Tofauti ya Daktari na Tabibu

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,578
7,281
Kumekuwa na mkanganyiko kati ya hizo kada mbili. Ubishi unakuja kwenye swali:" Je, mhitimu wa diploma nae ni daktari?". Nimecheck maandishi ya Ofisi ya Rais Tamisemi na pia yale ya Benjamin Mkapa Foundation na nilichogundua.

1. Daktari hutumika kuwaita wale wenye degree ya MD na nyingine kama hiyo
2. Tabibu ndiyo kiswahili cha Clinical Officer na
3. Tabibu Msaidizi ni Clinical assistant

Zamani hakukuwa na huu mkanganyiko kila mtu alijua nafasi yake na sisi laymen tulijua nani ni nani. Sikuwahi kumsikia yeyote akimuita mzee wangu daktari, siku zote ameitwa tabibu. Sasa naona kama Tanzania tunajenga utamaduni mpya. Ni vizuri tujitafakari.
 
Kwa uelewa mchache...Daktari aweza kuwa msomi wa elimu mbali mbali.

KM:- Dr. in Finance, Dr. In Economy nk nk.. ila Tabibu ni WA Health
 
Kwanza ufanano wao mkuu ni kwamba wote wanatibu.

Tofauti yao kubwa ni viwango vyao vya elimu, mmoja ana degree(daktari) na mwingine ana diploma(tabibu).

Daktari ni Tabibu pia, lakini Tabibu anaweza asiwe Daktari.

Kibongo huu mkanganyiko unaweza usiwe na issue sana sababu 80% ya population ni laymen.

Kwa nchi zilizoendelea ama ambazo zina high literacy rate hizi ni qualification mbili tofauti kabisa sababu wateja wanahitaji cha kwanza ujitambulishe wewe ni nani kabla hawajaanza kukueleza shida zao.

Na mteja anataka kama wewe ni tabibu basi useme ni tabibu, kama ni daktari useme ni daktari, kama ni specialist useme ni specialist na kama ni super-specialist basi useme.

Na wateja wanajua limit ama uwezo wa mwisho wa kila mtu iwe tabibu ama daktari ama specialist. Sasa ukijifanya wewe mjuaji sana basi hauchukui round mteja anaku-sue.
 
Mazowea -Je ni sawa?
Sio sawa..

Kimtaani mtaani sawa, ila inapokuja kwenye uandishi basi muandishi ni lazima aandike kile kinachotakiwa, kama ni tabibu basi waseme tabibu na kama ni daktari basi waseme daktari.
 
Back
Top Bottom