Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Habari wakuu,

Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda kwa Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema.

Kwanini Serikali wasingetumia pesa za kununulia ndege zisizozalisha na gharama za kufanya royal tour kufanya yote wanayotaka kufanya. Ni muda wa kufikiria kupunguza matumizi badala ya kututoza kodi mara mbilimbili kuongeza mapato kufanya matumizi yasiyo na kipaumbele au umuhimu.

Tozo benki.JPG
 
Naona hii ni hatari sasa
Tena inatakiwa iwe Benji zote na ghalama ziwe juu.

Hapa anayeathilika Ni mtu mwenye kipato Hawa WANYONGE hawahusuki kabisa,

Mnyonge akikuomba pesa unamtumia na ya kutolea kwa hiyo mtumaji anaghatwa ghalama ya mitandao na tozo,vivyo hivyo na mtumiwaja /mnyonge itakuwa umentumia ya pesa ya kutolea na pamoja na tozo,hivyo Basi anayeumia Ni mtumaji ambaye ndiye mwenye kipato.

Hapo mnyonge hawezi kujua ugumu wa maisha na uchaguzi ukifika ukimpa flana na kofia lazima akupigie kura ya ndiyo

Sijui tuwafanyaje Hawa WANYONGE?
 
Kuna mtu anatakiwa kubinywa naniii...hapa! Ngoja niangalie praiZi yangu Kama ipo
 
Habari wakuu,
Miamala yote ya fedha ya kibenki itayofanyika kupitia simu itaanza kukatwa tozo. Mathalan unataka kuhamisha fedha kutoka kwa Helena mwenye akaunti namba XX kwenda Huruma mwenye Account namba XY na ukatumia simu kufanya mchakato huo utawajibika kuichangia Serikali katika ujenzi wa madarasa, zahanati na mengineyo waliyoyasema...
Hatuhamishi pesa ng'ooo, tutakua tunaenda kufanya deposit bank au tunaandika cheque
 
Back
Top Bottom