TRA demands 3bn/- in taxes from FastJet

TRA demands 3bn/- in taxes from FastJet

1. mwandishi wa habari kaandika tra lakini ukisoma mchanganuo utaona kuna Taa parking and landing charges.
2. ukisoma utaona element kubwa ni departure tax a.k.a air port tax. kila abiria anakatwa 10,000 hii ni hela ya serikali.

3. wafanyakazi wa kigeni ambao wameajiriwa kwenye makampuni wanatakiwa kulipa kodi na nssf. Ambao hawalipi kodi ni kwenye embassy, UN na makundi yake. Fastjet ni private na wanatakiwa kulipia Paye.

4. ushindani ni kitu muhimu kwenye biashara kwa ajili unasaidia kushusha bei na kupata huduma bora, lakini isiwe kisingizio cha kukaa na mapato ya serikali

Mkuu hata kama, hizo pesa zinazodaiwa kwa muda waliofanya biashara hawa jamaa hicho kitu hakiwezekani, kama hizo figure zipo sawa basi nchi hii inakusanya kodi kubwa sana, sioni ni kwanini tuwe na madeni au kuomba omba toka nje, mashirika kama Precision,540, Air Tanzania, Coastal Travel (haya ni baadhi ya mashirika makongwe ya usafiri wa Anga nchini) yatakua yanalipa hivyo kwa muda wote wa kuwepo kwenye biashara mbona tungekua na mihela ya kutosha pale BOT? hapo hujagusa TRL, Makampuni ya simu, Migodi, haa , hapana bwana, waje na single nyingine, hii tayari imeisha chuja hata kabla haijaingia sokoni!
 
Sasa jamani hawa TRA ni watu waa ajabu sana, Fast Jet wameanza December 2012, wanawadai PAYE ya 2009, wao hawakusanya kwa fly 540 si ni ujinga wao?
 
Sie watanzania watu wa ajabu kwa hiyo mlitaka wasilipe kodi? Mimi tatizo langu ni kwanini TRA waliwaacha fly540 muda mrefu bila kulipa kodi zote hizo wanefunga virago na kuondoka kabisa? Halafu PAYE si inatakiwa kulipwa ndani ya siku 7 baada ya makato? Unaweza kukuta hata pension hawapeleki. Tusifumbwe macho na vitu vidogo. Kuna watu waliwahi kujifanya wafadhili wa vilabu vyetu halafu wakawa hawalipi kodi! Kila mtu alipe kodi tunapambana na wa migodi ili walipe kodi tusiongeze wengine.
 
Wenye nchi - nilimaanisha wafanya hujuma; kuhusu namna ya kuokoa fast Jet kutoka kwenye hii hujuma, ni ngumu kwa kweli, pengine (depending na jinsi gani kesi ita transpire), fast jet wafungue kesi commercial court, ingawa itachukua muda mrefu sana kabla ya kesi kufanyiwa hukumu/haki kutendeka na by that time, itakuwa too late kwa shirika hili kusimama tena kwani wanaolindwa na wenye nchi watajipanga vyema zaidi kukabiliana na usindani;

Ninafikiri kinachofanyika hapa ni mkakati wa kibiashara (au TAA na TRA) wanajaribu kutatua tatizo walilozembea huko nyuma kabla mambo hayajaaribika. Ukiangalia madeni haya idadi kubwa ni malimbikizo ya Fly540 na siyo ya FastJet.

Kumbuka FastJet ilinunua Fly540 na kuanza huduma hapa nchini mwezi November 2012. Hata hivyo FastJet wameshindwa kupata ruhusa ya kufanya biashara Kenya (ambako mwenye Fly540 yuko) na wakati huohuo aliyeuza Fly540 anadai hawajamlipa pesa zote walizokubaliana. Hata hivyo FastJet wanadai ameshalipwa na inavyoonekana wakati wakijadili na kukubaliana mauziano yawezekana Fly540 hawakuwaeleza kuhusu madeni haya.

Bahati mbaya watu wanahusisha na hujuma bila kuwa na details. Haya marumbano Kati ya FadtJet na Fly540 yalitangazwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Sisi tungepaswa kuwawajibisha TAA na TRA kwa nini hawakuhakikisha madeni hayo yanalipwa walipoona Fly540 inauzwa. Hata Kama ilisemekana ni Fly540 inaendelea kwa Jina jipya la kibiashara la FastJet kwani walikuwa na details za mauziano haya.
 
Ba (british airway) wanaondoka , tatizo ni nini? Au tra
 
TRA wanaweza kuwaambia watanzania Prescion Air wamelipa kodi kiasi gani? Au Vodacom, CocaCola, Bakhresa, Barrick, mahoteli ya kitalii kule Serengeti wamelipa kodi kiasi gani? Kama kweli TRA wako makini kwenye ukusaji kodi makini watupe mchangunuo wa ulipaji wa hayo makampuni kwa miaka 5 iliyopita.

Tanzania tunasemehe kodi kwa makampuni ambayo yanawanufaisha wachache (migodi) lakini tunaleta mizengwe kwenye mambo yenye manufaa kwa wengi. Fastjet imefanya usafiri wa anga uwe affordable wa watu wa kipato cha kawaida, tofauti na ilivyokuwa huko awali ambao wapanda ndege walikuwa ni hao hao TRA na walanguzi wenzao.

Hii nchi hatuna vipaumbele kabisa. Huyu bwana Fastjet anaweza kuondoa kampuni yake na kuepeleka Kenya na kutoa ajira huko huko. Na kwa hakika Kenya watampokea na red-carpet.

Duh! Ungekuwa karibu ningekubeba mgongoni.... ujumbe wako nimeupnda sana. TRA wasituletee zao, kodi wanayodaiwa fastjet ni yetu walalahoi kama vipi wawache tu. Hatutakuwa na Hasara!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
TRA nao ni janga la kitaifa,walikuwa wapi kukusanya kodi kwa FLY540 awali?kazi yao nini sasa?wanakomalia viduka vidogo vidogo wanawaacha wenye BLNS of money,pambaf sana.
 
Sina shaka ni hujuma ya kibiashara. Hii mizengwe tuko nayo kwenye sekta nyingi tu ila sasa ufike wakati na sisi wanancnhi tuseme ENOUGH!

Ubora wa huduma haufanani na gharama PA.Kama vipi tutaisusia Precision Air tu na badala yake tutapanda usafiri binafsi/mabasi na kwenda kupata huduma za mashirika mengine kwingineko.
 
Hujuma Zimeanza, nyukaneni viongozi muuane mzikane wenyewe. Mtakufa mkiwa macho wazi wana kulaaniwa nyinyi manyang'au viongozi fake wa nchi hii. Ndiyo maana laana inawatafuna kwa kula jasho la mnyonge wa Tanzania(mwananchi)
 
Ninafikiri kinachofanyika hapa ni mkakati wa kibiashara (au TAA na TRA) wanajaribu kutatua tatizo walilozembea huko nyuma kabla mambo hayajaaribika. Ukiangalia madeni haya idadi kubwa ni malimbikizo ya Fly540 na siyo ya FastJet.

Kumbuka FastJet ilinunua Fly540 na kuanza huduma hapa nchini mwezi November 2012. Hata hivyo FastJet wameshindwa kupata ruhusa ya kufanya biashara Kenya (ambako mwenye Fly540 yuko) na wakati huohuo aliyeuza Fly540 anadai hawajamlipa pesa zote walizokubaliana. Hata hivyo FastJet wanadai ameshalipwa na inavyoonekana wakati wakijadili na kukubaliana mauziano yawezekana Fly540 hawakuwaeleza kuhusu madeni haya.

Bahati mbaya watu wanahusisha na hujuma bila kuwa na details. Haya marumbano Kati ya FadtJet na Fly540 yalitangazwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Sisi tungepaswa kuwawajibisha TAA na TRA kwa nini hawakuhakikisha madeni hayo yanalipwa walipoona Fly540 inauzwa. Hata Kama ilisemekana ni Fly540 inaendelea kwa Jina jipya la kibiashara la FastJet kwani walikuwa na details za mauziano haya.
Mkuu Getstart, plus or minus huoni monopoly hegemony ikilindwa hapo? Fly540 walifanya nini ktk kipindi hicho hata accumulate tax arrears/liability za over 2bn?

Tunataka mahesabu yaliyokaguliwa ya mashirika yote ya ndege tuone kama ukokotoaji wetu na wa TAA/TRA kama unakubaliana.
 
Serikali inayojali ingeliingilia suala hili ili usafiri wa walalahoi ulindwa kwa misingi ya sheria. lakini hapo PA naituhumu haki ya nani, sio bure!
 
Mkuu Getstart, plus or minus huoni monopoly hegemony ikilindwa hapo? Fly540 walifanya nini ktk kipindi hicho hata accumulate tax arrears/liability za over 2bn?

Tunataka mahesabu yaliyokaguliwa ya mashirika yote ya ndege tuone kama ukokotoaji wetu na wa TAA/TRA kama unakubaliana.

Ronal Reagan ukiangalia utendaji wa vyombo vyetu na hasa TRA, hawakusanyi mapato Kama inavyotakiwa. Wanatengeneza madeni Mara zote. Nina hakika hata precisionAir na mashirika mengine wanadaiwa mapato ya TRA. UKienda ATCL utashangaa. Kwahiyo siyo suala la kutengeneza monopoly Bali ni uzembe uliokithjiri. Unafikiri kwa nini nchi inashindwa kujitegemea, hii ni moja ya sababu.
 
mfano departure tax ni mil 951,562,012, na kila abiria ni 10,000. kwa hiyo kama ukisema one way basi hawa ni abiria 95,1562.012 na kama ni return basi ni abiria 45,000. kwa hiyo siyo figure. kila mtu alipe kodi na sio majungu
 
Hata hivyo FastJet wanadai ameshalipwa na inavyoonekana wakati wakijadili na kukubaliana mauziano yawezekana Fly540 hawakuwaeleza kuhusu madeni haya.

Haiwezekani kutojua kuhusu haya madeni. Acqusition ya makampuni makubwa kama hayo due diligence is a must. So lazima ionekane
 
Ba (british airway) wanaondoka , tatizo ni nini? Au tra

Wanashindwa kutengeneza faida, Dar hailipi kwa sababu ya Emirates ... .... ... via Dubai unalipa i.e £400 return wakati BA unalipa i.e. £550 though its a direct flight, halafu Emirates ndege zao zote za kisasa na wanaongeza kununua ndege kama utitili ... .... ...
 
Back
Top Bottom