Tosamaganga high school

Lucas

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,457
Reaction score
1,111
katika pitapita yangu sehemu mbalimbali mtandaoni nimekutana na PIcha za Shule yangu niliyosoma miaka hiyo.



hapo juu ni quarter mile



hapa ni DH, ila hii inaonekana ni miaka ya karibuni



hapaa ni Sinagogi



Hapo ni juu ni parade na kwa nyuma ni madarasa ya f5



trench za dining



Bweni nililokaa enzi hizo nasikia siku hizi halitumiki!! lina zaidi ya miaka 100, na halina nondo!! kwa sasa ukitembea huko juu lina-swing



hapa bila shaka kulikuwa na event ama mitihani inaendelea dinning Hall



mlango wa ofisi ya Head prefect... hivi Zitto alipokuwa Tosamaganga alikuwa kiongozi wa nini?










hapo enzi hizo upite kwa umakini waweza pigwa "splash"








posta









hapa enzi hizo simu za mkononi zimeingia ilikuwa ni sehemu pekee iliyokuwa inakamata network!
 
dah! shukurani sana yaani umenikumbusha mbaaali sana.<o😛></o😛>
 
dah! shukurani sana yaani umenikumbusha mbaaali sana.<o😛></o😛>

Thanks mkubwa kwa kunikumbusha enzi hizo nilikuwa pale 2000 to 2002. Yaani umetudondoshea picha zote za kila Angle ya Tosa ukiondoa Mashamba ya nyanya na mahindi pia madarasa ya EGM na kwa masista si unakumbuaka banzi mkuu. Kupitia Tosa unajifunza mengi sana nitaenda pale kuvisit one day. My school i miss you so much.
 

ah ha ahahhah Darasa la rafiki yangu met wangu mmoja alikuwa anitwa Rashid Makwinya sijui yuko wapi huyu mtu!!
 
Asante kwa picha hizi kwani umenikumbusha mbali sana. Hapo zimekosekana za idete kule shambani na msiwasi uwanja wa mpira. Long live Tosamaganga!
 
mkuu nimekuaminia, ila nasikitika kama mandela halituiki, ndo lilikua bweni langu, umenikumbusha mbali mno,
enzi za mwalimu mkangwa, duuu kweli life goes on
 
duuuu! Umenkumbusha mbali mno, miaka 10iliyopita nlikuwa hapo, huyo apo assemble ground atakuwa ni mkakwa kama sio ka50, afu hyo picha itakuwa ilipigwa na Soja na itakuwa siku ya ijumaa, a.k.a ukaguzi day. Umenikumbusha splash a.k.a kiwora, du. Naskia maticha wengi wa enzi zile washavuta
 
Du! Asante sana kwa kumbukumbu nzuri. Nilikuwa hapo wakati wa ule mgomo uliomuondoa marehemu "Dudu". Walikuwepo akina Boyd "Mnazareti", Biga Kipemba, Joseph Paschal, Patrick Rwehumbiza, Kimti, Japhet Makau, Bruce Mwile, Msasalaga na wengineo wengi.
 
Asante kwa picha hizi kwani umenikumbusha mbali sana. Hapo zimekosekana za idete kule shambani na msiwasi uwanja wa mpira. Long live Tosamaganga!


Ngoja nizitafute za idete
 
Du! Asante sana kwa kumbukumbu nzuri. Nilikuwa hapo wakati wa ule mgomo uliomuondoa marehemu "Dudu". Walikuwepo akina Boyd "Mnazareti", Biga Kipemba, Joseph Paschal, Patrick Rwehumbiza, Kimti, Japhet Makau, Bruce Mwile, Msasalaga na wengineo wengi.

Hivi Mbanga mlikuwa mnamuita dudu?
 
nawaonea wivu sana mliosoma TOSA wote nnaowajua waliopita hiyo shule ni vichwa. mdau tafuteni picha za ile soccer ground yenu. nshaupiga sana pale na timu ya kita ya ipogoro. tukiwa daraja la tatu tukaja cheza na nyie ilikuwa 1994 mkatupiga 3-1 tukaishia kujipooza na ulanzi pale njia panda ya tosa. Lipuli walikuwa wanaweka kambi yao hapo wakati wakiwa ligi kuu miaka hiyo wakatualika tukaja cheza nao wakatutandika nne bila majibu tulichoka hadi tukashindwa kunywa tena mkangafu pale njia panda. Timu ya kitaa nayo KIBWABWA tukaja hapo Tosa kucheza na timu ya ma bruda ikiongozwa na bruda mmoja akiitwa Mvule km sikosei. hii timu ya kitaa ilikuwa special watu wawili ndo tulikuwa over 18 wengine wote ni under 16 lkn tuliwaendesha puta mabruda wakatushinda kwa mbinde 4-3 so tosa pananipa good memories
 
tatizo Tosa Boys walikuwa msuli sana, humu jamvin hawapo. Ila naskitika sana hamna mtu aliyevunja record ya Prof Sarungi so far.
 
Hapo pa kupigia simu palikuwa pakiitwa ''cattle unit"!
 
Mandela Old bado linatumika wakuu,ukipita kizembe splash kama kawa!Long live that place duh
 
Mkuu kwa waliopita miaka ya 1986 hadi 1989 watakumbukuka bweni hili lisilotumika lilikuwa linaitwa Muungano mabweni mengine yalikuwa yanaitwa Mapinduzi, Azimio n.k mmekunywa sifongo nyie? walahi nimekumbuka mbali enzi za heamaster Dudu
 
Asante sana kijana umenikumbusha mbali sana 1981-1984 huyo headmaster Dudu alikuwa noma sana usipime,ukiitwa ofisini kwake jiandae kwa ngumi pia,ni shule nzuri tatizo hivyo vimito wakati wa masika kichwani umekolea ulanzi weeee!!!!baadhi ya wanafunzi walipoteza maisha.Ni kipindi ninachokumbuka shule ilipokea wanafunzi toka kibiti secondary sikumbuki vizuri walipata matatizo gani shuleni kwao.
 
Shule la kimaskini mnapoteza muda kulipromoti. Na sisi tuliosoma Shaaban Robert kisha Bonn (Germany) tukiweka picha zetu? Mbaaffffff


kama hujasoma zooo ntashangaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…