Toka singida : Kamanda john mnyika kuwa shahidi kesi ya mauaji.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toka singida : Kamanda john mnyika kuwa shahidi kesi ya mauaji....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Jul 21, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

  Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

  Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

  Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.


  Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

  Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

  Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Yale ya Igunga na Arumeru yaliishia wapi?
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  hawa polisi na ccm yao ni wapuuzi!
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hivi kuld mwanza watuhumiwa wa kuwakata mapanga na kuwajeruhi wabunge hainess kiwia na machemuli wameshapatikana? Arumeru je mauaji ya mwenyekiti wa cdm vipi? Au siku zote anakunya kuku wengne wanatoa ushuzi
   
Loading...