Tofauti ya neno Christmas na Xmas

Mpingaji wa kitu gani..??

Xmas ni Sawa na Christmas hakuna tofauti...
Tofauti ipi ila kwakuwa unamsaidia baba yako ibilisi utaka kulazimisha kuwe hakuna tofauti hayo ni maneno mawili yenye maana kinzani
 
Wakuu habari za jioni!

Nimeona nitoe ufanunuzi juu neno sahihi kati ya hayo tajwa kwenye kichwa cha Uzi huu.

Christmas ni muunganiko wa maneno mawili yaani Christ na neno la pili mass likiwa na maana ya kusanyiko la kristo.

Neno la pili xmass likiwa na maana ya kupiga uwepo wa Christmas, na neno hili hutumika na mpinga kristo kwa lengo la kupotosha wasio na ufahamu.

Unapoandika Xmas iwe kwa kujua au kutokujua ktk ulimwengu wa roho unakuwa umemsaidia kazi mpinga kristo.

Niombe kwa wale waliokuwa wanaandika Xmas pasipo kujua basi waache na badala yake waandike Christmas.

Xmass SIYO kifupi cha neno Christmas Bali ni kinyume cha Christmas.

Zaidi niwatakie wana jf wote sikukuu njema ya christmas.

Mbarikiwe sana!
Tukianzia kwenye maneno hayo, kwa karibu kabisa tunarudi kwenye maneno ya lugha yaKiingereza cha enzi tatu: Kiingereza cha zamani, Kiingereza cha enzi ya miaka ya kati(karne 5 hadi15) na Kiingereza cha siku hizi.

Kwa Kiingereza cha zamani “Christmas” ilitamkwa “Cristes maesse” na maana yakeilikuwa “Christ’s festival” yaani sikukuu ya Kristo.

“Crist” ndiyo “Christ” ndiyo Kristo. Kristo maana yake “Mpakwa” ndiyo inayotafsiri jina la Kiebrania (lugha ya Wayahudi) “Meshiah”, yaani “Mpakwa wa Bwana” . “Meshiah” ndiyotunayotamka sisi Waswahili kama Masiya au Masiha.

Neno “maesse” maana yake “festival” yaanisikukuu au sherehe. Katika Kiingereza za enziya kati “Cristes maesse” ilinyooshwa na kuwa “Cristemas” ndipo katika Kiingereza cha siku hizi ikafika kutamkwa na kuandikwa “Christmass”.

Yaani hapa tunacheza na maendeleo ya lugha ya Kiingereza katika matamshi na maandishi tu. Hadi hapo nadhani nimeeleweka.

Lakini suala la CHRISTMAS na X-MAS linarudi kwenye lugha ya Agano Jipya ndiyo Kigiriki au Kiyunani. Jina hilo “Crist” au “Christ”limetoholewa kutoka jina “CHRISTOS” ndiyo Kristo (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni).

Walatini (watu wa Dola ya Rumi) wakatamka “CHRISTUS” ndiyo Kristu (tukifupisha kwa kudondosha “s” ya mwishoni). “Christos” maana yake ni Mpakwa, Masiya au Masiha. Masiya au Masiha yenyewe inatoholewa kutokajina la Kiebrania “Meshiah” kama nilivyoonesha hapo juu. Waingereza hutohoa “Meshiah” na kuandika na kutamka “Messiah”.

Kumbe katika Kigiriki au Kiyunani, “CHRISTOS”huandikwa kwa herufi ndogo "Χριστός” na kwa herufi kubwa “XPICTOC” au “ΧPIΣTOΣ” au kwa sanaa “XPISTOS”. Katika Kigiriki hiyo “X” siyo“eksi” bali ni “ch” na hiyo “P” siyo “pi” bali “r”. Hivi kwa Kigiriki “XPI” husomwa “Chri.”

Halafu, kutokana na herufi “X” na “P” kusimama mwanzoni mwa jina “XPISTOS” au "XPICTOC",Wakristo wa mwanzo walizitumia herufi hizo mbili kufupisha jina “CHRISTOS” hivyo wakawawanaandika wakibebanisha “X” na “P” na kuzaa alama moja maarufu sana mnayozoea kuiona kwenye nguo za misa au vitambaa vya altareni na kwenye vitabu. Ni alama ya “P” iliyokatwa mguuni kwa mstari -- au X.
(Poleni, hapa nashindwa kuichora. Herufi za Kigiriki zinagoma).Alama hizi huwa altaren,katika mavazi na vifaa vya kanisa.

Kwa maelezo haya basi, “X-MAS” si neno tofauti na “CHRISTMAS”. Ni neno lile lile isipokuwa badala ya kuandika CHRIST kirefu watu wanafupisha kwa X tu. Ndipo inapotokea X-MAS mahali pa CHRISTMAS. Hivyo hiyo “X” ya mwanzoni haimaanishi “mkasi” wenye maana ya “kukata” au “hakuna” bali “X” yenye kufupisha jina “CHRISTOS” na “MAS” huko mwishoni kumaanisha “SIKUKUU” au “SHEREHE”.

Kwa hiyo, asiwadanganyeni mtu wala asiwababaisheni mtu kwamba “X-MAS” maana yake “HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO” eti kwa vile “MAS” ni neno la Kigiriki linalomaanisha “MKUSANYIKO”. Hakuna neno la Kigiriki MAS linalomaanisha MKUSANYIKO.

Iweni na amani, vijana. Hata mtu akilazimisha maneno ya Kigiriki maneno yote yanayokaribiana na MAS japo kwa maandishi na matamshi hakuna neno lenye maana ya mkusanyoko.

Tazama maneno yaliyopo ni “μασάομαι” lenye maana ya kuuma, kung’ata, “μαστιγόω”lenye maana ya mchapo wa kiboko au kuadhibu, “μαστίζω”lenye maana ya kuchapa, “μάστιξ” lenye maana ya pigo la mjeledi na maradhi na “μαστός” lenye maana ya kifua.

Kama msomavyo hapa katika maneno haya hakuna neno linalomaanisha “MKUSANYIKO”.
Basi, vijana kuweni na amani. X-MAS si neno tofauti na CHRISTMAS. Ni neno lile lileisipokuwa badala ya kuandika CHRIST kwa urefu watu wanafupisha kwa X tu.

Nawatakieni maandalizi mema ya Krismasi au Noeli.
Kwisha kumaliza somo hili la lugha ya Kiingereza na Kigiriki naomba kuwaongezea mambo kidogo.
Majina: sikukuu hii huitwa pia Kuzaliwa (Nativity) au Yule.

Ni sikukuu ya utamaduni wa Kikristo. Maanayake ni kukumbuka na kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Na kwa vile ni shauri la Mungu kutupatia sisi wakosefu zawadi ya Mkombozi, katika kuadhimisha sikukuu hii zawadihutawala. Ni sikukuu inayosherehekewa kwamikusanyiko, upambaji wenye ishara nyingi kama vile miti ya Krismasi na dhifa za keki, kula na kunywa pamoja.

Tarehe ya kuadhimisha katika Kanisa la Magharibi na baadhi ya Makanisa ya Mashariki pamoja na walimwengu wengine ni tarehe 25 Desemba. Lakini katika baadhi ya Makanisa ya Mashariki huadhimishwa tarehe 7 Januari. Na katika makanisa ya Kiarmeni huadhimishwatarehe 6 Januari.
KILA LA HERI KWENU NYOTE!
 
Toa upu.mbavu wako hapa...

Mada kama hii tumeshaijadili hapa JF..

Mods ondoeni huu uchafu haraka
sio ustaarabu jaribu kuheshimu mawazo ya mtu hatakama yanakuudhi basi kaa kimya. mana huna uhakika kua kila unachosema ww ni bora kwakua sio bora ila huoni mtu anakutukana wala kukupuuza basi ujue wanaona unahaki ya kusema na kutoa mawazo hata kama sio ya maana
 
ninyi nao hamuaminiki, juzi kuna mmoja kaja humu kuelezea jambo hili hili mbona mmetofautiana maelezo??
 
sio ustaarabu jaribu kuheshimu mawazo ya mtu hatakama yanakuudhi basi kaa kimya. mana huna uhakika kua kila unachosema ww ni bora kwakua sio bora ila huoni mtu anakutukana wala kukupuuza basi ujue wanaona unahaki ya kusema na kutoa mawazo hata kama sio ya maana
Kuna mawazo hapo au kinyaaa???
 
Wakuu habari za jioni!

Nimeona nitoe ufanunuzi juu neno sahihi kati ya hayo tajwa kwenye kichwa cha Uzi huu.

Christmas ni muunganiko wa maneno mawili yaani Christ na neno la pili mass likiwa na maana ya kusanyiko la kristo.

Neno la pili xmass likiwa na maana ya kupiga uwepo wa Christmas, na neno hili hutumika na mpinga kristo kwa lengo la kupotosha wasio na ufahamu.

Unapoandika Xmas iwe kwa kujua au kutokujua ktk ulimwengu wa roho unakuwa umemsaidia kazi mpinga kristo.

Niombe kwa wale waliokuwa wanaandika Xmas pasipo kujua basi waache na badala yake waandike Christmas.

Xmass SIYO kifupi cha neno Christmas Bali ni kinyume cha Christmas.

Zaidi niwatakie wana jf wote sikukuu njema ya christmas.

Mbarikiwe sana!
Iwe inapatiwa au inakosewa hakuna cha maana,kwasababu sikukuu yenyewe HAITAMBULIKI KTK BIBLIA.
 
Huu upuuzi mmeutolea wapi nyie wenye laana ya babu zenu...

Hii Xmas ni Sherehe ya Kikatoliki hivyo ni vyema kupata ufafanuzi kutoka kwa Wakatoliki sio kukurupuka
Ndio. Xmass ni sherehe ya kikatoliki. Ni uthibitisho mwingine kuwa ukatoliki ndiye mpinga-Kristo.
 
Kama X maana yake ni kupinga kila kitu, vipi kuhusu wale wachezaji kina Xavi Alonso na Xavi Hernandez nao wanapinga nini?

Nawaza tu!
 
Wakuu habari za jioni!

Nimeona nitoe ufanunuzi juu neno sahihi kati ya hayo tajwa kwenye kichwa cha Uzi huu.

Christmas ni muunganiko wa maneno mawili yaani Christ na neno la pili mass likiwa na maana ya kusanyiko la kristo.

Neno la pili xmass likiwa na maana ya kupiga uwepo wa Christmas, na neno hili hutumika na mpinga kristo kwa lengo la kupotosha wasio na ufahamu.

Unapoandika Xmas iwe kwa kujua au kutokujua ktk ulimwengu wa roho unakuwa umemsaidia kazi mpinga kristo.

Niombe kwa wale waliokuwa wanaandika Xmas pasipo kujua basi waache na badala yake waandike Christmas.

Xmass SIYO kifupi cha neno Christmas Bali ni kinyume cha Christmas.

Zaidi niwatakie wana jf wote sikukuu njema ya christmas.

Mbarikiwe sana!
Without source/s? No. Thank you!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom