Wako wengi wanamjua na wana tabia kama zake katika mambo fulani fulani. Na pia wako wengi ambao hawajui mambo kwa jumla. Remember, watu hawakumtaka Obama kwa sababu si mzungu. Lakini kuficha hilo walifurahi kusikia mtu akitumia pesa nyingi kudai kwamba Obama alizaliwa Kenya. Na Trump ndiyo huyo mtu aliyetamba ametumia pesa zake kujaribu kulichimbua hilo. Mpaka leo kuna asilimia kubwa ya republicans (kama robo yao hivi) wanaamini kwamba alizaliwa Kenya, pamoja na ushahidi wote. Hilo lieleweke vipi? Ni wale wale wasioridhika na kuongozwa na mtu ambaye si mzungu. Na wengine kwa hakika wanasema hivyo kabisa. Kwa sababu hiyo basi, wengi wanaona kwamba Democratic party kimejiweka karibu mno na watu ambao wao wanaona hawastahili.Umesema mm simjui Trump vizuri nimeanza kumfuatilia trump juzi tu.
Sawa hilo unaweza kuwa sahihi lakini swali linakuja je hao walio mchagua Trump kwenye Kura za maoni nao hawamjui Trump vizuri?
Na kama Trump ni mwizi inamaana hao waliokuwa wanamchagua Trump hawakuwaona watu wengine ambao sio wezi.