Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili
Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi
The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya
Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz