Tofauti ya neno Christmas na Xmas

Wakuu habari za jioni!

Nimeona nitoe ufanunuzi juu neno sahihi kati ya hayo tajwa kwenye kichwa cha Uzi huu.

Christmas ni muunganiko wa maneno mawili yaani Christ na neno la pili mass likiwa na maana ya kusanyiko la kristo.

Neno la pili xmass likiwa na maana ya kupiga uwepo wa Christmas, na neno hili hutumika na mpinga kristo kwa lengo la kupotosha wasio na ufahamu.

Unapoandika Xmas iwe kwa kujua au kutokujua ktk ulimwengu wa roho unakuwa umemsaidia kazi mpinga kristo.

Niombe kwa wale waliokuwa wanaandika Xmas pasipo kujua basi waache na badala yake waandike Christmas.

Xmass SIYO kifupi cha neno Christmas Bali ni kinyume cha Christmas.

Zaidi niwatakie wana jf wote sikukuu njema ya christmas.

Mbarikiwe sana!
Mkuu elyza kuna uhusiano mkubwa sana kati ya dini na elimu.
Yaani unapokuwa umekamata "dini" fulani bila kuwa na "elimu" yake,unaweza kupepesuka sana kiimani na kupotosha watu.

Ndio maana kuna umuhimu kwa wafundisha dini na wahubiri walau kuwa na elimu ya "Falsafa" na "Taihudi"(Theology).Hii inasaidia "Reasoning and Logic"...Wakati Taihudi inakupa nafasi ya kujua maandiko na chimbuko lake.

Hebu tazama maelezo ya kina juu ya neno "Xmass na Chrismass" hapa chini

UFAFANUZI WA MANENO CHRISTMAS NA X-MAS
Kwa leo nina jambo moja la kuweka sawa. Vijana kadhaa wameniomba nitoe maelezo kuhusiana na maneno “CHRISTMAS” na “X-MAS” maana wanachanganywa na wenzao. Kifupi, maelezo yanayosambazwa kwenye mitandao yetu ni kwamba “Christmas” ni sahihi na “X-mas” siyo sahihi. Maelezo haya yanayosambazwa si sahihi, ni ya uongo.


Tukianzia kwenye maneno hayo, kwa karibu kabisa tunarudi kwenye maneno ya lugha ya Kiingereza cha enzi tatu: Kiingereza cha zamani, Kiingereza cha enzi ya miaka ya kati (karne 5 hadi15) na Kiingereza cha siku hizi.

Kwa Kiingereza cha zamani “Christmas” ilitamkwa “Cristes maesse” na maana yake ilikuwa “Christ’s festival” yaani sikukuu ya Kristo.

“Crist” ndiyo “Christ” ndiyo Kristo. Kristo maana yake “Mpakwa” ndiyo inayotafsiri jina la Kiebrania (lugha ya Wayahudi) “Meshiah”, yaani “Mpakwa wa Bwana” . “Meshiah” ndiyo tunayotamka sisi Waswahili kama Masiya au Masiha.

Neno “maesse” maana yake “festival” yaani sikukuu au sherehe. Katika Kiingereza za enzi ya kati “Cristes maesse” ilinyooshwa na kuwa “Cristemas” ndipo katika Kiingereza cha siku hizi ikafika kutamkwa na kuandikwa “Christmass”.

Yaani hapa tunacheza na maendeleo ya lugha ya Kiingereza katika matamshi na maandishi tu. Hadi hapo nadhani nimeeleweka.

Lakini suala la CHRISTMAS na X-MAS linarudi kwenye lugha ya Agano Jipya ndiyo Kigiriki au Kiyunani. Jina hilo “Crist” au “Christ” limetoholewa kutoka jina “CHRISTOS” ndiyo Kristo (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni).

Walatini (watu wa Dola ya Rumi) wakatamka “CHRISTUS” ndiyo Kristu (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni). “Christos” maana yake ni Mpakwa, Masiya au Masiha. Masiya au Masiha yenyewe inatoholewa kutoka jina la Kiebrania “Meshiah” kama nilivyoonesha hapo juu. Waingereza hutohoa “Meshiah” na kuandika na kutamka “Messiah”.

Kumbe katika Kigiriki au Kiyunani, “CHRISTOS” huandikwa kwa herufi ndogo "Χριστός” na kwa herufi kubwa “XPICTOC” au “ΧPIΣTOΣ” au kwa sanaa “XPISTOS”. Katika Kigiriki hiyo “X” siyo “eksi” bali ni “ch” na hiyo “P” siyo “pi” bali “r”. Hivi kwa Kigiriki “XPI” husomwa “Chri.”

Halafu, kutokana na herufi “X” na “P” kusimama mwanzoni mwa jina “XPISTOS” au "XPICTOC", Wakristo wa mwanzo walizitumia herufi hizo mbili kufupisha jina “CHRISTOS” hivyo wakawa wanaandika wakibebanisha “X” na “P” na kuzaa alama moja maarufu sana mnayozoea kuiona kwenye nguo za misa au vitambaa vya altareni na kwenye vitabu. Ni alama ya “P” iliyokatwa mguuni kwa mstari -- au X.
(Poleni, hapa nashindwa kuichora. Herufi za Kigiriki zinagoma).Alama hizi huwa altaren,katika mavazi na vifaa vya kanisa.


Kwa maelezo haya basi, “X-MAS” si neno tofauti na “CHRISTMAS”. Ni neno lile lile isipokuwa badala ya kuandika CHRIST kirefu watu wanafupisha kwa X tu. Ndipo inapotokea X-MAS mahali pa CHRISTMAS. Hivyo hiyo “X” ya mwanzoni haimaanishi “mkasi” wenye maana ya “kukata” au “hakuna” bali “X” yenye kufupisha jina “CHRISTOS” na “MAS” huko mwishoni kumaanisha “SIKUKUU” au “SHEREHE”.

Kwa hiyo, asiwadanganyeni mtu wala asiwababaisheni mtu kwamba “X-MAS” maana yake “HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO” eti kwa vile “MAS” ni neno la Kigiriki linalomaanisha “MKUSANYIKO”. Hakuna neno la Kigiriki MAS linalomaanisha MKUSANYIKO.

Iweni na amani, vijana. Hata mtu akilazimisha maneno ya Kigiriki maneno yote yanayokaribiana na MAS japo kwa maandishi na matamshi hakuna neno lenye maana ya mkusanyoko.

Tazama maneno yaliyopo ni “μασάομαι” lenye maana ya kuuma, kung’ata, “μαστιγόω”lenye maana ya mchapo wa kiboko au kuadhibu, “μαστίζω”lenye maana ya kuchapa, “μάστιξ” lenye maana ya pigo la mjeledi na maradhi na “μαστός” lenye maana ya kifua.

Kama msomavyo hapa katika maneno haya hakuna neno linalomaanisha “MKUSANYIKO”.
Basi, vijana kuweni na amani. X-MAS si neno tofauti na CHRISTMAS. Ni neno lile lile isipokuwa badala ya kuandika CHRIST kwa urefu watu wanafupisha kwa X tu.

Nawatakieni maandalizi mema ya Krismasi au Noeli.
Kwisha kumaliza somo hili la lugha ya Kiingereza na Kigiriki naomba kuwaongezea mambo kidogo.
Majina: sikukuu hii huitwa pia Kuzaliwa (Nativity) au Yule.

Ni sikukuu ya utamaduni wa Kikristo. Maana yake ni kukumbuka na kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Na kwa vile ni shauri la Mungu kutupatia sisi wakosefu zawadi ya Mkombozi, katika kuadhimisha sikukuu hii zawadi hutawala. Ni sikukuu inayosherehekewa kwa mikusanyiko, upambaji wenye ishara nyingi kama vile miti ya Krismasi na dhifa za keki, kula na kunywa pamoja.

Tarehe ya kuadhimisha katika Kanisa la Magharibi na baadhi ya Makanisa ya Mashariki pamoja na walimwengu wengine ni tarehe 25 Desemba. Lakini katika baadhi ya Makanisa ya Mashariki huadhimishwa tarehe 7 Januari. Na katika makanisa ya Kiarmeni huadhimishwa tarehe 6 Januari.
KILA LA HERI KWENU NYOTE!

Cc: Mwanga Lutila Otorong'ong'o
 
Wakuu habari za jioni!

Nimeona nitoe ufanunuzi juu neno sahihi kati ya hayo tajwa kwenye kichwa cha Uzi huu.

Christmas ni muunganiko wa maneno mawili yaani Christ na neno la pili mass likiwa na maana ya kusanyiko la kristo.

Neno la pili xmass likiwa na maana ya kupiga uwepo wa Christmas, na neno hili hutumika na mpinga kristo kwa lengo la kupotosha wasio na ufahamu.

Unapoandika Xmas iwe kwa kujua au kutokujua ktk ulimwengu wa roho unakuwa umemsaidia kazi mpinga kristo.

Niombe kwa wale waliokuwa wanaandika Xmas pasipo kujua basi waache na badala yake waandike Christmas.

Xmass SIYO kifupi cha neno Christmas Bali ni kinyume cha Christmas.

Zaidi niwatakie wana jf wote sikukuu njema ya christmas.

Mbarikiwe sana!

Acha uongo wewe, christmass ni sherehe ya Wakatoliki, ndio waliyoianzisha, wao ndio wanajua Kuwa hakuan tofauti ya Christmass na Xmass wewe nani aliyekufundisha hiyo tofauti?

Watafute wenye sherehe yao Wakatoliki wakufafanulie kabla haujakuja kupost uongo humu
 
Mungu endelea kuipigania JF idumu milele na milele ili elimu kama izi tuzidi kuzipata waja wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom