TRA Dodoma na madalali wenu muache ubabaishaji wenu

TRA Dodoma na madalali wenu muache ubabaishaji wenu

Mwanakili90

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,568
Reaction score
246
Naamini wabunge wapo dodoma lakini hawaelewi hili swala la wakusanya kodi wao wanachokifanya,ukweli ni kwamba watu hawajakataa kupokea mashine za EFD kama serikali ilivyoelekeza,kinyume chake wamekuwa wanawatumia madalali wa mahakama kufunga milango ya wafanya biashara wa dodoma mjini kwa kuweka kufuli jipya kwenye milango ya wafanya biashara,na ili waje kufungua inakubidi ukanunue mashine ya laki nane na uwape hao madalali kiasi cha elfu hamsini kama gharama za kufuli.

Je wabunge waliopo dodoma wanaelewa hujuma hii? Serekali na Chama tawala wanaelewa hujuma hizi juu ya serikali yao?Kodi inautaratibu wake ila siyo kwa staili hii wanayoenda nayo TRA Dodoma.

Wadau kama kuna mkoa mwingine wanatekeleza haya tujuzane ili wahusika wajue wazi na wachukue hatua stahili kwa mradi huu wa kitatanishi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom