Wazazi wangu wametokea sehemu tofauti kwa Mama yangu Kilimanjaro bibi yangu anakaa karibu na barabara ya lami, ana maji, umeme na nyumba ndogo ya matofali na haya yapo zaidi ya miaka 25 sasa. Kwa baba yangu vijijini lushoto rangwe hakuna maji, hakuna barabara hata ya ngeda, hakuna umeme ingawa ni kuzuri zaidi kimazingira, kwa kilimo na mambo mengine. Bibi yangu alivyoenda kwa babu zetu hakuamini kulivyo nyuma. Cha kushangaza ni kwamba watu wa kule bado wanasema CCM itawaletea mandeleo!! wakati kwa bibi yangu kumekuwa na upinzani kwa miaka zaidi ya kumi na tano kuanzia wakati wa Mrema. Maendelo gani bila shule, maji, umeme, barabara je serikali imefanya nini hasa bado nashangaa