Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,472
- 4,771
baada ya timu yetu ya taifa kubolonga katika mashindano makubwa na kushindwa kupata nafasi ya kucheza michuano mikubwa ya afrika na kombe la dunia, na mashindano mbalimbali ya soka ulaya na kwengineko kuwa yamekwisha watanzania sasa wamerudi nyumbani kufuatilia kombe la kagame ambalo zamani lilijulikana kama klabu bingwa afrika mashariki na kati.
ni nadra kukuta makipa wenye viwango sawa wanakuwa timu moja na kugombea namba. hii imezoeleka kwa wachezaji wa ndani katika vilabu mbali mbali vya soka na ndo maana wahenga walisema "kuku mmoja hachinjwi na watu wawili". lakni kwa yanga imeonekana kuwa si kitu cha kustusha kwani imetumia gharama nyingi kumnyakuwa kipa kutoka kwa hasimu wake simba bwana juma kaseja al maaruf kama ilala one.
leo napenda kuzungumzia kwa kifupi tu kinyang'anyiro cha kugombea lango katika klabu ya yanga kati ya tanzania one ivo mapunda na ilala one juma kaseja. tathmini za haraka haraka zinaonyesha kuwa yanga mpaka sasa imeshacheza mechi mbili katika kombe hili na kujikusanyia pointi 4, magoli matatu ya kufunga na mawili ya kufungwa.
mabao hayo mawili ya kufungwa alifungwa ilala one juma kaseja, na yote yakitokana na mipira iliyotokana na adhabu, kitu kilichopelekea baadhi ya washabiki wa yanga kusema kama kaseja kaonyesha udhaifu wa kufungwa mipira iliyokufa je itakuwaje siku akipata mashambulizi ya nguvu ya mipira iliyo hai?
na sasa wanajiuliza wakati ivo ameweza kudaka na kuhakikisha yanga wanaondoka na ushindi kitu ambacho ilala one kaseja alishindwa kukifanya basi kwa nini asiaminiwe ivo kupewa milingoti?
kivumbi hiki cha kugombea namba kinaendelea, na kuna matabaka yameshaanza kujitenga mengine yakimtaka ivo huku yakisema "nazi ya muda mrefu mtini ndo iliyo komaa na tayari kwa kuliwa" na mengine yanamtetea kaseja yakisema "hata mbuyu ulianza kama mchicha" na mimi nasema "the sagga continua" na iko siku tutakamilisha ule msemo wa wahenga kuwa "dobi wa kweli utamjua siku akipewa nguo nyeupe" kwani tutamjua wa ukweli ni yupi na kanjanja ni yupi.

Last edited: