Maneno haya ni sawa lakini pia nitofauti kutegemeana na mazingira fulani, Mf: neno chukua unaweza kulitumia kumpa mtu kitu ambacho kitakua cha kwake kabisa, hata kama hakuna lolote mliloongea na kukubaliana kwanza. Tofauti na neno shika, kama hatujakubaliana kwamba nitakupa kitu fulani kiwe chako, Mimi nikisema hebu shika (labda nimekupa kitu fulani) huwezi kufanya maamuzi ya kukifanya chako, mfano hela ukazitumia, mimi nilikwambia shika na sio chukua hivyo nitakudai tu.