Tovuti ya maoni ya wananchi imeishia wapi?

Sep 20, 2007
69
2
Wakati rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alitangaza kuanzishwa kwa tovuti ya serikali kwa ajili ya kupokea maoni, kero na kutolea ufafanuzi.

Mwishoni mwa mwezi wa August 2007, mkurugenzi wa Habari ndg Mpenda alitangaza kwa mbwembwe kuanzisha tovuti hiyo na alinukuliwa na Gazeti la Tanzania daima kama ifuatavyo:
Tanzania Daima August 31, 2007
SERIKALI imeanzisha tovuti maalumu ambayo itawawezesha wananchi kuuliza maswali na kuwasiliana na serikali, kutoa maoni, ushauri au kero mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi wa Idara hiyo, Kassim Mpenda, alisema Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imekamilisha utekelezaji wa agizo la rais la kuanzishwa kwa tovuti hiyo.

"Tovuti ipo hewani tayari kwa kutumiwa na wananchi, tumeifanyia majaribio kwa miezi miwili sasa na tumeridhika kuwa sasa inaweza kutumiwa na wananchi bila wasiwasi," alisema.

Mpenda alisema taratibu zipo mbioni ili tovuti hiyo izinduliwe rasmi katika siku na wakati muafaka ili kuwa tayari kwa kutumiwa na wananchi.

Alisema kuwa kwa kuanzishwa kwa tovuti hiyo, sasa kutamwezesha mwananchi kuwasiliana na serikali kwa kutumia njia nne ambazo ni tovuti hiyo, barua, ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu ya mkononi au mwananchi kwenda moja kwa moja idara husika kuwasilisha kero yake.

Mpenda alisema tayari wameshaingia mkataba na kampuni za Vodacom, Celtel na Tigo na kusisitiza kuwa bado wanafanya mazungumzo na Zantel, hivyo mwananchi atakapotumia huduma hiyo atalipia sh 150 kwa ajili ya huduma ya ujumbe mfupi wa simu.

Alisema kila mwananchi atakayewasilisha maswali au kero serikalini kupitia www.mwananchi.go.tz au simu namba 15715, atakuwa anapatiwa majibu kutoka katika wizara husika kwa kipindi kifupi iwezekanavyo.

Kama ilivyo kwa njia nyingine zote za mawasiliano, hasa vyombo vya habari, tovuti ya wananchi inakusudia kufanikisha utekelezaji wa kifungu cha 18 cha katiba, ambacho pamoja na mambo mengine, kinampa kila raia haki ya kupata taarifa.
Nimejaribu kufungua toviti hiyo kwa anwani aliyotoa mpenda ya www.mwananchi.go.tz lakini tovuti hiyo haifunguki. Nimejaribu kusearch google kwa keywords mbali mbali bila mafaniko. Je ni nini kimetoka?

Awali tovuti hiyo ambayo inasemakana iligharimu vijisenti vya kutosha ilikuwa inapatikana kwa anuani hiyo. Hata hivyo ilikuwa inaonekana kudorora huku ikipatikana kwa shida (Slow).

Ina maana kumbe hata maagizo ya rais huwa yanapuuzwa?
 
Kwi kwi kwi kwi

Tovuti ya wananchi hii hapa www.wananchi.go.tz

Tatizo lenu mumeamua matatizo na kero za wananchi kupeleka kwenye hizi tovuti zenu za mitandao JF, Michuzi Blogg na KLN news... kazi kwenu!
 
Wakati fulani mimi nilipeleka maswali kupitia tovuti hiyo, hayajajibiwa hadi hii leo na zaidi ya mwaka umepita
 
Wakati rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alitangaza kuanzishwa kwa tovuti ya serikali kwa ajili ya kupokea maoni, kero na kutolea ufafanuzi.

Mwishoni mwa mwezi wa August 2007, mkurugenzi wa Habari ndg Mpenda alitangaza kwa mbwembwe kuanzisha tovuti hiyo na alinukuliwa na Gazeti la Tanzania daima kama ifuatavyo:
Tanzania Daima August 31, 2007
Nimejaribu kufungua toviti hiyo kwa anwani aliyotoa mpenda ya www.mwananchi.go.tz lakini tovuti hiyo haifunguki. Nimejaribu kusearch google kwa keywords mbali mbali bila mafaniko. Je ni nini kimetoka?

Awali tovuti hiyo ambayo inasemakana iligharimu vijisenti vya kutosha ilikuwa inapatikana kwa anuani hiyo. Hata hivyo ilikuwa inaonekana kudorora huku ikipatikana kwa shida (Slow).

Ina maana kumbe hata maagizo ya rais huwa yanapuuzwa?

Huna haja ya Kushangaa Mkuu, website ya Taifa yenyewe bado imelala doro ije kuwa maoni tena ya wananchi tukiwamo WANAJF!
 
Wakati rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alitangaza kuanzishwa kwa tovuti ya serikali kwa ajili ya kupokea maoni, kero na kutolea ufafanuzi.

Mwishoni mwa mwezi wa August 2007, mkurugenzi wa Habari ndg Mpenda alitangaza kwa mbwembwe kuanzisha tovuti hiyo na alinukuliwa na Gazeti la Tanzania daima kama ifuatavyo:
Tanzania Daima August 31, 2007
Nimejaribu kufungua toviti hiyo kwa anwani aliyotoa mpenda ya www.mwananchi.go.tz lakini tovuti hiyo haifunguki. Nimejaribu kusearch google kwa keywords mbali mbali bila mafaniko. Je ni nini kimetoka?

Awali tovuti hiyo ambayo inasemakana iligharimu vijisenti vya kutosha ilikuwa inapatikana kwa anuani hiyo. Hata hivyo ilikuwa inaonekana kudorora huku ikipatikana kwa shida (Slow).

Ina maana kumbe hata maagizo ya rais huwa yanapuuzwa?

Wananchi wameisusa wameona ni usanii tu na wengi wameamua kuja hapa JF ambapo wanaona issue zinajadiliwa kwa mapana na marefu tena bila woga. Na wanazidi kumiminika kila kukicha.
 
Kwi kwi kwi kwi

Tovuti ya wananchi hii hapa www.wananchi.go.tz

Tatizo lenu mumeamua matatizo na kero za wananchi kupeleka kwenye hizi tovuti zenu za mitandao JF, Michuzi Blogg na KLN news... kazi kwenu!

Kasheshe... jaribu kutuma ya kwako.. wenzio tumewaandikia hao watu hadi vidole vimeuma! majibu yao miezi nenda ni:

HIlo jambo limepelekwwa kunakohusika na utapatiwa majibu. Kwanza hakuna cha email ya kuacknowledge wala nini. It is one of the biggest scam run by the government.
 
Mtu mmoja alisema tusiwe tunailaumu serikali kila kitu. Eti hayo ni matatizo ya wananchi wenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom