8][/I]Vigenzo: ni sifa au ni njia ya kuingilia pahala,kwanza ukamilishe vigenzo ndio uingie au ukubaliwe,Mfano: Ili uingie chuo cha ufundi ni lazima uwe umefaulu Hesabu,Fiziksi, na kiengereza.
Masharti : ni Taratibu au mambo ambayo ni lazima kuyafanya,sikuzote huja baada yakigenzo, Mfano: mwanafunzi atakaekubaliwa anatakiwa aingie darasani saa 1 kamili asubuhi, kama hakufika kwa muda atafukuzwa skuli. kufukuzwa skuli sio kua kakosa vigenzo au sifa za kusoma bali ameshindwa kufuata taratibu za shule, ila sifa anazo.
Tukirudi kwenye mfano wako,Kigenzo cha kuoa ni sifa anayotakiwa mpangaji awenayo, lakini masharti ataambiwa adumishe usafi,alipe umeme na maji, usafi,kulipa umeme na maji sio sifa( vigenzo) bali ni taratibu za nyuma alopanga(masharti).