"CCM mbona imekaa kimya? CUF mbona wamekaa kimya? Tunataka waseme, naona wanajua Watanzania ni wepesi kusahau na inethibitishwa na hapa jinsi michango ilivyofifia na kuhamia katika topic nyingine ambayo nayo itakufa ikiibuka mpya, hakuna utekelezaji wala ufuatiliaji.
Hapa kuna issue nzito, ama CCM imemtuma RA kuua upinzani, ama yeye RA anatumia hiyo ili kupata kinga kwa upande wa upinzani!! Yote si mema hata kidogo kwa mustakabali wa nchi yetu, na hakuna anayejali!!!!"
__________________________
Halisi:
Umenena ndugu yangu, hakuna anayejali. RA anaogopwa sana na serikali ya CCM -- anaweza hata kuamrisha JK ajiuzulu -- na kweli JK akajiuzulu, kwani anaogopa asije RA akamwaga mambo -- you know Kagoda, Afriteiner, Richmond etc -- kutoa evidence walikuwa pamoja.
Hali hii imekuwa inadhhofisha kipindi hiki cha kwanza cha utawala wa JK pamoja na mazuri aliyokuwa akitarajia kuyafanya kwa Watanzania.
Aidha inatisha kuona kuwa hali itajirudia hivyo hivyo katika kipindi chake cha pili, iwapo atakuwa Rais tena -- kama jinsi anavyotaka, na huku RA akiwa bado na 'mpini' wake -- kwani haitarajiwi atauachia -- kwani anaona ni kinga kubwa sana kwa ufisadi aliowafanyia Watanzania.
Namshauri JK ajitutumue angalau kidogo, apige moyo konde na aseme potelea mbali na aanze kumshughulikia mtu huyu -- na nina imani umma utakuwa nyuma yake. Mtu mmoja hawezi akaachiwa akasumbua umma mzima kama vile sote ni mambumbu kwake.
Hatari ni kwamba Ra anazidi kujizatiti na inaweza kufikia hatua ambayo JK hawezi kubakiwa na uwezo wowote wa kumshughulikia na ikawa kwamba yeye ndiyo atashughulikiwa.
Siamini kabisa kama mawazo haya yanatoka kwa mtanzania. Natamani kulia nashindwa. Umekata tamaa, unaishi maisha ya jana, mawazo yako yamekanamizwa, umekuwa mtumwa huna uhuru.
Ulichosema hapo hakiingii akilini hata kidogo. Unaposema RA anaweza kumwambia JK ajiuzulu! kwa kifupi una declare RA yuko juu zaidi ya JK.
Unaposma JK ajitutumue sijajua how, wakati juu yake yuko RA!
Unachoficha hapa ni kuwa JK na uwezo wa kufanya lolote! lakini bado unasema ajitutumue, wakati ni rais wa nchi, ivi unaua unachosema??
unataka kuvunja ndoa ya JK RA an EL, kwa maneno yako ya 'kichovu' kuwa eti JK alipanga kufanya mambo mazuri kwa watanzania?? mwongo wewe! mambo gani mazuri aliyopanga ?
Mapango wa hawa jamaa watatu ulianzia miaka 10 iliyopita, leo kwa sentensi zako za kitoto bado unaamini kuwa JK anakupenda!!!!!
wewe amka sasa acha mawazo haya ya kitumwa, fanya uwezavyo , hubiri kwa kila kiumbe kule kuwa CCM waondoke madarakani, RA alitumiwa na angetumiwa yeyote yule, hii ni sera ya CCM kutumia kodi zenu ili wazidi kukaa madarakani.
Mnapomsema RA inaonyesha jinsi gani msivyotaka kuvamia na kung'oa mzizi huu uitwao CCM.
Sentensi za aina zako ni nyingi kuwa tumuone JK msafi wakati ananuka yeye na serikali yake, sitasita kussema kwa mawazo yako wewe ni FISADI na adui namba moja kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Nyie na mawazo yenu ya RA mnaficha ukweli RA atabaki tu maadam CCM ipo pale, LAO MOJA wote si akina mwakyembe wala akina kilango
kaa na mawazo yako hayo utaona mwisho wake
wewe na mawazo yako haya ya kifisadi endeleeni kuwadanganya hao hao kuwa tusiiseme CCM NA JK wake tumseme RA. kamtu kadogo kuliko kawaida! RA ashindane na usalama wa taifa, mahakama, jeshi, RA aongoze watanzania milioni 40 RA??
CCM wanaweza mpaka kuwachukulia wake zenu mkabaki kusema Rostam! pia kumbuka mafisadi walioifilisi na wanaoifilisi nchi hii ni wengi na wamekula hela nyingi kuliko kukaa kumsema RA aliyeiba na kupewa support na weusi kama wewe na mimi kwa kupitia CCM! wabaya ndugu zetu hawa hawa, tunaopanda daladala zao na wanatuchangia harusi zetu!
CCM has to go with all its roots, that is a solution