Toka lini TAKUKURU wanatembea na SMG na AK47 na bila vitambulisho?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hebu tuache hii tabia ya kijinga ya kuumauma maneno na kujipendekeza. Call a spade a spade, not a big spoon. Wazee wa kujipendekeza wameanza kupayuka "ooh Nyalandu yupo TAKUKURU, Chadema mmezusha kuwa amekamatwa na watu wasiojulikana"

Iko hivi. Nyalandu alikua kwenye kikao cha ndani pale Itaja. Wamekuja watu wakiwa na silaha za moto, AK47 na Sub Machine Gun. Kufika wakasema wanamtaka Nyalandu, David Jumbe na Mwenyekiti wa Chadema kwenye kata hiyo. Walipoulizwa wao ni nani wakakataa kujitambulisha. Hata vitambulisho wamegoma kutoa. Wakawashurutisha watu hao watatu hadi kwenye gari na kuondoka nao.

Sasa mlitarajia Chadema waote kuwa hao ni maafisa wa Takukuru? Hivi kama wamekataa kujitambulisha wangejulikanaje kuwa ni Takukuru? Kwahiyo taarifa kwamba ni watu wasiojulikana ni sahihi as long as walikataa kujitambulisha.

Pili; hivi ni kuanzia lini maafisa wa Takukuru wameanza kutembea na silaha za kivita kama AK47 au SMG? Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 ya mwaka 2007 inazuia afisa wa Takukuru kubeba silaha yoyote (hata rungu). Leo watu wanaenda na AK47 halafu tunaambiwa ni maafisa wa Takukuru na tunakubali kirahisi kabisa. Shame on u. JPM aliwahi kusema watanzania sio wajinga kama mnavyodhani.

Halafu Takukuru kama walikua wanamhitaji Nyalandu wangeweza kumpa tu 'notice' akaripoti ofisini kwao. Hakukua na haja ya kutuma watu wenye silaha za kivita kwenda kumfanyia ambush kama jambazi. Nguvu zote hizo kwa faida ya nani?

Tatu, ni mara ngapi ndugu zetu wamechukuliwa na watu ambao walikataa kujitambulisha na hawajaonekana hadi leo? Azory Gwanda alichukuliwa na watu waliokataa kujitambulisha na hadi leo hajaonekana hata mfupa wake. Erick Msyaliha the same. Sasa leo wanakuja watu kumchukua Nyalandu wanakataa kujitambulisha mlitaka tueleweje.

Kule Musoma it was the same scenario. Watu waliokataa kujitambulisha walitaka kumchukua Zacharia. Alipowazidi nguvu na kuwatandika risasi ndio tukaambiwa ni maafisa usalama. Kama wangefanikiwa kumchukua, sina hakika kama wangekaa wajulikane kuwa ni watu wa usalama. Pengine tungeendelea kuambiwa ni watu wasiojulikana.

Mwisho ni kwa wafuasi na wanachama wa Chadema pale Itaja. Mmezingua sana. Yani watu wanachukuliwaje kwa nguvu wakiwa kwenye kikao na nyie mnakaa kimya? Nyie ndo mnafanya tuonekane 'maboya' wa kutekwa tu wakati wowote hawa 'maharamia' wanapojisikia kufanya hivyo.

Kitendo cha hao jamaa kukataa kujitambilisha ilitakiwa muwazuie kuwachukua kina Nyalandu. Jukumu la wanachama ni pamoja na kuwalinda viongozi wao kwa gharama yoyote. Sasa nyie mmeona mitutu mkanywea? Mkaacha jamaa wakachukuliwa kama kuku? Mmezingua sana. Kama na nyie mnajiita 'makamanda' basi tuna safari ndefu sana ya kufikia ukombozi.

Credit to G malisa
 
Nyarandu au Nyalandu?

Pili kwani Afisa wa TAKUKURU haruhusiwi kubeba silaha?

Pengine hatuna uelewa wa kutosha kwamba TAKUKURU nao ni askari?

Ila kwakuwa kila jambo tunaingiza siasa tunaweza ama mtetea Nyalandu wakati Ana makosa, au Tukamuonea wakati hana Kosa,

Britannica
 
Umesoma vizuri andiko la mtoa mada? Kuna sehemu katoa kifungu cha sheria kuhusu ubebaji silaha. Relax
 
Mtu kama rambirambi anaiba Atashindwa kufanya hivi??
 
Umesoma vizuri andiko la mtoa mada? Kuna sehemu katoa kifungu cha sheria kuhusu ubebaji silaha. Relax
Nyumbu hawajielewi ndo maana wanatuletea kwa nguvu viongozi washamba na malimbukeni
 
Nakumbuka kuna kamanda alitekwa makambako jamaa wakasema.eti Amekamatwa na Tanesco
Makamanda walikua kina marehemu Mawazo na aliyebaki ni Jacob meya ubungo,huku kujifanya kutii ccm watawachezea sana wapinzani kwa kutumia vyombo vya dola.
 
Nyarandu au Nyalandu?

Pili kwani Afisa wa TAKUKURU haruhusiwi kubeba silaha?

Pengine hatuna uelewa wa kutosha kwamba TAKUKURU nao ni askari?

Ila kwakuwa kila jambo tunaingiza siasa tunaweza ama mtetea Nyalandu wakati Ana makosa, au Tukamuonea wakati hana Kosa,

Britannica
No hapo uko wrong. Hatukuzoea au hatukupewa elimu ya kuwa Takukuru kuwa nao wanabeba silaha kubwa za kivita ktk kumkamata mtuhumiwa wa rushwa. Mtu ujakamatwa na rushwa inabidi uitwe kwenye ofisi husika ikizingatiwa aliyekamatwa kwa vifaa vya kivita amewahi kuwa waziri ktk nchi hii na anayo address inayotambulika.

Acha kutetea upuuzi. Serikali ya Magufuli imekuwa ya kipumbavu sana isiyojali sheria siyo jali utu wala kujua binadamu anayothamani gani. Hakika nakuambia hakuna watu watakaoteseka hapo baadae kama viongozi wengi wakuu wa serikali wenye kupindisha sheria kwa kumfuata Magufuli.

Unajua watanzania wengi hasa hao viongozi wamejisahau hawajui yanayokuja kesho. Wanachojua ni kuwa watatawala MILELE na akiingia mtawala mwingine atakuwa ni ccm na atawatetea.

Ipo siku yote haya yatafufuliwa na akina Magufuli watakuwa jela hata zikipita miaka 50 maadamu wako hai sheria itachukua mkondo wake pasipo kujali umri.
 
Nyarandu au Nyalandu?

Pili kwani Afisa wa TAKUKURU haruhusiwi kubeba silaha?

Pengine hatuna uelewa wa kutosha kwamba TAKUKURU nao ni askari?

Ila kwakuwa kila jambo tunaingiza siasa tunaweza ama mtetea Nyalandu wakati Ana makosa, au Tukamuonea wakati hana Kosa,

Britannica
Kifupi uelewa wa chadema kwenye Mambo mengi ya nchi uko chini unashangaa mtu wanataka kushika nchi kwa uelewa mdogo huu walionao.They are too low hawajafikia upeo wa kupewa nchi kiwango Chao Cha uelewa Kiko chini mno Tena mno
 
No hapo uko wrong. Hatukuzoea au hatukupewa elimu ya kuwa Takukuru kuwa nao wanabeba silaha kubwa za kivita ktk kumkamata mtuhumiwa wa rushwa. Mtu ujalamatwa na rushwa inabidi uitwe kwenye ofisi husika ikizingatiwa aliyekamatwa kwa vifaa vya kivita amewahi kuwa waziri ktk nchi hii hivyo anayo address inayotambulika. Acha kutetea upuuzi
Eti uitwe nyoooo wewe Nani Huwezi pangia chombo kikubwa Kama hicho au polisi waku fanyieje je Kama ulikuwa na mpango wa kutoroka nchi ? Huo muda wakikustua kukuita Sio ndio utapata nafasi ya kutokomea gizani.Usiwafundishe kaxi
 
Screenshot_20190527-213938_1.jpeg
 
Eti uitwe nyoooo wewe Nani Huwezi pangia chombo kikubwa Kama hicho au polisi waku fanyieje je Kama ulikuwa na mpango wa kutoroka nchi ? Huo muda wakikustua kukuita Sio ndio utapata nafasi ya kutokomea gizani.Usiwafundishe kaxi
Independent na kesi na kesi usifikiri kila kitu ni kukamata tu kwa silaha hivi nyie watu mko dunia ya wapi mbona mko kama wanyama. Tofautisha binadamu na mnyama
 
Back
Top Bottom