TRA excels in revenue collection, says JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA excels in revenue collection, says JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 13, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  TRA excels in revenue collection, says JK
  JAPHET SANGA in Ileje
  Daily News; Sunday,October 12, 2008 @20:03

  President Jakaya Kikwete has announced that Tanzania Revenue Authority (TRA) last month broke its monthly revenue collection record after collecting 427bn/-.

  Speaking after receiving Ileje District development report, President Kikwete said the amount had never been collected by the authority since its inception in 1996.In July and August this year, TRA collected only 268bn/- in each month, creating fear that the budget could be affected.

  According to the authority's recent report, TRA has never exceeded 327bn/- in its monthly collection.President Kikwete revealed the record after the District Commissioner, Ms Esther Wakati, said that Kiwira Coal Mine Company had not been paying tax to the District Council.

  He told the DC to take the necessary actions against any tax defaulters, as they had the mandate to do so including taking culprits to court.The president said that TRA had managed to collect such amount because it had been strict and aggressive in collecting taxes, urging the council to borrow a leaf from the authority.

  On his part, the District Executive Director, Gladis Dyamvunye, said that the firm owes the council arrears totalling 7.5m/- for 2007 and 2008 and that they had issued a notice of suing the company.Meanwhile, Kyela residents have been told to desist from 'smuggling' medicine to neighbouring Malawi, therefore, causing drugs shortage in the border district.

  In his third day tour of Mbeya Region on Saturday, President Kikwete told a rally at Kimbalu that instead of 'smuggling' the drugs to Malawi, they should ask their kith and kin to come for treatment to Kyela.

  The president was reacting to reports that there was a shortage of medical supplies in hospitals, forcing patients to seek treatment in Rungwe District -- about 50 kilometres away.However, he told another rally at Mwakangale ground here that measures had already been taken to avert further shortage by deploying more serious medical personnel.

  The president said after a successful campaign in construction of primary and secondary schools, efforts were now being directed at building dispensaries and health centres."Our intention now is to ensure that we have a dispensary in every village and a health centre in every ward so that people do not walk more than five kilometers for medical services," he said.

  Kyela district has 29 dispensaries, 24 of which are government run, four owned by religious organisations and one by a civil organisation -- KCP.The district has two hospitals, one owned by a religious organisation at Matema and a government hospital. It has one health centre at Ipinda.

  The president also called on people to abstain from reckless sex as the HIV infection rate was high in the region. Mbeya ranks second to Iringa with 17 per cent infection rate.In most cases, he said, people contracted HIV/Aids out of volition as they had the luxury to fix a date, time and place to meet. "But why go without protective gear (condoms)?" he asked.

  He said there was no emergency in courting as people had ample luxury to decide on a venue, date and time, therefore, reminded them to carry condoms on such missions to avoid the pandemic.

  On malaria control in the district, President Kikwete said Kyela was one of the 26 districts in the country that would benefit from residual spraying and distribution of insecticide treated mosquito nets to children less than five years old.
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Bubu,

  Kila mwezi mapato ya Serikali kupitia kodi yanaongezeka na ni mara chache sana kushuka. Kitu cha kujiuliza, kwa mapatao kuongezeka WaTz tumepata nafuu gani? Mbona kila siku ikipita heri ya jana? Mapato yakiongezeka, mafisadi nao matumbo yao yanaongezeka.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa, ongezeko la makusanyomya kodi yanatakwia yaonekane kupitia mabadiliko kwa maisha ya wananchi, si rekodi za TRA
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kiwira coal mine wanalipa tax kupitia Ileje na sio Kyela kwanini?

  Kwa ufahamu wangu Kiwira coal mine iko Kyela na sio Ileje.

  Kama hawalipi kodi si wanyang'anywe leseni? Wanalipa hata akina mama Ntilie ndio iwe kampuni ya mafisadi?
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Halafu hawa TRA huwa wananiudhi mimi.
  Sijui labda ni umbumbu wangu au vipi,,,,, ila wanakera, wanakera sana tu! AAgh
  Labda tujadili haya:-
  Mtanzania anayefungua kibanda tu cha kuuza tumaandazi twa watoto,,, kabla hajafungua lazima alipe kodi! jamani kodi hata sijaua biashara italipa ama vipi? Biashara ya mkopo pale pride? Lipa kodi kwanza,,, tax clearance!!! ptuuuuu,,, inanuka hiyo. Aibu hawaoni hawa jamaa hata kidogo,,,, aagh
  Upande wa pili anakuja jamaa na mahela yake,,,, nywele zimekaa upande,, sijui mzungu,,, sijui mhindi,,,,anapewa TAX HOLIDAY YA MIAKA MITANO!!!!! five years my friend!!!! UUUUUwi. Eeee habari ndo hiyo bwana. wakimaliza 5years wanabadilisha jina kwenda kwa mtoto, mke au hata mjomba au jina lake la utotoni,,, makampuni yote tunayajua na hawa TRA wanaangalia tu! aah!
  Hapa ni sawa na mtoto anataka kwenda shule unamwambia kabla hajaenda shule akupe kitu kidogo kwanza. Kwa nini TRA WASIWAPE WAZAWA WA TANZANIA HATA MWAKA TU WATU WASTUDY BIASHARA KAMA INAGENERATE THEN WALIPE KODI BAADA YA MWAKA TU.
  Haya kuna biashara niliona sehemu fulani hapa Tanzania,,,,TRA wanakamata wamama wanaoenda kununua vibidhaa border ambavyo havina hata faida ya shs 10,000. at the same time kuna mfanyabiashara anapitisha container la 40 feet bila kulipia ushuru,,,, oooh my God! na wanajua,, wanamwona ila huyu aliyeenda kununua vijisabuni ili tu ajepushe na balaa anakamatwa na kupelekwa TRA eti wamekamata magendo! Huyu dada yako amesema umalaya basi atafuta tu mia twa mafuta ya taa unamkamata na mara ingine wanalazimishwa hongo ya ngono! Kweli? Halafu mnasema tutafika! Kwa namna hiii? TRA wamelaaniawa na hata maandiko yaliwalaani watoza ushuru!!!!!!!!!!!
  Sisemi tusilipe kodi, la hasha, tuwe utaratibu wa kumsaidia Mtanzania ajikomboe na shuruba na ukata unaotukabili.

  Narudia sijui kama ni umbumbu wangu ama vipi ,,,,, ila INAKERA MNO!!!!!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kabisa. Fisadi Mkapa aliongeza sana mapato ya kodo wakati wa awamu yake na alikuwa kilipigia debe sana hili. Lakini mafanikio yake ya ongezeko hilo mimi huwa nayafananisha na Baba mtaani anayetamba pale mtaani kwamba yeye ndiyo mwenye mshahara mkubwa sana kuliko mababa wengine wote pale mtaaani, lakni watoto hawanufaiki na mapato makubwa ya baba yao maana mshahara wote unaishia kwenye nyumba ndogo, nyama choma, pombe n.k. na watoto wa huyo Mzee wana utapia mlo.

  Hivyo basi pamoja na ongezeko kubwa la mapato ya TRA Watanzania hawajanufaika na lolote bado hospitali zetu hazina dawa, hazina vitanda hazina vifaa muhimu, bado mashule yetu hayana madarasa yenye hadhi hayana madawati na vifaa vingine muhimu mashuleni, bado wataalamu wetu mbali mbali wanalipwa ujira mdogo ambao hauendani na hali halisi ya maisha pamoja na kulalamika miaka nenda miaka rudi, bado usafiri wetu wa barabara, reli na hata majini ni wa kusikitisha na kutishia afya na maisha ya Watanzania. Kwa kifupi maongezeko hayo makubwa hayakuleta ahueni yoyote kwa Watanzania.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  JK amshukia mwekezaji wa mgodi Kiwira

  2008-10-13 10:24:56
  Na Thobias Mwanakatwe, Kyela

  Rais Jakaya Kikwete, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba Hussein Mashimba, kumbana mwekezaji wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira, ili ahakikishe anawalipa afanyakazi wa mgodi huo mishahara ya miezi miwili wanayodai.

  Rais Kikwete alitoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela kuomba msaada wa serikali wa kumbana mwekezaji wa mgodi huo ambao pia Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amekuwa akihusishwa kuwa mmoja wa wamiliki wake, ili aweze kuwalipa mishahara wafanyakazi ambao hivi sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha. Mwingine anayehusishwa na mgodi huo ni aliyekuwa waziri katika serikali ya Mkapa, Daniel Yona.

  Rais Kikwete alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa, suala hilo lipo chini ya uwezo wake na kumtaka afanye kila jitihada za kumbana mwekezaji wa mgodi huo ambaye ni kampuni ya Kiwira Tanpower aweze kuwalipa wafanyakazi mishahara iliyobaki.

  ``Kama umeweza kumbana mwekezaji akalipa mishahara ya miezi mitatu, sasa unashindwaje kumbana tena amalizie mishahara ya miezi miwili iliyobaki. Hakikisha unambana tena awalipe, hili lipo chini ya uwezo wako,`` Rais Kikwete alisisitiza.

  Inadaiwa kwamba, mbali na wafanyakazi kutolipwa mishahara yao, kumekuwepo na hujuma ambazo zimekuwa zikifanyika kwa kuuza kinyemela mali za mgodi huo.

  Wafanyakazi waliotoa maombi hayo ni wale waliopunguzwa kazi na na serikali mwaka 2005, ambao wanaidai serikali zaidi ya Shilingi bilioni 47.

  Wafanyakazi hao walidai kusikitishwa na hali hiyo, kwani hata kamati ya rais aliyoiunda kuchunguza sekta ya madini na mikataba, chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, ilipita katika mgodi huo na kupokea kilio cha wafanyakazi hao, lakini bado hawajalipwa fedha zao.

  Wafanyakazi hao wanaililia serikali kwamba hawajalipwa mafao na mishahara yao ya miezi kadhaa waliyokuwa wakidai tangu mgodi huo ulipokuwa chini ya serikali na kuwafanya washindwe kuondoka kwenye nyumba za mmiliki mpya aliyekabidhiwa mgodi huo.

  ``Baada ya suala letu kushindikana kwa muda mrefu, sasa tunataka kutumia ujio wa rais kuwasilisha kilio chetu kwake kwani ndiye pekee tunadhani anaweza kutusaidia,``alisema mmoja wa wafanyakazi hao zaidi ya 500.

  Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO), Thomas Cheyo, alisema hali za wafanyakazi hao waliopunguzwa kazi tangu mwaka 2005 ni mbaya na wengi hawana chakula, hivyo ujio wa Rais Kikwete ni faraja kwao.

  ``Tumepata taarifa kuwa Rais Kikwete anakuja Mbeya, tunaomba atembelee hapa mgodini ili tuweze kumfikishia kilio chetu,`` alisema.

  SOURCE: Nipashe
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Hiyo article hapo juu inaashiria umiliki wa Kiwira hautarudishwa kwa Watanzania pamoja na fisadi Mkapa kuukupua mgodi huo alipokuwa Rais na kuamua bei yake ni shilingi milioni 700 pamoja na kuwa una thamani ya shilingi bilioni 4, mapaka sasa amelipa shilingi 70 millioni tu, kisha kuwashinikiza wazungu wa NET GROUP aliowaleta kuiendesha TANESCO kusaini mkataba wa shilingi bilioni 326 ambapo fisadi Mkapa analipwa shilingi 146 milliono kwa siku na TANESCO.
   
Loading...