TENGEFU
Senior Member
- Jan 25, 2017
- 138
- 206
Kwa utafiti wa siku nne niliofanya TRA Arusha hususani idara ya Dept Management ambao pia nimehusisha baadhi ya wateja waathirika wenzangu nime note deliberate sabotage ya mapato ya serikali inayofanywa na wafanyakazi haswa kwenye issue ya TAX clearence.
Katika utafiti wangu nimebaini yafuatayo:
Tunawapowahoji hawa wafanyakazi wa TRA kwa nini huduma zimekuwa almost grounded wanasema tatizo mtandao uko chini; hii ni sabotage. Ni almost wiki tatu TRA Arusha wanasingia mtandao kuwa chini kama chanzo cha huduma mbovu. Ina maana hawa watu hawana kitengo cha wataalamu wa komputa na kusababisha ukusanyaji wa kodi kuwa mbovu kiasi hicho; hii ni hujuma ya wazi kama wiki tatu zote wimbo unaoimbwa ni wa mtandao wa mfumo wa TRA Arusha uko chini na hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa .
Hasara wanayosababisha kwa serikali :
Ushauri wa bure kwa TRA na serikali:
Katika utafiti wangu nimebaini yafuatayo:
- Kati ya wateja 200 wanaongia kutaka kufanyiwa tax clearence ni wateja kati ya 30-40 tu wanaofanikiwa kuhudumiwa;
- Wateja wengi wanaotaka kufanyiwa tax clearence wameshafika TRA Zaidi ya mara 2 bila mafanikio
- Wateja wengi (99%) wanasubiri kuanzia masaa 3 -7 kupata huduma wakiwa congested ndani ya TRA ambayo ni hatari sana kwa kipindi hiki cha covid-19
- Mfanyakazi wa TRA Arusha kwenye kitengo cha Debt management kwa wastani anahudumia wateja 3 tu kwa siku na kisa anarudi nyumbani na mwisho wa mwezi anataka alipwe mshahara wake
- Majority ya wafanyakazi hawako serious na kazi kwani muda mwingi wanaongea na simu mara na sometime kuwaacha wateja na kutoka nje kwa muda usiojulikana huku akiacha foleni ndefu ikimsubiri.
- Cha kushangaza Wafanyakazi wa TRA Arusha walioko kwenye dept management ni wengi kuliko wateja lakini efficiency ya kazi yao ni almost zero (0)
- Kwa dharau kubwa wakati watu wakiwa kwenye foleni leo tarehe 17/03/2021 saa 4 asubuhi bosi wa mmoja akaitisha kikao na wenzake cha kujadili wanayoyafahamu ikabidi kazi zisimame tukasubiri kwenye foleni hadi kikao kikaisha ndio huduma ikarejea tena kwa kujivuta sana. .
Tunawapowahoji hawa wafanyakazi wa TRA kwa nini huduma zimekuwa almost grounded wanasema tatizo mtandao uko chini; hii ni sabotage. Ni almost wiki tatu TRA Arusha wanasingia mtandao kuwa chini kama chanzo cha huduma mbovu. Ina maana hawa watu hawana kitengo cha wataalamu wa komputa na kusababisha ukusanyaji wa kodi kuwa mbovu kiasi hicho; hii ni hujuma ya wazi kama wiki tatu zote wimbo unaoimbwa ni wa mtandao wa mfumo wa TRA Arusha uko chini na hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa .
Hasara wanayosababisha kwa serikali :
- Wafanya biashara wanaokuja kufanya tax clearance tayari wanakuwa wameandaa fedha ya kulipa kodi kwa robo ya kwanza ya mwaka wa kodi inayoishia tarehe 31/03/2021. Wengi wa wafanyabiashara hawa asilimia 80% wamehairisha kufanya tax clearance maana hawako tayari kupoteza masaa 5 TRA. Hivyo say wastani wa malipo ya kila robo ni laki tano (500,000) na kila wiki wafanyabiashara 2000 wanahairisha kulipa kodi; hii ina maana serikali ina kosa kulipwa kwa wakati bilioni moja(1,000,000) kila wiki ambazo zinahitajika kwenye miradi ya maendeleo haswa kipindi hiki serikali inatumia Zaidi hela zetu za ndani katika miradi ya maendeleo.
- Serikali inapata hasara kubwa kutumia mamilioni ya fedha za wavuja jasho kuwalipa wafanyakazi wasio na sifa wasiojituma , wasiojiongeza na wasio na uzalendo na nchi yao.
Ushauri wa bure kwa TRA na serikali:
- Serikali ikifumue hiki kitengo cha debt management na kutafuta vijana wanaojituma kwani walioko wengi wanafanya kazi kwa mazoe na kiburi
- Kuna baadhi ya wafanyakazi ndio wamehodhi suala la kufanya tax clearance licha ya kuwepo wafanyakazi wengi lukuki; hawa ndio wanalsababisha matatizo makubwa. Kwa mfano pale block ya Kijenge kuna mdada pale ni mzito kama jiwe na ndiye peke yake anayefanya Tax Clearance na anamhudumia mteja mmoja Zaidi ya saa na nusu very slowly na simu ikiita anakuacha anatoka nje anarudi baada ya dakika 20. Hii ni hujuma ya wazi.
- Baadhi ya wafanyakazi wa TRA hapo debt department wanafanya kazi kwa mazoea (business as usual na wamekosa ubunifu wa kuboresha ufanisi wa idara na wasiposhughulikiwa mtavuna mabua. Wao jua liwake mvua inyeshe they don’t care bora mwisho wa mwezi wamepokea chao. Hii ni hujuma, usaliti na kukosa uzalendo.
- TRA iboreshe appraisal forms za wafanyakazi ili wapimwe on performance basis na kila siku wapewe strict targets kama kigezo moja wapo cha kuwapima na siyo kujifanyia kazi kienyeji wakati wanai gharimu serikali mamilioni ya hela.