Top universities in Tanzania 2018

Mleta maada kasoma UDOM kwahyo anaamua kufool jamii kuonyesha kwamba UDOM ni chuo bora. UDOM haiwezi kuisogelea UDSM na haiwezi kuwa juu ya Mzumbe na SUA....
 
Wengi mnaobishana na takwimu hamna la kujitetea isipokuwa hoja ya mazoea yenu mliyokuwa nayo
 
Kwa ukubwa wa maeneo hii takwimu si eti eeee[emoji2]
 
Kati ya hivyo ni ambacho graduates wake wanaongoza kwa ufisadi, ubadhirifu, ulaji rushwa, uhujumu uchumi, nk?
 
Namba 1 wamependelewa maana wanatoa products za ovyo sana sana
 
Mkuu research ulifanya lini?, kama haukufanya hii list piga nayo picha tuma kwenye whatsapp
 
Watu wasioijua UDOM watashangaa imefikaje hapo juu, lakini mm ninayeijua sishangai kabisa. Hawa jamaa walianza vibaya saana wakiwa hawana waalimu wenye degree 3, au 2 lakini wakawaendeleza saaana na sasa wana waalimu wakutosha saana. Hawana haja tena ya kuajiri PhD holders, wenyewe wanaajiri first degree tu then wanamtrain mpaka anakuwa na PhD. Na training zao zina malengo sio kuwa watu wanajisomea watakavyo bali wanasoma waje wajaze upungufu wa chuo. Kwa ss UDOM ina PhD holders weengi karibia na UDSM kama (hawajaipita bado)
 
Mmmh! Source of information please, UDOM kuizidi MUHAS na SUA
 

unafeli, kuna waalimu UDSM hawa qualify kufundisha baadhi ya kozi lakini UDOM ina wa bookia tiketi za ndege kila wiki waje kufundisha
 
hizo mbwembwe zote za top university mganga mkuu ni mtaani, jua likikuwakia ndo utajua ajira ni bahati sio chuo ulichosoma haya mambo huwa tunajisifia tukiwa chuo, lakini mwisho wa siku inafika hatua unakichukia cheti chako , kujua vitu na utendaji wako havihusiani na chuo ulichotoka bali ni juhudi zako binafsi za kujifunza vitu vingi, kuna mdada mmoja alisoma Udsm alimaliza sheria mwaka 2012 mpaka ninapoandika hapa hajabahatika kupata kazi kaamua kuuza vitenge na nguo za ndani, lkn alivyokuwa anasifia hicho chuo kwa sisi ambao hatukubahatika kusoma hapo tulikuwa hatulali, mungu si athumani tukamaliza mwaka wa mbele yake tukapata ajira na tukajiendeleza na fani nyingine hapohapo UDSM na maisha yanasonga, siku hizi simsikii kabisaa akileta hizo story nilichojifunza mimi ni kwamba mwisho wa siku ni kupata ajira huko makazini hawakuulizi jina la chuo bali huangalia perfomance yako tuu, na uzuri wake vyuo vyote viko chini ya TCU, mtu usijisikie vibaya kwamba chuo chako ni kibovu kazana tuu kusoma kwa bidii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…