Tour fupi ya shamba langu la greenhouse


Bro Open Field Kit ni kiasi gani na inachukua ukubwa gani kwa balton
 
Duuh umenifungua akili ila niko mbali na wewe. Niko arusha alafu shamba langu liko karibu na maji kabisa. Nataka kulima nyanya mda si mrefu nasaka hiyo hybrid.
 
mbona hata hujaitaja sasa hii aina ya mbegu?
 
Mwala juzi nilipata simu kutoka kwa jamaa anaitwa Jackson akitaka nimfundishe haya maujuzi ya kilimo. Nikamwambia aje shamba ajifunze. HaKuja. Sasa leo ananipigia tena akitaka aanze kulima. Akasema ni uoga tu wa kujaribu vitu vipya ndio umekuwa ukimrudisha nyuma.

Nimeamua kuandika haya kwa kuwa nimegundua kuwa watz ss ni waoga wa kujaribu vitu vipya km kilimo n k. Hivyo kuna umuhimu wa watu wrote kujaribu kuondoa uoga na kuamua kulima kisasa. Tusiruhusu kuwa watumwa wa uoga. Tembelea shamba darasa ujifunze
 
Mkuu biashara 2000 ukienda pale balton wanaweza kukuzia vifaa vya greenhouse kama zile UV plastic, drop irrigation... bila ya kutaka wao wa kujengee? yaaan ukitaka kununua vifaa tu wanaruhusu bila wao kuja kukujengea?
 
Mkuu biashara 2000 ukienda pale balton wanaweza kukuzia vifaa vya greenhouse kama zile UV plastic, drop irrigation... bila ya kutaka wao wa kujengee? yaaan ukitaka kununua vifaa tu wanaruhusu bila wao kuja kukujengea?
Yes wanaweza ila wale wa arusha 0719222722
 
Mkuu biashara 2000 zile. mbegu za anna f1 zinakubali nchini kwetu hapa? au ni mbegu gani ya hybrid inayokubali Tanzania kwenye greenhouse?
 
Mkuu kabla sijakupigia simu ili uniweke sawa baadhi ya mambo, naomba kuuliza huko dar mbegu aina ya eden f1 inauzwaje?
Huku arusha gm 50 ni sh 405000/=
 
Mkuu habari

Tafadhali hiki kilimo cha green house kinawezekana kufanyika maeneo ya Dar es salaam, Kibaha au Bagamoyo?
 
Green house inakubal popote tanzania hii sema tutambue watanzania wengi tunatumia walking tunnels sio green house maana green house ni ile inayoweza ku control all weather elements kama mvua,jua,hali ya hewa etc,sasa hizi walking tunnels popote unafanyia kazi sema vipimo vitakua tofauti usitegemee vipimo vya Arusha kufanya vyema dar es salaam
Pili tusiruke hatua ,tafadhar kabla hujajenga green house/walking tunnel pima udongo na maji ujue kweli yanafaa wewe uweke green house /walking tunnels,maana kama eneo lina magadi unalima mazao yanayovumilia kama beetroot bila hata ya kuweka hiyo gh/walking tunnel.
Mazao ya green house ni hoho(za rangi na zile ndefu zenye mchanganyikl wa hoho na kali,nyanya ndefu (indeterminate),tango ,maua hapo itakulipa sio green house/walking tunnel unalimia mboga za majani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…