Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Biashara2000

JF-Expert Member
Nov 9, 2013
636
540
Habari za asubuhi.

Kwa wale waliotaka angalau kuona kwa ufupi shamba langu la greenhouse ambalo nimelima nyanya ndani ya greenhouse na nje pia yaani bila greenhouse ila kwa kutumia formula maalumu ya kitaalamu ya kutumia gharama kidogo ila mavuno mengi na makubwa wanaweza ku click hiyo video hapo chini na kuangalia.

0758 308193

Last edited by a moderator:
Nimeona hapo umeongelea kuhusu formula. Je kwa mimi niko huku mbeya gharama yako ya kunieleza hiyo formula ni bei gani?
 
Ngoja nikupe mfano. Tuseme unaishi katika nyumba ambayo kwa upande wa nyuma una eneo ambalo lina ukubwa wa upana hatua tano na urefu vile vile. Hivyo 5 x 5 = 25 square meter. Katika kila square meter 1 unapanda miche 4 hivyo x 25 ni miche 100. Kila mche unakupa kilo 15 yaani sawa na ndoo moja na nusu ya nyanya kwa mwezi. Bei ya shambani ukiamua kufanya mia tano x 15 ni sh. 7,500 kwa kila mche kwa mwezi. 7,500 x miche 100 = sh. 750,000 kwa mwezi. Je kwa miezi nane ya uvunaji itakuaje? 6,000,000. Na hii ni bila greenhouse

Je utaendelea kunyanyaswa na bosi wako ulipoajiriwa na kuendelea kumtajirisha mpaka lini?
 
Nimeipenda hii. Vipi kuhusu maji?

Nadhani umeuliza i general zaidi sijajua nijibu vipi ila ntajibu kama nilivyolwa. Maji si lazima uwe nayo t neo lako ila unataiwa tu uwe na sehemu ya kuyahfadhia pindi unapoyaleta kutoka huko utaapoyatoa. Unaweza uaweka tanki au mapipa kuhifadhia maji. Si lazima uwe na kisima au maji ya dawasco
 
Nadhani umeuliza i general zaidi sijajua nijibu vipi ila ntajibu kama nilivyolwa. Maji si lazima uwe nayo t neo lako ila unataiwa tu uwe na sehemu ya kuyahfadhia pindi unapoyaleta kutoka huko utaapoyatoa. 0Unaweza uaweka tanki au mapipa kuhifadhia maji. Si lazima uwe na kisima au maji ya dawasco

Kweli nimeuliza general. Nilimaanisha kwa siku maji yanatumika kiasi gani kwa hiyo miche 100
 
naomba kujua ni aina ipi ya nyanya nzuri kulima ambayo iko na shelf life kubwa???

Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili

Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi

The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya

Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz
 
Asante sana na ubarikiwe maana wengi tunaposikia mbegu ya yanya tunaikimbilia pasipokujiuliza hio mbegu ni kwaajiri ya eneo lenye hari ipi ya joto
umeongelea mbegu moja unayotumia ila hukuweka jina la hio mbegu, nitashukuru kama ukanijulisha jina la hio mbegu nikaitafuta
 
Kwa ambae ashatumiwa fomula na biashara 2000 atoe ushahidi tusije tuma 20000 zikabebwa. ..mjini shule
 
Nimepata hamasa ya kufanya hichi kilimo cha nyanya. Ningependa kujua kama nyanya ili kustawi zinahitaji udongo wa aina gani? Eneo kama Kibaha is it favourable?
 
Similar Discussions

54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom