Togolai Kimweri arushiwa virago vyake TBA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Togolai Kimweri arushiwa virago vyake TBA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Aug 22, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kimweri aondolewa TBA [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 21 August 2011 21:30 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Ramadhan Semtawa
  OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Togolai Kimweri, ameondolewa kwenye wadhifa huo.Kwa sasa nafasi yake inashikiliwa kwa muda na msaidizi wake aliyefahamika kwa jina moja la Njau.

  Kuondolewa kwa Kimweri kumekuja mwaka mmoja baada ya wakala hiyo, kuunganishwa na Kurugenzi ya Ufundi na Umeme katika Wizara ya Miundombinu.

  Hata hivyo ilipobadilishwa, kurugenzi na wakala hiyo ilihamishiwa katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk John Magufuli.Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zilisema Kimweri amehamishiwa katika makao makuu ya Wizara ya Ujenzi kwa kazi nyingine.

  Taarifa hizo zilisema, mabadiliko hayo yamemgusa pia Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam , aliyefahamika kwa jina la Lyatuu ambaye amehamishiwa katika Mkoa wa Kigoma, kutokana na kile kilichoelezwa ni kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za upotevu wa fedha katika wakala hiyo.


  Hata hivyo alipoulizwa kuhusu habari hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo, alisema hakuwa nazo kwa sababu alikuwa nje ya ofisi.Ntemo alisema kama kuna kitu kama hicho asingeshindwa kujua.

  "Mimi sijasikia taarifa hizo. Kama kungekuwa na kitu cha aina hiyo, kisingekuwa cha siri, lakini kwa kweli sijui chochote," alisema.

  Taarifa zaidi zilisema mbali ya Meneja wa TBA wa Mkoa wa Dares Salaam Meneja wa Mwanza, Michael Nsangalo amechukua nafasi ya Lyatuu na kwamba, taarifa rasmi za mabadiliko hayo zinatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa

  Pamoja na majukumu mengine, wakala wa majengo ndiyo msimamizi mkuu wa majengo ya serikali na kwa sasa amekuwa kiungo muhimu cha kukusanya madeni ya nyumba za serikali.Mchakato wa kuuzwa kwa nyumba hizo umekuwa ukilalamikiwa na umma kwamba haukuzingatia maslahi ya taifa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  TBA kuna mambo mwenye taarifa za ziada asiache kutupasha khabari............
   
 3. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,998
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  du kigoma hii hatari jamani ,,,hv haya mambo ya kuhamishiwa kigoma au mtwara huwa yanasaidia kweli............
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  duh! hii habari iliishia wapi? maana naona jina la huyo bwana linaendana na jina langu,
  kinachonishangaza hata mimi ni architect, what a coincidence!!!
   
Loading...