Tovuti ya maoni ya wananchi imeishia wapi?

Sep 20, 2007
69
2
Wakati rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alitangaza kuanzishwa kwa tovuti ya serikali kwa ajili ya kupokea maoni, kero na kutolea ufafanuzi.

Mwishoni mwa mwezi wa August 2007, mkurugenzi wa Habari ndg Mpenda alitangaza kwa mbwembwe kuanzisha tovuti hiyo na alinukuliwa na Gazeti la Tanzania daima kama ifuatavyo:
Tanzania Daima August 31, 2007
Nimejaribu kufungua toviti hiyo kwa anwani aliyotoa mpenda ya www.mwananchi.go.tz lakini tovuti hiyo haifunguki. Nimejaribu kusearch google kwa keywords mbali mbali bila mafaniko. Je ni nini kimetoka?

Awali tovuti hiyo ambayo inasemakana iligharimu vijisenti vya kutosha ilikuwa inapatikana kwa anuani hiyo. Hata hivyo ilikuwa inaonekana kudorora huku ikipatikana kwa shida (Slow).

Ina maana kumbe hata maagizo ya rais huwa yanapuuzwa?
 
Kwi kwi kwi kwi

Tovuti ya wananchi hii hapa www.wananchi.go.tz

Tatizo lenu mumeamua matatizo na kero za wananchi kupeleka kwenye hizi tovuti zenu za mitandao JF, Michuzi Blogg na KLN news... kazi kwenu!
 
Wakati fulani mimi nilipeleka maswali kupitia tovuti hiyo, hayajajibiwa hadi hii leo na zaidi ya mwaka umepita
 

Huna haja ya Kushangaa Mkuu, website ya Taifa yenyewe bado imelala doro ije kuwa maoni tena ya wananchi tukiwamo WANAJF!
 

Wananchi wameisusa wameona ni usanii tu na wengi wameamua kuja hapa JF ambapo wanaona issue zinajadiliwa kwa mapana na marefu tena bila woga. Na wanazidi kumiminika kila kukicha.
 
Kwi kwi kwi kwi

Tovuti ya wananchi hii hapa www.wananchi.go.tz

Tatizo lenu mumeamua matatizo na kero za wananchi kupeleka kwenye hizi tovuti zenu za mitandao JF, Michuzi Blogg na KLN news... kazi kwenu!

Kasheshe... jaribu kutuma ya kwako.. wenzio tumewaandikia hao watu hadi vidole vimeuma! majibu yao miezi nenda ni:

HIlo jambo limepelekwwa kunakohusika na utapatiwa majibu. Kwanza hakuna cha email ya kuacknowledge wala nini. It is one of the biggest scam run by the government.
 

Mtu mmoja alisema tusiwe tunailaumu serikali kila kitu. Eti hayo ni matatizo ya wananchi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…