KWA UMMA .....UTABAKI KUCHANGIA MWENEWE....SISI NDO GREAT THINKERS BWANA....!
 
Kutransfer kitu chochote kile kuna sheria zake. Kwanza inategemea the status of the current registration. Kama gari iliingia kwa ajili ya kufanya kazi za NGO and the like ni dhahili ilikuwa tax exempted. Anything like kubadili status will require new user to pay the exempted taxes kabla hajalibadili gari hilo. Kama gari lilikuwa linadaiwa kodi yoyote ile ni lazime iwe cleared kwanza kabla ya kutransfer ambapo pia kutakuwa na other costs associated with that.

Kwa hiyo kabla hujanunua gari hakikisha umefahamu historia yake yote vinginevyo ulinunue liwe lako lakini jina na kila kitu viendelee kuwa vya aliyekuuzia kitu ambacho ni risk kwa muuzaji na mnunuzi. Kwa muuzaji kama gari likijihusisha katika uhalifu na likakamatwa wanakufuata wewe. Kwa mnunuzi ni kwamba jamaa anaweza kukugeuka wakati wowote kuwa hajakuuzia na analitaka gari lake. Watu wengi sana Tanzania wapo hapa kwa kukwepa gharama ila wanasahau risk nyuma ya hii option

Ni bora kufuata sheria zaidi. Chukua kadi ya gari ongozana na muuzaji(Current owner)TRA watakusaidia kujua kila kitu, nina sema kadi siyo namba maana ukienda na kadi watajua kuwa kuna ownership relationship na hivyo kukusaidia.
 
MADA ZA KUELIMISHA WATU HATUCHANGII.....ULIZA MASWALA YA NGUVU ZA KIUME.....UMEFUMANIWA.....KUIBIWA KURA......BAR/CLUB NZURI IPO WAPI UTAPATA MAJIBU LUKUKI....lakini...MADA YENYE FAIDA KWA UMMA .....UTABAKI KUCHANGIA MWENEWE....SISI NDO GREAT THINKERS BWANA....!
ndio nini sasa Mkuu? Badala ya kuponda ungetoa unaloelewa wewe kuhusiana na mada husika
 
..................Kwa hiyo kabla hujanunua gari hakikisha umefahamu historia yake
Mkuu, ahsante sana. Kwa hiyo mimi ndio nitabebeshwa mzigo wa deni la Muuzaji na TRA.

Ngoja nikawasikilizie TRA kabla sijanunua, lakini gari ni nzima sana ukilinganisha na bei yake.
 
Watu wengi wanatumia magari yenye kadi za watu wengine,hii inatokana na usumbufu wa TRA yani ukienda pale utaambiwa mkataba wenye stempu,kitambulisho cha muuzaji,ole wako uweke bei halisi ulionunulia utaambiwa transfer fee hukuitegemea.
 
Kwa kadri ninavyoelewa kama mtu anadaiwa kodi,( kutoka na maelezo yako nahisi ni kodi ya mapato) haiwezekani kodi anayodaiwa mtu mmoja haiwezi kudaiwa mtu mwingine SIJAWAHI KUSIKIA KESI AMBAYO MDAIWA KODI NA WATEJA WAKE WAKAJUMUISHWA KWENYE KULIPA KODI ALIYOKWEPA MUUZAJI. iwapo kama gari haijalipiwa USHURU ilipoingia nchini basi inaweza kukamatwa muda wowote na TRA au wakala wake.
ukitaka kufanya transfer ni kwamba unaenda TRA unajaza fomu za transfer na taratibu zote watakufahamisha, lakini uwe mvumilivu kuhusu uchelewesha jambo muhimu ni kujua tu kama kweli huyo mtu anamiliki hilo gari kihalali kuhusu kodi ya mapato ni yeye na TRA. Kuhusu ni namba ambayo inamtambulisha mlipa kodi kwahiyo utakapoanza biashara lazima uwe nayo ( unaomba TRA hii haina usumbufu)
 
Back
Top Bottom